Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya Simu Tanzania (TTCL) imekabidhi mradi wa kuiunganisha matawi 12 ya
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika huduma za mawasiliano ya sauti,
intaneti pamoja na data ili kuviwezesha vituo hivyo kufanya kazi katika
mfumo wa kisasa kimawasiliano jambo ambalo litaboresha utendaji kazi wa
kampuni hiyo.
Akikabidhi
mradi huo leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa
kampuni ya TTCL, Peter Ngota alisema kwa sasa wamekamilisha kuyaunga
kimawasiliano ya kisasa matawi 12 ya kampuni ya bia Tanzania ambayo ni
pamoja na tawi kuu la Dar es salaam (HQ), Arusha, Moshi, Mwanza, Ubungo,
Mwenge, Konyagi, Masaki, Bukoba, Shinyanga, Iringa na tawi la Tanga.
Alisema
mfumo huo wa mawasiliano unaunganisha makao makuu ya ofisi na matawi
yake ambayo yako maeneo tofauti nchini kwa lengo la kurahisisha utoaji
na upokeaji wa Taarifa
(Data) huku ukiwa salama tofauti na mifumo mingine.
"...Katika
mfumo huu wa Multiprotocol Label Switching Virtual Private Network
(MPLS VPN), Tanzania Breweries Ltd inapata huduma ya sauti, intaneti
pamoja na data. Kwa huduma hizi TBL sasa iendelee kwa kasi kuboresha
mifumo ambayo itasaidia kuongeza tija katika utendaji kazi wake na kwa
wateja kwa ujumla," alisema Ngota.
Ofisa huyo Mkuu wa Masoko na Mauzo aliongeza kuwa kwa sasa TTCL ni
kampuni pekee yenye mtandao wa Mkongo (Fibre) ambao umesambaa nchi nzima
huku ukiwa chachu ya kuleta mabadiliko katika kutoa huduma kwa wananchi
na utendaji kazi wa jumla wa makampuni mbalimbali.
TTCL
imekuwa nguzo muhimu kwa Taasisi za kifedha (Kibenki), Balozi,
Mashirika, Wizara na taasisi za serikali, makampuni ya kimataifa na
binafsi katika kuboresha utendaji na uendeshaji wa shughuli zao
kisayansi na kukidhi viwango vya kimataifa.
TTCL
pia imefanikiwa kuunganisha wateja mbalimbali ikiwa ni pamoja taasisi na
ofisi za serikali; TAMISEMI, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Wizara
ya Fedha, Kampuniya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Bima la Taifa
(NIC).
Alisema
huduma hiyo ya mkongo pia imerahisisha kazi katika Hospitali ya
Muhimbili, Mwananyamala, Temeke, MOI, Bugando, KCMC pamoja na Hospitali
za Mkoa nchi nzima ikiwemo Zanzibar pia zinaendelea kuunganishwa kupitia
Mkongo wa TTCL kwa huduma bora za kiafya kupitia afya mtandao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya TBL, Kevin O'Flaherty
akipokea mradi huo alisema tayari wameanza kuona mafanikio makubwa baada
ya kuanza kutumia mfumo huo huku ukisaidia kukua kwa biashara yao
tofauti na awali.
Aidha
alisema kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayoendelea
kukua kila uchao kampuni hazina budi kufanya kazi kwa kutumia teknolojia
mbalimbali ili kuongeza ufanisi wa kazi na ubora hali itakayochangia
kukua pia kwa biashara zao. "...Tayari tumeanza kuona mafanikio tangu
kuanza kutumia huduma hii na tunaamini tutapata mafanikio zaidi, kwa
sasa unaweza kutofautisha na ilivyokuwa kabla ya kuanza kutumia MPLS
VPN," alisema O'Flaherty.*
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni