Erick Evarist
OHOOO!
Mchekeshaji maarufu Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amedaiwa
kupewa fedha za kampeni kutoka kwa wagombea wawili tofauti wa urais
2015, Bernard Membe na Stephen Wasira.
Chanzo makini kimepenyeza ubuyu kuwa, Steve hakuwa na msimamo wa
kumfanyia kampeni mgombea mmoja kwani Jumamosi iliyopita alilipwa na
kwenda mkoani Mwanza…

kwenda mkoani Mwanza kumuunga mkono Wasira alipokuwa anatangaza nia huku
pia akiwa ameweka kibindoni ‘mtonyo’ wa Membe.
“Jamaa amekula huku na huku. Jumamosi iliyopita aliwachukua wenzake
kina JB (Jacob Steven) na Ray (Vincent Kigosi) wakaenda Mwanza kwa
Wasira kumuunga mkono alipokuwa anatangaza nia. Wakati huohuo amelamba
mkwanja wa Membe ambapo Jumamosi hii (leo) anatarajia kwenda kumuunga
mkono nyumbani kwake Mtama atakapokuwa anatangaza nia,” kilisema chanzo
chetu.
Mwanahabari wetu alimtafuta Steve Nyerere ili kumsikia anazungumziaje
suala la yeye kudaiwa kufanya kampeni kwa wagombea wawili tofauti
wakati inaaminika kabisa msikie alichojibu:
“Watu wanashindwa kuelewa, Wasira aliniita mimi na wenzangu kama
rafiki na si kazi. Bila hiyana tuliamua kwenda na ndiyo maana pale
hutukuzungumza sababu tulikuwa kama waalikwa wengine.“Kwa Membe hiyo
haina kificho, nitakwenda na wenzangu kama kazi sababu ni kweli namuunga
mkono kitambo tu, si leo wala jana,” alisema Steve Nyerere.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni