Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Jakaya Kikwete akiagana na
Balozi wa Canada hapa nchini,Alexandre Leveque baada ya maadhimisho
hayo,kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Umoja wa Mataifa(UN) hapa
nchini,Alvaro Rodriguez na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Felix Ntibenda.
Rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania ameonyesha kusononeshwa na mauaji ya watu wenye
ulemavu wa ngozi yanayoendelea nchini kwenye uso wa sura za kimataifa.
Rais
Kikwete aliyasema hayo jana kwenye kilele cha maadhimisho ya watu wenye Ualbino kuongeza
uelewa juu ya watu wenye ualbino pamoja na kupinga unyanyapaa, unyanyasaji na
mauaji ya Albino yaliyofanyika duniani kote mkoani Arusha mapema jana katika
viwanja vya sheik amri abeid.
Rais Kikwete
alisema kuwa matukio ya mauaji na ukataji viungo vya Albino imekuwa fedheha
kwake hasa anapotembelea nchi zingine .
“Naomba
niseme kuwa imani hizi za kusema eti kuwa kiungo cha binadamu mwenzako inaweza
kusababisha utajiri au kupata cheo hizi ni za kupiga vita kabisa kwani kila mtu
anajua kabisa chanzo cha mafaniki yoyote au utajiri ni kufanya kazi kwa bidii,
juhudi na ufanisi kazini” alisema Rais Kikwete.
Akijibu juu ya
ucheleweshaji wa utekelezaji wa kesi za mauaji, Rais Kikwete alisema kuwa jumla
ya watu 139 wamekamatwa na 15 wamepatikana na hatia ambapo 13 kati yao
wamehukumiwa kunyongwa lakini bado hawajanyongwa kutokana na msururu wa hatua
za kupitisha zoezi hilo kukamilika hivyo wavute subira kwani linafanyiwa kazi.
“Katika
msako ule tuliyoendesha kuanzia mwaka 2006 hadi2010 juu ya matukio haya,
tulifanikiwa kukamata watu 139 ambapo walipelekwa mahakamani na baadae watu 15
wakakutwa na hatia hivyo wawili kati yao wakapewa adhabu ya kawaida na 13
wakahukumiwa kunyongwa huku wengine wakiachiwa kwa kuonekana hawana hatia”
“Lakini
naomba niseme ndugu zangu kuwa kesi za mauaji si kesi ndogo hivyo huendeshwa
kwa mda mrefu ili kujiridhisha kuwa anaenyongwa ndie muhusika halisi wa kosa
isije kutokea akanyongwa mtu asiyehusika hivyo kuna mlolongo mrefu sana wa kesi
hizo hivyo tuvumiliane tu maana watu wawili karibu msururu wao unaisha na
adhabu zitatolewa”
Akizungumzia
swala hili, Rais Kikwete alionekana kama anampigia debe Waziri wa mambo ya
ndani Mathias Chikawe baada ya kusema kuwa waziri huyo kwakuwa ametangaza nia
ya kugombea urais, endapo atapata basi swala hili litakuwa limefika sehemu
salama.
Waziri Chikawe ebu njoo useme kidogo swala la mapambano ya albino lilipofikia kwani
naona pia umevuta fomu ya kugombea Urais na kama utapata naamini swala hili
litamalizika haraka, hivyo jamani kama akipata kuwa Rais wanchi.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni