Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika Equality for Growth (EfG), JaneMagigita
akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) wakati wa ufunguzi
wa Kongamano hilo Dar es salaam leo.
Ofisa
Programu Dawati la Uangalizi wa Serikali wa Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC), Hussein Sengu (kulia) akitoa mada katika Kongamano la
siku mbili la Wanawake Wafanyabiashara Sokoni Tanzania lililofanyika Dar
es Salaam leo. Kongamano hilo lililowahusisha wanawake kutoka mikoa tisa ya Tanzania Bara limeandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)
Mwezeshaji wa Kongamano hilo, Japhet Makongo akizungumza na Wanawake wafanyabiashara waliohudhuria Kongamano hilo.
Maofisa wa EfG, wakiwa kwenye Kongamano hilo. Kutoka kushoto ni Sarah Mambea na Brenda Kharono.
Maofisa wa EfG, wakiwa kwenye Kongamano hilo, kutoka kulia Mussa Mlawa,Susan Sitta na Munaa Abdalah.
Wafanyabiashara wanawake Masokoni wakiwa kwenye Kongano hilo.
Na Dotto Mwaibale
MKURUGENZI
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti Tanzania (Repoa), Samwel Wangwe
amewataka watanzania kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo hususani
wanawake kwani wananafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa.
Akizunguza
Dar es Salaam leo wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la kwanza la wanawake
wafanyabiashara sokoni Tanzania, Wangwe alisema ni muhimu kuhakikisha
wafanyabiashara hao wanawezeshwa na kuwajali katika uzalishaji na
uendeshaji wa biashara zao.
Alisema
kwa mujibu wa takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa hali ya kiuchumi
duniani katika sekta ya wafanyabiashara wadogo inaendelea kukua hivyo
kutoa changamoto kubwa katika kuhakikisha inawekewa mazingira mazuri ya
kisera.
"Wafanyabishara
wadogo ni wengi sana hivyo wananafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa
kutokana na uwepo wa asilimia 43 ya wajasiriamali wanawake Tanzania,"
alisema Wangwe.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth
(EfG), Jane Magigita, alisema lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha
wanawake wafanyabiashara walio sokoni kutoka katika mikoa mbalimbali ya
Tanzania Bara kwa lengo la kuwajengea mshikamano na kujadili masuala muhimu yanayowahusu katika biashara zao.
Alisema
kongamano hilo limehusisha wanawake 200 kutoka katika mikoa ya Mwanza,
Shinyanga, Mtwara, Lindi, Mara, Mbeya, Iringa, Dar es Salaam, na mkoani
Tanga katika Wilaya ya Lushoto huku wakiongozwa na kauli mbiu isemayo
'Sauti ya Mwanamke Sokoni'.
Alisema
kauli hiyo inalenga kumkomboa mwanamke mfanyabiashara kwa kumjengea
uwezo kutambua yeye ni nani na nafasi yake kama raia katika kuendesha
shughuli biashara za shughuli za soko.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni