Kaimu 
Mkurugenzi wa Shirika la  Madini la Taifa (STAMICO), Mhandisi  Edwin 
Ngonyani (kushoto mwenye suti ya kijivu) akipata maelezo kutoka kwa 
mtaalam wa  Wizara ya Nishati na Madini,  Habas Ngulilapi mara baada ya 
kuwasili kwenye banda hilo katika Maonesho ya  Wiki ya Utumishi wa Umma 
 yanayoendelea katika  viwanja  vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.
Kaimu 
Mkurugenzi wa Shirika la  Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi  Edwin 
Ngonyani (kushoto) akisaini kitabu  cha wageni kwenye banda la Wizara ya
 Nishati na Madini.
Mtaalam
 kutoka Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC), Jumanne  Shimba ( wa kwanza 
kulia) akimwonesha Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la  Madini la Taifa 
(STAMICO) Mhandisi  Edwin Ngonyani (katikati)  moja ya  bidhaa 
zinazotengenezwa na  kituo hicho, kwenye  banda la Wizara ya Nishati na 
Madini.
Kaimu 
Mkurugenzi wa Shirika la  Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi  Edwin 
Ngonyani (katikati)  akifurahia moja  ya vinyago  vinavyotengenezwa na 
Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC), kwenye  banda la Wizara ya Nishati 
na Madini.
Afisa 
Uhusiano kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA), Yisambi Shiwa
 (kulia) akieleza shughuli zinazofanywa na  wakala huo kwa Kaimu 
Mkurugenzi wa Shirika la  Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi  Edwin 
Ngonyani (Kushoto) mara alipotembelea banda la wakala huo. Katikati ni 
Omari Rwakyaya kutoka wakala  huo.
Kaimu 
Mkurugenzi wa Shirika la  Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi  Edwin 
Ngonyani (kulia) akisalimiana na  Afisa Uhusiano wa shirika la STAMICO, 
Bibiana Ndumbaro mara alipotembelea banda hilo. Wengine kushoto ni  
Mhandisi Migodi Mwandamizi, Ibrahim Dauda  na kulia ni Mhandisi 
Uchenjuaji Madini, Pili Athumani.
Mhandisi
 Migodi Mwandamizi, Ibrahim Dauda (kushoto) kutoka Shirika la Madini la 
Taifa (STAMICO) akitoa maelezo juu ya kazi za shirika hilo kwa Kaimu 
Mkurugenzi wa STAMICO, Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia) kwenye banda la 
shirika hilo.
Kaimu 
Afisa Masoko Mkuu kutoka makao makuu ya Shirika la Umeme Nchini 
(TANESCO) (Katikati), Monica Massawe akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi
 wa Shirika la  Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi  Edwin Ngonyani 
(Kushoto) mara alipotembelea banda la TANESCO. Kulia ni Afisa Uhusiano 
Wateja –TANESCO  Mkoa wa Illala, Lucas Kusare.
Mtaalam
 kutoka Idara ya Nishati – Wizara  ya Nishati na Madini, Jacob Mayala 
(Kulia) akimweleza Abdul Naseka (Kushoto) majukumu  ya Idara ya Nishati 
kwenye maonesho ya  Wiki ya Utumishi wa Umma  yanayoendelea katika  
viwanja  vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.
Kaimu 
Mkurugenzi wa Shirika la  Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi  Edwin 
Ngonyani (katikati aliyevaa suti) akiwa katika picha ya pamoja na  
baadhi ya washiriki wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kutoka 
Wizara ya Nishati na Madini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni