Askari
wa Jeshi la Zima moto nchini, Josephat John akieleleza matumizi ya
Kizimamoto wakati wa mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa watumishi wa
Ofisi ya Waziri Mkuu, mjini Dodoma tarehe, 21 Juni, 2015.
Afisa
Tawala, Ofisi ya Waziri Mkuu, Leah Kibassa, akifanya mazoezi ya kutumia
kizima moto wakati wa mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa watumishi wa
Ofisi hiyo, mjini Dodoma tarehe, 21 Juni, 2015.
Mkurugenzi
wa Idara ya Uratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi
Msuya (mwenye tai) akishuhudia, Salma Juma akikabidhiwa Kizima moto
kilichonunuliwa na washiriki wa mafunzo ya menejimenti ya maafa wa Ofisi
hiyo mjini Dodoma tarehe, 21 Juni, 2015, Kwa lengo la kuhamasisha
watumishi wa Ofisi hiyo kukabili majanga ya moto.
Watumishi
wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia mafunzo ya majanga ya moto wakati
wa mafunzo ya menejimenti ya maafa mjini Dodoma tarehe, 21 Juni, 2015.
Na. Mwandishi Maalum
Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa inaandaa mkakati wa elimu kwa umma wa
menejimenti ya maafa ambao utawatumia watu maarufu nchini wakiwemo wasanii wa
sanaa mbali mbali kwa lengo la kufikisha elimu kwa umma ya menejimenti ya maafa.
Akiongea wakati wa mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa watumishi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu, Mjini Dodoma mwishoni mwa wiki hii, Brig.Jen, Mbazi Msuya alibainisha
kuwa jamii ikielimishwa kikamilifu juu ya menejimenti ya maafa athari za maafa
zinapunguzika.
“Tunaposema menejimenti ya maafa tunazingatia, kuzuia, kukabili maafa na kurejesha
hali ya awali baada ya maafa kutokea. Kwa mantiki hii kama tunavyo elewa Wasanii
wanao uwezo wa kufikisha ujumbe kwa haraka, lugha nyepesi, kwa watu wengi na
kwa ujumbe mmoja, hili ndo linalotusukuma kufikiria kutumia hawa watu katika kutoa
elimu ya menejimenti ya maafa kwa jamii yetu” alisema Msuya.
Msuya aliongeza kuwa nchi yetu imekuwa ikikumbwa na majanga ya asili na yale
yanayosababishwa na binadamu, ambapo majanga yanayosababishwa na binadamu
kwa kiwango kikubwa jamii inaweza kuyakabili tu ikiwa elimu ya menejimenti ya
maafa hayo imemfikia kila mwanachi. Hivyo kwa kuwa wasanii wengi msingi wa kazi
zao za sanaa huaksi yanayojiri katika jamii yao hivyo hii itakuwa ni fursa kwao
kuijengea jamii uwezo wa kuyakabili maafa.
“Athari za Majanga yanayosababishwa na binadamu kama moto yanaweza kuzuilika
ikiwa menejimenti ya majanga hayo itatolewa kwa umma. Wananchi wakielimishwa
umuhimu wa kuwa na vizima moto majumbani mwao na katika vyombo vya moto
wanaweza kukabili majanga ya moto na hili litawezekana kwani tayari tunayo mikakati
ya mawasiliano ya kukabiliana na maafa ” alisisitiza Msuya.
Ofisi ya waziri Mkuu kupitia Idara ya Uratibu maafa tayari imeshaandaa Mkakati wa
Mawasiliano wa kukabiliana na maafa kwa mkoa wa Mtwara, Shinyanga na Dodoma
lengo ikiwa ni kila mkoa nchini kuwa na mkakati huo utakowezesha menejimenti ya
maafa kwa jamii ya watanzania. Aidha mkakati huo unabainisha kila mdau wa maafa
wajibu wake katika menejimenti ya maafa wakiwemo wasanii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni