Kituo
Cha Radio Cha Coconut FM Kilichopo Zanzibar Kwa Kushirikiana na Idara
ya Wanawake na Watoto, Kimeandaa Bonanza linaloitwa "PEPEA - Uhuru Wa
Nafsi, Akili na Mwili" litakalozinduliwa Jumanne tarehe 16 June, 2015
SIKU YA MTOTO WA AFRIKA katika Viwanja vya Maisara mjini Unguja kuanzia
saa 8 Mchana.
Bonanza hili lenye lengo la
kuhamasisha Wananchi juu ya Kulinda na Kutetea Haki za Watoto Zanzibar,
linatarajiwa kuhudhuriwa na Wadau Mbalimbali wa Haki za Mtoto, Watoto wa
Mabaraza ya Watoto, Wazazi, Walezi, Walimu, Wanafunzi, Wanasheria,
Wanahabari na Viongozi wa Dini, Kuunganisha nguvu pamoja katika Kupinga
na Kupiga Vita Vitendo vya Udhalilishaji dhidi ya watoto, Ukiukwaji wa
Haki za Watoto pamoja na "Kutokomeza Ndoa za Utotoni na Mimba za Umri
Mdogo".
Burudani za Kupambia Tamasha ni IGIZO
kutoka kwa Watoto wa Mabaraza, Jakaya, Ras Ndaroh, Wakata Minazi Comedy
pamoja na Ngoma ya Kilua.
PEPEA Bonanza
litakuwa likifanyika Mara mbili kwa Mwaka, Tarehe 16 June (Siku Ya Mtoto
Wa Afrika) kila mwaka na Tarehe 20 Novemba (Siku Ya Watoto Duniani)
Kila mwaka.
PEPEA Bonanza 2015, limefadhiliwa
na MRADI WA KILIMO BIASHARA (MIVARF), mradi wenye lengo la
kuwaunganisha wakulima na masoko na taasisi za fedha, kwa Kushirikiana
na Coconut Media Group, Kituo Cha Huduma Za Sheria Zanzibar (ZLSC), Cool
Coco Accessories, Diligent Consulting Ltd, Save The Children, ZIFF
pamoja na Nyumbani Kwanza Media.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni