Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu saba kwa
tuhuma za kujihusisha na matukio ya uhalifu ikiwa ni pamoja na
unyang’anyi wa kutumia silaha. Watuhumiwa wamekamakwa katika matukio
tofauti jijini Dar es Salaam kufuatia oparesheni kali inayoendelea ya
kuwasaka wahalifu wa makosa mbalimbali.
Katika
tukio la kwanza mnamo tarehe 03/06/2015 majira saa 08:00HRS maeneo ya
Tabata Kinyerezi mtaa wa Kibaga askari wa kikosi kazi (TASK FORCE)
walimkamata mtuhumiwa HEMED S/O HASSAN MRISHO @ BUDA, Miaka 31,
Mfanyabiashara, Mkazi wa Tabata Kinyerezi, akiwa na Bunduki aina ya SMG
iliyofutwa namba zake ikiwa na risasi 10. Mtuhumiwa alikamatwa kufuatia
taarifa toka kwa msiri kuwa anajihusisha na uhalifu wa kutumia silaha.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mtuhumiwa HEMED S/O HASSANI
akishirikiana na wenzake ambao wanasakwa, wanajihusisha na unalifu wa
kutumia silaha. Atafikishwa mahakamani mara uchunguzi utakapokamilika.
Katika
tukio lingine, mnamo tarehe 01/06/2015 majira ya saa 02:00 huko maeneo
ya Tegeta Mashimo ya Kokoto, Polisi walifanikiwa kukamata risasi 49 za
bunduki aina ya Short Gun zikiwa katika mfuko wa Rambo baada ya
kuwakurupua vijana wanaokaa katika vijiwe vya mashimoni hayo.
Hii ni
kufuatia kundi la vijana wanaokadiriwa kufikia kumi wakiwa na mapanga
na silaha nyingine za jadi kuvamia nyumba ya VERONICA D/O SABATH MAMBOYA
na kuiba vitu mbalimbali vikiwemo vitambulisho, TV, Laptop na Pesa
taslim TSHS. 300,000/=. Baada ya tukio mlalamikaji alitoa taarifa kituo
cha polisi Kawe na ufuatiliaji ulianza mara moja. Polisi walifanikiwa
kuwakamata vijana watatu ambao walionyesha vijiwe vya vijana wenzao.
Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam (DCP), Simon Sirro akiwaonesha risasi zilizokamatwa katika oparesheni hiyo. |
Wakati
polisi wakijiandaa kuwakamata walikurupuka na kukimbia ndipo polisi
walifanya upekuzi wa eneo hili na kufanikiwa kupata risasi hizo zikiwa
katika mfuko wa plastiki maarufu kama “mfuko wa Rambo”. Watuhumiwa
waliokamatwa ni pamoja na
1. RAMADHANI S/O NUHU, Miaka 20, Mkazi wa Kiwangwa.
2. ABED S/O SALUM, Miaka 18, MKAZi wa Kibaoni.
3. HANIF S/O HAMIS, Miaka 19, MKAzi wa Tegeta.
KUKAMATWA KWA ROLA 15 ZA NYAYA ZA UMEME PAMOJA NA WATUHUMIWA SABA.
Katika
hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum limefanikiwa kukamata
kontena lenye namba 00LU2876031 likiwa na rola 15 za nyaya (zenye
thamani ya shilingi 150,000,000/= milioni mia moja na hamsini)
zilizoibwa tarehe 26/02/2015 zikiwa zinasafirishwa kuelekea mkoani
Kagera kwa ajili ya mradi wa umeme vijijini (REA). Baada ya wizi wa
kontena hilo kesi ilifunguliwa kituo cha Polisi Buguruni na watuhumiwa
watano walikamatwa na kufikishwa mahakamani.
Wakati
upelelezi ukiendelea ndipo tarehe 25/05/2015 Polisi Buguruni walipokea
taarifa toka kwa msiri kwamba huko maeneo ya Kibamba mtaa wa Kibwegele
wilaya ya Kimara Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kuna kontena limefichwa
katika kiwanda cha kutengeneza matofali.
Askari
wa kikosi kazi walifika eneo la tukio na kukuta kontena hilo lenye
namba 00LU2876031 na walimhoji mlinzi wa eneo ili kupata mmiliki wa eneo
na kontena hilo. Ilipofika saa 23:55hrs mmiliki wa eneo hilo aitwaye
DONESIA D/O AIDAN @ KIFYOGA, Miaka 40, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mbezi
Makabe ambaye ni mtuhumiwa wa sita.
Taratibu
zilipokamilika kontena hilo lilifunguliwa ndipo zilipokutwa rolla za
nyaya zipatazo 15 kati ya 17 zilizokuwepo katika kontena hilo siku
lilipokuwa linasafirishwa. Tarehe 27/05/2015 majira ya saa 00:30hrs
maeneo ya Kimara mwisho alikamatwa mtuhumiwa mwingine wa saba PROSPER
S/O MTEI, Miaka 43, Mfanyabiashara na upelelezi unaendelea ili aweze
kuunganishwa na watuhumiwa wengine katika kesi ya msingi.
KUKAMATWA KWA BASTOLA MOJA NA MAGANDA YA RISASI
Mnamo
tarehe 28/05/2015 majira ya saa 23:00hrs maeneo ya Kiwalani Minazi
Mirefu Kata ya Ilala WIlaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Polisi
walifanikiwa kukamata silaha Bastola yenye nambari 05532 pamoja na
maganda mawili ya risasi aina ya SMG katika eneo la tukio baada ya
majambazi kuitelekeza mara walipozingirwa na wananchi waliotaka
kuwakamata.
Majambazi
hao walikuwa wamefanya tukio la uporaji maeneo ya vingunguti wakitumia
pikipiki mbili ambapo moja ina namba za usajili MC610 ABU aina ya Boxer
rangi nyekundu ambayo pia waliipora kwa mtoa taarifa. Aidha katika tukio
hilo pia majambazi hao walimpiga mtoa taarifa na kitako cha bunduki
waliyokuwa nayo kisha kumpora pikipiki hiyo na pesa taslim shilingi
300,000/= Hata hivyo majambazi hao walifanikiwa kutoroka. Polisi kwa
kushirikiana na wananchi waliweza kuikamata pikipiki hiyo.
KUKAMATWA KWA VIPANDE 20 VYA PEMBE ZA NDOVU.
Katika
oparesheni iliyoendeshwa tarehe 25/05/2015 na idara ya INTERPOL jijini
Dar es Salaam ya kukamata magari, madawa ya kulevya na uhalifu mwingine.
Ilipofika majira ya saa 18:00hrs maeneo ya Kimara Suka ambapo kutokana
na foleni ya magari iliyosababishwa na ukaguzi wa magari katika zoezi
hilo alishuka kijana mmoja mwenye umri kati ya miaka 39- 45 kwa dhumuni
la kukodi pikipiki.
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida baada ya kuwaona askari wa unifomu kijana
huyo alitupa kifurushi alichokuwa nacho na kukimbia. Askari walilichukua
hilo furushi na kulipekuwa na kukuta kuna meno ya tembo vipande
ishirini pamoja na nguo kuku. Kielelezo kilipelekwa kituo cha Polisi
Mbezi na kufunguliwa jalada la uchunguzi KMR/PE/67/2015.
KUKAMATWA KWA MLIPUKO, VIFAA VYA KUVUNJIA, DAWA ZA KULEVYA PAMOJA NA MTUHUMIWA.
Tarehe
04/06/2015 majira ya saa 10:00hrs maeneo ya Chamazi ulifanyika msako
mkali wa kupambana na uhalifu na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa MICHAEL
S/O KASAMBALE, Miaka 28, Mkazi wa Chamazi akiwa na mlipuko mmoja na
vifaa vya kuvunjia. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani upelelezi
utakapokamilika. Aidha mtuhumiwa huyo amekamatwa na kete kadhaa za
madawa ya kulevya.
KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA AKIWA NA BASTOLA BANDIA
Polisi
wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa JACOB S/O NATHANIEL MWETA, Miaka 30,
Mfanyabiashara, Mkazi wa Kimara ambaye alikuwa anaitumia kutishia watu
kisha kupora. Mtuhumiwa ame kiri kuhusika katika matukio kadhaa ya
unyang’anyi hasa katika maeneo ya Tegeta na Kunduchi jijini Dar es
Salaam.
MAFANIKIO MENGINE YA OPARESHENI INAYOENDELEA JIJINI DAR ES SALAAM.
Aidha,
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na oparesheni ya
kupambana na uhalifu katika jiji la Dar es Salaam na kufanikiwa
kukamata vitu vifuatavyo:
1. Mitambo mitano (5) ya kutengeneza pombe ya moshi (Gongo)
2. JUmla ya lita mia mbili (200) za pombe ya Moshi (Gongo)
3. Gunia mbili za banghi.
4. Kupatikana na Mirungi box moja (1).
5. Kete kadhaa za madawa ya kulevya.
SIMON SIRRO – DCP
KNY. KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni