Mahmoud
Ahmad Arusha
KATIBU wa
chama cha Mapinduzi wilaya ya Arusha , Feruzi Banno amewataka watiania ya
kuomba ridhaa ya Ubunge kupitia chama cha mapinduzi jimbo la Arusha , kuacha kampeni kabla ya
wakati .
Onyo hilo
amelitoa jana alipokuwa akizungumza na watia nia kumi na mbili kati ya kumi na
nane walioonyesha nia ya kugombea ubunge kupitia CCM.
Katibu
Feruzi, amewaambia watia nia hao kuwa Chama cha mapinduzi kina kanuni na
maadili ambayo kila mtia nia anapaswa kuyazingatia ili kuepuka asipoteze sifa
ya kuwa miongoni mwa wagombea watakaopitishwa na chama .
“NInawakumbusha
kila mmoja wenu kuzoifuata na kuzizingatia kanuni hizo na atakae kiuka atachukuliwa
hatua ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa kuwa amepoteza sifa’’,alisema Feruzi.
Alisema kuwa
chama kimeshapokea taarifa za kuwepo kwa baadhi ya wagombea kuanbza kampeni
kabla ya wakati na hilo likithibitika wataondolewa.
Aliwataka
watia nia wote kutokuchafuana wa
kupakana matope bali wazingatie taratibu.Akijibu maswali ya wanahabari kuwepo
taarifa za baadhi ya wagombea kuchapisha Tsheti na Vipeperushi ,Katibu, alisema
chama kinafuatilia nyendo za watia nia hao na ikibainika watachukuliwa hatua.
Banno
,alisisitiza kanuni na maadili ya uongozi katika uchaguzi
ndani ya chama hicho yanatakiwa kufuatwa na kila mtia nia na kuwa atakayekiuka
kanuni na taratibu za chama kwa kuanza kampeni mapema chama kitafuata
kanuni na taratibu za uchaguzi ndani ya chama kumwajibisha.
Alisema kuwa
Form ndani ya chama hicho zitaanza kutolewa June 15 na mwisho wa kurudisha form
za kuomba ridhaa ya ubunge ndani ya ccm ni June 19 saa kumi jioni na kura za maoni zitafanyika August 1 na
kuwataka atakayepitishwa kumuunga mkono kwa nguvu zao ilikuweza kulirudisha
jimbo kwenye mikono ya chama hicho.
Amewataka
watia nia hao Kimu Fute,David Rwenyagira,Justin Nyari,Philemon Mollel,Aziz
Nassoro,Deo Mtui,Edmund Ngemela,Mahmoud Said,Michael Sekajingo,Victor
Njau,Mustaf Panju na Aloice Kilimbo wawe na umoja, mshikamano na upendo na wawe
tayari kukabali matokeo na kumuunga mkono mgombea ambae atakuwa ameshinda.
Ametoa wito
kwa wanachama wengine wa ccm, wenye nia ya kugombea ubunge katika jimbo hilo
kujitokeza kwa wingi .Wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya kikao
hicho watia nia hao wamesema wameridhishwa na hatua ya katibu kuwakutanisha na
hivyo kufahamiana.
Akizungumzia
hatua hiyo, mgombea mmoja David Rwenyagira,
amesema utaratibu uliowekwa na
chama ni mzuri hivyo kila mgombea anapaswa kuuheshimu.Kwa upande wake Kim Fute,
amepongeza hatua hiyo na kuahidi kufuata taratibu na kanuni za ccm.
Kwa upande
wake Justin Nyari, yeye ameahidi kuzingatia kanuni na taratibu .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni