|
Christian Bella akijimwaga jukwaani. |
Masaa
machache baada ya kukosa kitatanishi tunzo ya wimbo bora wa mwaka katika
Kili Music Awards Christian Bela (King of melodies) alipagawisha
wapenzi wa muziki mjini Tabora alipoporomosha bonge la show akiwa na
kundi zima la Malaika Band. Christian Bela alitarajiwa na wadau wa
muziki nchini kuwa angebeba tunzo hiyo bila ushindani mkubwa kutokana na
wimbo wake wa Nani kama mama ambao aliomshirikisha Ommy Dimpoz kutamba
sana katika vituo vyote vya redio na Runinga hapa nchini, lakini kama
kawaida ya tunzo hizo zinazosimamiwa na BASATA na kudhaminiwa na kampuni
ya utengenezaji bia ya Tanzania TBL zimekuwa zikilalamikiwa kila mwaka
huku waanadaaji wakioneka kuweka pamba mbichi masikioni. Tunzo hiyo ya
wimbo bora wa mwaka ilienda kwa wimbo wa Mwana wa msanii Ali Kiba.
Onesho hilo lilifanyika katika viwanja vya Bwalo la Polisi Tabora.
|
Bella akifanya yake jukwaani. |
|
Mashabiki wa Malaika Band wakpozi |
|
Hapo sasa! |
|
Baadhi ya mashabiki wakijmwaga! |
|
Music Producer Dula K kulia na msanii Masha Kay kushoto wakiwa na mdau. |
|
Wacha wee Benny Ngwasuma akijiachia |
Picha na habari na Mkala Fundikira TBN CENTRAL ZONE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni