NSSF YABORESHA HUDUMA KWA WATEJA

SHIRIKA la  Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeboresha huduma kwa
wateja kwa kubadilisha muonekano wa ofisi zake Jijini Dar es Salaam
ili kupunguza urasimu wa kutoa huduma sanjari na utaratibu wa wateja
kubonyeza kitufe maalum kwaajili ya maoni ya huduma zinazotolewa.

Aidha sekta isiyo rasmi na rasmi zimeaswa kujiunga na mifuko ya
hifadhi ya jamii itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi kwani
waliojiandikisha kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii ni wachache hali
inayopelekea wazee kujiingiza katika ulinzi .

Hayo yalisemwa jana Jijini hapa na Meneja Kiongozi Uhusiano na Huduma
kwa Wateja Eunice Chiume wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari .

Alisema  lengo la kuboresha ofisi hizo ni kuhakikisha wateja wanapata
kile wanachokihitaji  sambamba na kuondoa msongamano  wa kupata huduma
mbalimbali zinazotolewa na mfuko huo lakini pia wamekuja na huduma
nyingine muhimu kwaajili ya kupima utendaji kazi kwa wafanyakazi
wanaowahudumia wateja.

Alisema sababu nyingine ya kuboresha ofisi za Dar es salaam ni
kutokana na kuwa na wachama wengi ambapo asilimia 7 ya wanachama wa
Mfuko huo wapo huko.

“Lakini tukishamaliza huko tutaenda mikoa mingine kuboresha ofisi na
mazingira ya ofisi yawe mazuri, ili wateja wapate huduma bora na za
uhakika”.

Akizungumzia suala zima la  sekta isiyo rasmi na rasmi ni vyema
kujiunga katika mifuko hiyo ya jamii ili waweze kujiwekea akiba na
baadaye kunufaika na mafao mbalimbali kwani vijana hivi sasa
wanafariki na kuwaacha wazee hali inayopelekea wazee kukosa misaada
kwa tegemezi wao na kusababisha kuingia katika sekta mbalimbali ili
waweze kupata fedha za kijikimu na maisha.

“wazee hivi sasa ndio wanabaki na vijana ambao ni tegemezi wanakufa
hivyo ni vyema sasa kuhakikisha watu wanajiunga na mifuko ya hifadhi
za jamii na kuboreshwa maisha yao “.

Kuhusu Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii(SSRA) kukutoa
mafao na kuainisha kuwa mifuko yote itoe mafao yanayolingana alisema
SSRA imetoa kikokotozi sahihi  wa mafao hayo lakini changamoto iliyopo
sasa ni kila mfuko kubuni aina ya mafao kwaajili ya kuongeza idadi ya
wanachama na NSSF inatoa mafao bora zaidi hivyo ni vyema wanachama na
wananchi mbalimbali wakajiunga kwenye mfuko huo.

Aliongeza kuwa hivi sasa NSSF inajivunia utoaji  mikopo kwaajili ya
wajasiriamali hivyo ni vyema sasa Vicoba na Vyama vya Kuweka na Kukopa
(Saccos) kujiunga na mfuko huo ili waweze kukopeshwa kwani masharti ni
vyama hivyo kukaguliwa na wakaguzi wa mahesabu sambamba na kujiunga na
mfuko huo ili waweze kukopeshwa kama kikundi na kurejesha mikopo kwa
jinsi wanavyochangia NSSF.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni