MKUU WA WILAYA YA KINONDONI, PAUL MAKONDA, AONGOZA MAMIA MAZISHI YA BABA YAKE MSANII STEVE NYERERE

 Marehemu Francis Festus Mengele, enzi za uhai wake.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Francis Festus Mengele.
 Shangazi wa Msanii, Steve Nyerere, Grace Mengele (katikati), akiwa na wadogo zake Steve Nyerere wakati akiwasili makaburi ya Kinondoni kwa mazishi ya mpendwa wao, Francis Mengele.
 Watoto wa marehemu na dada zake wakiwa kwenye ibada ya maziko makaburi ya Kinondoni.
 Ibada ya maziko ikiendelea.
 Hali ilivyokuwa wakati wa mazishi.
 Jeneza lenye mwili wa marehemu Francis Mengele 
likishushwa kaburini.
  Jeneza lenye mwili wa marehemu Francis Mengele 
likishushwa kaburini.
 Wasanii mbalimbali wakiwa kwenye mazishi hayo.
 Ni huzuni tupu.
 DC Makonda akiwa udongo kwenye kaburi la Francis Mengele wakati wa mazishi.
 Kaburi likijengwe baada ya kuwekwa mwili wa marehemu kaburini.
 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Francis Mengele.
 Waombolezaji wakiwasili makaburi ya Kinondoni tayari 
kwa mazishi.
 Hali ilivyokuwa makaburini.
 Hali ilivyokuwa makaburini.

Wasanii  mbalimbali wakiwa kwenye maziko hayo.

Na Dotto Mwaibale

WASANII mbalimbali wa filamu na bongo fleva  wamejitokeza kwa wingi katika mazishi ya baba ya msanii mwenzao Steve Mengele 'Steve Nyerere, aliyofanyika juzi makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Msanii Jacob Stephen JB ni miongoni mwa wasanii waliohudhuria mazishi ya marehemu Francis Mengele baba yake na msanii huyo aliyefariki wiki iliyopita kutokana na maradhi ya mapafu.
Wasanii wengine waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Micky, Vicent Kigosi 'Ray' Elizabeth Michael 'Lulu' Chuchu Hans, Kajala Masanja 'Kajala' , Mtunzi na muongozaji wa filamu Myovela Mswaisa na wengine wengi.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda aliyeongoza mazishi hayo alisema kifo cha Mengele ni pigo kubwa katika wilaya hiyo ya Kinondoni na familia kwa ujumla.
"Mengele alikuwa na mchango mkubwa katika wilaya yetu ya Kinondoni katika kulipa kodi kutokana na biashara zake alizokuwa akizifanya na wingi huu wa watu waliojitokeza katika mazishi yake inaonesha jinsi alivyokuwa akishirikiana na wenzake hasa waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Kimara alikokuwa akisali" alisema Makonda.
Makonda alitumia fursa hiyo kuiomba Manispaa ya Kinondoni ndani ya miezi mitatu kuhakikisha inajenga choo katika makaburi hayo ya Kinondoni kwani ni aibu kwa eneo hilo kukosa choo hivyo kuwafanya wananchi wanaofika kwa ajili ya maziko kukosa huduma ya choo. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni