Baadhi ya watumishi wa Tanapa wakiwa na Wahariri wa vyombo
mbalimbali vya Habari wakifatilia kwa makini hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa
Tanapa.
|
Waandishi Adam Ihucha(The East African)Paul Sarwat(Raia
Mwema)na Charles Ngereza(Radio One) wakiwa miongoni mwa waandishi waandamizi
wanaoshiriki Kongamano hilo jijini Mwanza.
|
Baadhi ya watumishi wa Tanapa wakiwa na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari wakifatilia kwa makini hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa. |
Wahariri wakibadilisha na mawazo |
SALAM ZA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA
NDUGU ALLAN KIJAZI KATIKA UFUNGUZI WA WARSHA YA
WAHARIRI WA HABARI TANZANIA, MWANZA, 29.06.2015
·
Ndugu
Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali nchini;
·
Ndugu
waandishi wa habari
·
Menejimenti
ya TANAPA
·
Mabibi
na Mabwana;
Napenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za
dhati kwenu Wahariri kutoka Vyombo mbalimbali vya habari nchini kwa kukubali
mwaliko wetu wa kuhudhuria Warsha hii nina imani kwamba munaelewa umuhimu wa
uhifadhi na sekta ya Utalii kwa maendeleo ya nchi yetu. Tunaelewa bayana majukumu
mazito mliyo nayo, lakini kwa heshima kubwa mmekubali kutenga muda wenu
kujumuika nasi. Tunawashukuru sana kwa moyo huo. TANAPA tutaendelea kuthamini ushirikiano huu
mnaoendelea kutuonyesha siku hadi siku.
Ndugu Wahariri na Waandishi wa Habari,
Utalii ni sekta mtambuka na inachochea ukuaji wa sekta nyingine ikiwa
ni pamoja na kilimo, usafirishaji wa anga na barabara, huduma za fedha, huduma
za chakula na malazi kudorora kwa sekta nyingineazi. Hivyo kudorora kwa sekta hii huchangia kwa
kiasi kikubwa kudorora kwa sekta nyingine.
Aidha, hadi sasa, Utalii unaongoza katika kuingiza fedha za kigeni ikiwa
ya kwanza na kufuatiwa na sekta ya madini na kilimo. Kwa na
kwa ujumla unachangia asilimia 17.5 ya Pato la Taifa lakini tathmini inaonyesha
sekta hii inaweza ikachangia zaidi ya 30% ya pato la Taifa. Asilimia zaidi ya 80 ya utalii nchini ni
utalii wa kutembelea kwenye Hifadhi za Taifa, na hii inaonyesha kuwa hifadhi
hizi ni muhimu kwa ustawi wa taifa letu.
Ni zaidi ya mara tatu ya idadi ya wanaotembelea Hifadhi hizi.
Ndugu Wahariri,
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) linayo dhamana
ya kusimamia maeneo yote yaliyotengwa kisheria kama Hifadhi za Taifa nchini.
Dhamana hii tuliyopewa na nchi ni kubwa inayohitaji ushirikishwaji wa wadau
mbalimbali. Hivyo,TANAPA imekuwa ikijitahidi sana kuinua uhifadhi katika maeneo mengi tuliyokabidhiwa
na Serikali. Mfano wa maeneo hayo ni Saadani, Mkomazi na Kitulo. Maeneo haya
yalikuwa na hali mbaya sana ya kiuhifadhi kabla hayajakabidhiwa kwa TANAPA,
lakini kwa sasa maeneo hayo ni mazuri na yanaanza kuvuvutia wageni na idadi ya
wanyama inaongezeka hasa katika Hifadhi za Saadani na Mkomazi.
Ndugu Wanahabari,
Maeneo yaliyo chini ya Hifadhi za Taifa yana faida nyingi za kiikolojia
(ecosystem services) kama vile kuwa vyanzo vya maji (mfano; Hifadhi za
Kilimanjaro, Arusha na Udzungwa). Maji hayo pia hutumiwa kwa ajili ya kuzalisha
umeme unaotumika kwenye gridi ya Taifa. Hivyo faida za kusimamia Hifadhi hizi
haziishii tu kwa watalii kufurahia bali pia kuna faida nyingine za kiuchumi
ambazo sio rahisi sana kuziainisha katika mfumo wa kifedha (i.e. other values which are not easily
tagged in financial terms).
Mabibi na Mabwana,
Takribani fedha zote za uendeshaji
wa Shirika zinatokana na shughuli za utalii.
Hivyo,ili tufanikiwe tumekuwa tukitangaza vivutio vyetu ndani na nje ya
nchi. Juhudi hizi zimetuwezesha kufanya vizuri katika soko na kupata Tuzo
mbalimbali kimataifa.
Kwa mwaka huu tu wa 2015, mtandao maarufu kimataifa unaojulikana kwa
jina la “Safari Bookings” uliiteua Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuwa “The best park for African safaris” na hii
ni baada ya kushindanishwa na hifadhi nyingine 50 Barani Afrika zikiwemo za
Afrika Kusini.
Aidha, Hifadhi za Mikumi na Arusha zilitunukiwa “Certificate of Excellence”
na mtandao maarufu duniani ujulikanao kama TripAdvisor. Vilevile, tumekuwa
tukipata tuzo mbalimbali kwa ushiriki wetu kwenye maonyesho ya kimataifa na
Mwezi Juni mwaka huu Banda la TANAPA kwenye maonyesho ya Korea World Travel
Fair lilipata “The Best Tourism Marketing Award”. Nitumie fursa hii kutoa
shukrani kwa wadau wote tulioshirikiana kwa njia moja au nyingine katika kupata
tuzo hizi.
Ndugu Wahariri,
Hifadhi ya Serengeti imepata jumla ya alama 4.89
kati ya 5-98%. Kwa mara ya kwanza
Hifadhi ya Ruaha imeingia kwenye kumi bora kama best park for African
safaris. Katika vivutio 140
vilivyoshindanishwa zipo hifadhi za Taifa nne ambazo zimeingia kwenye vivutio
hamsini bora. Hifadhi hizo ni Serengeti,
Ruaha, Katavi (22) na Tarangire (42).
Mwelekeo huu mpya wa kuendelea kutambulika kwa
Hifadhi kati ya ukanda wa kusini na kaskazini mwa Tanzania. Hali hii ni muhimu kwa uwiano wa maendeleo
(balanced dev.) Tunashukuru wadau wote,
hasa vyombo vya habari kwa jitihada kubwa zilizofanyika kuvitangaza vivutio
vyetu.
Pamoja na mafanikio haya, hatuna budi kuongeza
weledi na kasi ya kuvitangaza vivutio vyetu ili viingie kwa wingi zaidi kwenye
orodha ya vivutio bora vya Afrika.
Tunategemea pia kwamba jitihada hizo zitajikita
kwenye kupambana na ujangili ambao umebadilika sura kila mara, kwani unatishia
uwepo wa rasilimali zetu ambazo ni urithi wa kizazi hiki na vzazi vijavvyo.
Ndugu wanahabri,
Tusiposhikamana na kushinda vita dhidi ya ujangili,
tutakuwa tumewakosea haki Watanzania.
Ushirikishwaji wa vyombo vya habari umekuwa
unatekelezwa na TANAPA kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukutana na
Wahariri na Wanahabari mbalimbali kila mwaka, kufanya ziara mbalimbali zinazojumuisha
vyombo vya habari katika maeneo yetu ya Hifadhi za Taifa; pamoja na kuwa na
vipindi katika vyombo mbalimbali vya habari tukilenga kuifahamisha jamii
shughuli zetu pamoja na wajibu wa sekta nyingine katika kuunga mkono shughuli
za uhifadhi na utalii.
Mkutano huu wa Mwanza unakuwa ni wa tatu kuwahusisha
Wahariri na Wahariri wa Habari ambao kimsingi ndio wasimamizi muhimu katika utoaji
wa habari kila siku katika vyombo wanavyotoka. Mwaka jana Mkutano kama huu
ulifanyika hapa hapa Mwanza. Mikutano hii imekuwa na mafanikio makubwa sana kwa
Shirika na hasa tunaona kuwa kiwango na mwamko wa wanahabari kuandika masuala
ya uhifadhi na utalii hususan katika Hifadhi za Taifa unakua kwa kiwango
kikubwa.
Ndugu Wanahabari,
Eneo la Utalii wa Ndani nalo limekuwa ni changamoto
kubwa sana kwa shirika ambapo licha ya sekta utalii hii kuwa na fursa kubwa kutoa
mchango mkubwa kwenye uchumi wa nchi, bado kwa kiwango kikubwa tumekuwa
tukitegemea wageni kutoka nje ya nchi. Ni dhahiri kuwa wakati umefika sasa kwa
Watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea maeneo haya kwa ajili ya kutalii.
TANAPA kwa upande wake itatoa ushirikiano katika kufanikisha dhamira kwa
mustakabali mzuri wa uchumi wa nchi yetu.
Kauli mbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni “Wajibu
wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”. Pamoja na kuelezea shughuli za
TANAPA, mada zitakazowasilishwa zitahusu masuala ya Utalii na Uhifadhi na namna
wanahabari wanavyoweza kushirikiana nasi katika kuhimiza uhifadhi na kuendeleza
utalii. Mada kuu nne zitawasilishwa na
viongozi wa TANAPA na wanazuoni maarufu akiwemo Nd. Jenerali Ulimwengu na Dkt.
Alfred Kikoti. Inatarajiwa kuwa washiriki watapata fursa ya kuchangia na
mwishoni watatushauri namna ya kuboresha utekelezaji wa majukumu yetu.
Ndugu Wahariri,
Baada ya kusema hayo, naomba sasa nitamke kuwa
warsha hii imefunguliwa rasmi na niwaombe mchangie na kutoa ushauri na maoni
mazuri yatakayotusaidia sote kwa pamoja kuendeleza sekta ya uhifadhi na utalii
nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni