…………………………………………
Halmashauri za 
majiji,manispaa,na miji zimeagizwa kubuni vyanzo vya mapato ili 
kujiongezea uwezo wa kuhudumia miradi ya maendeleo Katika dhana nzima ya
 kutotegemea misaada ya wahisani.
Kauli hiyo imetolewa wakati wa 
ufunguzi wa kongamano la upatikanaji wa fedha za ndani za maendeleo 
lililoandaliwa na mfuko wa umoja wa mataifa wa ukuzaji 
mitaji(UNCDF)uliofanyika jijini hapa kwa siku mbili.
Akizungumzia umuhimu wa 
kongamano hilo mratibu wa mashirika ya umoja wa mataifa hapa nchini 
Alvaro Rodrigeuz alisema kuwa anaipongeza serikali ya Tanzania kwa 
kufuata mfumo wa ufuatiliaji wa fedha za ndani kwa ajili ya kukuza 
uwekezaji katika miundombinu ya kibiashara inayoleta mabadiliko kwa 
umma.
Rodriguez alisema kuwa katika 
hotuba yake kwamba kwa kuwezesha mfumo wa UNCDF LFI kwenye serikali za 
mitaa ndio jibu la uhakika la uwekezaji wenye mafanikio endelevu kwa 
taifa zima huku akitanabaisha kuwa mpango huo wa LFI ambao umekuwepo 
nchini kwa miaka mitatu sasa umewezesha kuleta mabadiliko katika 
jamii,na unafaa kumilikiwa na jamii ili kuwezasha mafanikio ya juu 
katika uwekezaji.
“umoja wa mataifa kupitia UNCDF 
utaendelea kufanyakazi na serikali ya Tanzania kwa kuamini kwamba vita 
dhidi ya umaskini itafanikiwa kwa kuhamisha mitaji na kuipeleka katika 
ngazi za chini kwa maendeleo ya wananchi”alisema Rodrigeuz.
Aidha Kongamano hilo ambalo ni 
mwendelezo wa uwezeshaji wa kubadilishana uzoefu na elimu kwa lengo la 
kuwezesha miradi ya umma na binafsi inayochangia maendeleo kujengwa 
katika siku ya kwanza ya kongamano hili washiriki wataonyeshwa miradi 
iliyotekelezwa na manispaa ya Busia Uganda na ule wa mji wa Kibaha hapa 
nchini.
Akisisitiza umuhimu wa kogamano 
hilo meneja nwa LFI duniani Peter Malika alisema kwamba kongamano hilo 
linatoa nafasi kwa watumishi wa serikali za mitaa na wengine kujifunza 
namna mpya ya kupata mitaji kwa kutumia vyanzo vya nyumbani ili 
kufadhili miradi ya miundombinu ya kiuchumi inayohitajika kwa kutoa 
fursa za ujasiriamali,biashara,uwekezaji,ajirakuboresha maisha ya watuna
 ukusanyaji kodi na utoaji wa huduma.
Alisema kuwa washiriki 
watajadiliana na kujipanga kwa ajili ya utekelezaji wa mfumo huo katika 
nchi zao wanakotoka il kupiga hatu mbele katika undelezaji wa miradi ya 
maendeleo inayofadhiliwa na serikali za mitaa bila ya kutegemea fedha za
 nje.
Aidha Mwakilishi wa Katibu mkuu 
wa Tamisemi Denis Bandisa alielezea dhamira ya serikali ya kutumia mfumo
 huo ulioasisiwa na UNCDF kwa kuufanya uwe wa kitaasisi Zaidi ilkuweza 
kusaidia kuutekeleza mipango ya maendeleo na uwekezaji ya serikali za 
mitaa.
Bandisa alisifu kazi ya mpango 
ya uwezeshaji wa fedha za ndani kwa maendeleo(local finance initiative 
LFI) chini ya sekretarieti ya UNCDF kwa ubunifu wake unaowezesha 
kupatikana kwa mitaji ya kuwekeza katika miradi ya maendeleo 
inayofadhiliwa na serikali za mitaa hapa nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni