Afisa masoko wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Bw Jimmy 
Kiwelu (kulia)  akiwa na   wafanyakazi  wenzake baada ya  kutwaa tuzo ya ubora ya Kitaifa katika  bidhaa za Asas Dairies Ltd  
Hii  ndio kampuni  iliyoweza  kushinda tuzo ya  ubora 
Medali  ,vyeti na  tuzo  ya ushindi  ambayo kampuni ya Asas Dairies Ltd imeshinda  tena  mwaka huu katika maonyesho ya maziwa mkoani Mara 
Vyeti na medali  tatu  ambazo kampuni   ya Asas Dairies Ltd imeshinda  tena kwa 
Baadhi ya  bidhaa za kampuni ya Asas Dairies Ltd zilizoshinda medali  
Na Matukiodaima Blog
BIDHAA
 na maziwa yanayotengenezwa na kampuni ya  Asas Dairies Ltd ya  mkoani 
Iringa kwa  mwaka  wa tatu  mfululizo  zimeendelea kushikilia tuzo ya 
ubora na  kuwa kampuni  bora kuliko  makapuni mengine ya maziwa hapa 
nchini .
Kampuni
 hiyo  ya   Asas Dairies Ltd ambayo ni  moja kati ya makampuni ya  
kizalendo nchini na moja kati ya makampuni yaliyopata  kupewa  tuzo  ya 
ulipaji  kodi mzuri na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imeshinda katika
 maadhimisho ya wiki ya maziwa mwaka  huu tena yaliyofanyika wilaya 
Babati mkoani Mara kwa  kushindanisha kampuni  zaidi ya 20.
 Akizungumzia
 ushindi  huo afisa masoko wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Bw Jimmy 
Kiwelu  alisema kuwa mbali ya kampuni  hiyo kuongoza kwa mwaka  huu 
wa tatu mfululizo bado  bidhaa  zake  nyingine  zimeendelea  kushinda 
medali mbali mbali na kuonyesha uwezo mkubwa wa kampuni  hiyo katika 
ubora.
Alisema
 baadhi  ya makampuni makubwa ambayo  yalipata  kuingia  katika 
mashindano  hayo ni  pamoja na Tanga Fresh, DarFresh,Kilimanjaro 
Fresh,Creamer Fresh,Cefa, Grand DeMom ya Engingteng, Nansinya ya Arusha 
 ,Nnronga  ya Kilimanjaro mengine  mengi.
 Alisema kuwa bidhaa  kwa  mwaka  huu kila kampuni  lilikuwa likishindanisha bidhaa zake tatu huku kampuni  yake Asas Dairies Ltd bidhaa  zake  zote  tatu  zilishinda na kupewa medali.
Pamoja na kushinda katika bidhaa hizo bado kampuni  hiyo ilinyakua  tuzo ya  jumla katika  ubora.
 Bw   Kiwelu 
 aliwataka  watanzania kuendelea  kuzipenda  bidhaa za Asas Dairies Ltd 
 kutokana na kuendelea kuongoza katika ubora na kuwa lengo  la kampuni 
hiyo  kuendelea kushinda  tuzo  za  ubora 
 Pia 
 alipongeza watanzania na watumiaji wa bidhaa za Asas Dairies Ltd 
kutokana na ushirikiano mkubwa  wanaombwa  kuihamasisha jamii   
kuendelea  kutumia maziwa hayo na  bidhaa nyingine za chini ya kampuni 
ya kizalendo ya Asas Dairies Ltd.
Bw Kiwelu  alisema mwaka huu  jumla ya Medali 9  zilikuwa  zikishindaniwa ila kampuni  Asas Dairies Ltd iliweza  kuongoza  kushinda medali 3 kati ya 9.
 Aliyekuwa mgeni rasmi tena kwa  mwaka  huu  Waziri
 wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani pamoja na  kupongeza 
mshindi  huyo wa jumla na washiriki  wengine katika maonyesho  hayo 
bado  alitaka makampuni zaidi  kuendelea  kushiriki maonyesho hayo 
kwani  yanasaidia  kutambua changamoto katika utengenezaji wa bidhaa 
bora .
Pia 
 alieleza  kufurahishwa na hatua  kubwa ya 
 kampuni  hiyo ya Asas Dairies  Ltd  kwa  kuendelea  kufanya  vizuri 
katika mashindano hayo ya ubora  wa maziwa nchini na kuwa  mbali ya kuwa
 ni  heshima ya kampuni na mkoa wa Iringa ila bado ni  heshima kwa 
Taifa  kuona kamapuni ya ndani yanaonyesha ufanisi  mkubwa katika bidhaa
 zake .





 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni