Muonekano
 wa nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha leo, 
wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa tano wa Wadau wa NSSF.
Mgeni 
rasmi kwenye Ufunguzi wa Mkutano wa tano wa Wadau wa NSSF, Waziri Mkuu, 
Mh. Mizengo Pinda akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,
 Mh. Joshua Nassary wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa 
Kimataifa wa AICC jijini Arusha leo. Kushoto ni Waziri wa Kazi na Ajira,
 Mh. Gaudencia Kabaka na kulia ni Mwenyekiti
 wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii 
(NSSF),Ndg. Aboubakar Rajab pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la 
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau.
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda na ujumbe wake wakiangalia burudani ya ngoma kabla ya kuingia ukumbini.
Sehemu wa Wadau wa Mkutano Mkuu wa tano wa NSSF wakishiriki kwa pamoja kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Waziri
 Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akitoa hotuba yake ya Ufunguzi wa Mkutano wa 
tano wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza 
leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.Mh. 
Pinda awewasihi wasomi nchini pamoja na watanzania  kuacha fikra ya 
kusubiri kuajiriwa mara wanapomaliza vyuo badala yake wajiajiri wenyewe 
ili waweze kukabiliana na changamoto za maisha.
Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudencia Kabaka akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda ili aweze kuufungua Mkutano wa tano wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Ndg. Aboubakar Rajab akitoa shukrani kwa Mgeni Rasmi, Wajumbe na Wadau walioshiriki kwenye Mkutano wa huo, ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akizungumza mapema leo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa tano wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo, kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha. Dkt. Dau amesema, NSSF kwa sasa imeanza kutoa mikopo kwa wajasiriamali na imeshatoa mikopo kwa wanachama wake yenye thamani ya Sh. bilioni 55.6.
Dkt. Dau akiendelea kuzungumza.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi wakifatilia Mkutano huo.
Mmiliki wa Hoteli ya Peacock, Mzee Joseph Mfugale akitoa ushuhuda wake wa ujasiriamali katika Mkutano wa tano wa Wadau wa NSSF, ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Mmiliki wa Kampuni ya SSTL Group, Bw. Almas Maige akitoa ushuhuda wake wa ujasiriamali katika Mkutano wa tano wa Wadau wa NSSF, ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Waziri
 Mkuu, Mh. Mizengo Pinda na Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudencia 
Kabaka wakisikiliza kwa umakini ushuhuda wa ujasiriamali uliokuwa 
ukitolewa na Mzee Joseph Mfugale pamoja na Bw. Almas Maige, wakati wa 
Mkutano wa tano wa Wadau wa NSSF, ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi
 Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau 
akifatilia hotuba ya Mgeni Rasmi, Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda.
Wadau wakifatilia Mkutano.
Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudencia Kabaka.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Makongoro Mahanga.
Mkutano ukiendelea.
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF, Bw. Aboubakar Rajab.
Dkt. 
Dau akisikiliza Ushuhuda wa ujasiriamali uliokuwa ukitolewa na Mzee 
Joseph Mfugale pamoja na Bw. Almas Maige, wakati wa Mkutano wa tano wa 
Wadau wa NSSF, ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Wadau 
wa Mkutano wa tano wa NSSF wakifatilia kwa umakini ushuhuda wa 
ujasiriamali uliokuwa ukitolewa na Mzee Joseph Mfugale pamoja na Bw. 
Almas Maige, leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Waziri
 Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya Muajiri bora Sekta ya Utali,
 kwa Afisa Mwajiri wa Hifadhi ya Grumeti, Bw. Som Kakiva.
Waziri
 Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya Ubora wa Sekta ya Afya, 
Meneja Muajiri wa Hospitali ya Agha Khan, Bi. Mary Mlay.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akishuhudia namna Kadi ya Wastaafu inavyofanya kazi kupitia ATM za Selcom zitakazokuwe maeneo mbali mbali nchini ili kuwawezesha wastaafu kujipatia Fedha zao za pensheni kwa haraka, wakati wa Uzinduzi wa huduma hiyo mpya itakayokuwa ikitolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Ndg. Aboubakar Rajab pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau.
Baadhi wa wawakilishi wa Mifuko ya Hifadhi za jamii.
Zawadi
 kwa Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudencia Kabaka kazi kubwa 
anayoifanya kusimamia na kuhakikisha Mifuko ya Hifadhi za Jamii inakuwa 
bora hapa nchini.
Zawadi kwa Mgeni Rasmi.
















































Hakuna maoni:
Chapisha Maoni