TANZANIA YAKABILIWA NA UKAME

01
Mtunza ghala la kuhifadhi vifaa vya maafa mkoani Shinyanga, Asha Issa akiwaonesha Wakaguzi wa Hesabu za Serikali, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini, Jacob Ndaki (katikati) na John Obeid, rangi zitumiwazo na wanafunzi kuchora zilizo hifadhiwa ghalani hapo, wakati Ofisi ya Waziri Mkuu ilipokagua ghala hilo, tarehe 3 Juni, 2015.
02
Baadhi  ya marobota ya mablangeti yaliyohifadhiwa katika ghala la kuhifadhi vifaa vya maafa mkoani Shinyanga, wakati Ofisi ya Waziri Mkuu ilipokagua ghala hilo,
03
Baadhi ya makasha yaliyohifadhi vifaa vya maafa katika ghala la kuhifadhi vifaa hivyo mkoani Shinyanga, wakati Ofisi ya Waziri Mkuu ilipokagua ghala hilo,

TANZANIA YAKABILIWA NA UKAME

????????????????????????????????????Mgeni Rasmi katika Semina ya Kukuza Uelewa wa Usimamizi wa Mazingira kwa Watendaji wa Halmashari ya Jiji la Tanga, Bwana Salim Chima ambaye pia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga akifungua Semina hiyo ya siku moja iliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
????????????????????????????????????Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Julius Ningu akizungumza jambo katika Semina ya Kukuza Uelewa katika Masuala ya Mazingira kwa Watendaji wa Halmashari ya Jiji la Tanga iliyofanyika jijini humo leo.
????????????????????????????????????wakurugenzi wasaidizi wa Mazingira toka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Esther Makwaia na Bi Magdalena Mtenga wakiwa pamoja na Mgeni Rasmi Bwana Salim Chima wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa.
????????????????????????????????????Washiki wa semina
????????????????????????????????????Mgeni Rasmi katika Semina hiyo Bwana Salim Chima akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wote walioshiriki katika Seminas hiyo
…………………………………………………………..
Na Victor Mariki – Ofisi ya Makamu wa Rais
Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira imebainisha kuwa takribani ya asilimia 61 hadi 75 ya eneo la ardhi ya Tanzania imeathirika na janga la ukame ambao unaweza kupelekea uzorotaji katika ukuaji wa uchumi na hata kutoweka kwa baadhi ya viumbe hai.
Hayo yalielezwa na Afisa Mazingira wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi Zainab Shaban Bungwa wakati akitoa mada katika semina ya kukuza uelewa wa masuala ya usimamizi wa mazingira kwa watendaji wa Halmashauri ya jiji la Tanga mkoani humo leo.
Aidha Bi Bungwa alifafanua kuwa uchumi wa Tanzania unategemea kwa kiasi kikubwa rasimali asili kama vile ardhi, misitu, wanyamapori na maji ambapo inakadiriwa asilimia 75 ya wanachi waishio vijijini hutegemea zaidi ardhi katika uendeshaji wa maisha yao.
Pia aliongeza kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira imechukua hatua mbali mbali katika kukabiliana na janaga hilo kwa kuunda sera, mikakati na sheria mbalimbali za kudhibiti uharibifu wa mazingira nchini.
Baadhi ya mikakati, sera na sheria hizo ni Mkakati wa Hatua za Haraka Kuhifadhi Mazingira na Vyanzo vya Maji, Mkakati wa Bahari na Mabwawa, Program za Kupambana kwa Kuenea Hali ya Jangwa na Ukame, Mkakati wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi pamoja na Program na Miradi inayotekelezwa na Sekretarieti ya Mikoa katika suala la Utunzaji Mazingira.
Sanjari na hayo Bi Bungwa alienda mbele zaidi kusema kuwa hivi sasa robo ya dunia ipo hatarini kukumbwa na hali ya jangwa kwa kuwa zaidi ya hekta bilioni 3.6 za ardhi yake tayari zimeshaathiriwa na janga hilo ambalo mpaka sasa limeathiri zaidi ya watu milioni 900 duniani kote .
Kwa upande wa bara la Afrika hivi sasa hali hiyo ya jangwa imekuwa ni tatizo sugu kwakuwa mpaka sasa tayari asilimia 73 ya ardhi yake imeshathirika vibaya na janga hilo hali ya jangwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni