NYAMLANI MGENI RASMI MASHINDANO YA ROBO FAINALI YAKWANZA YA MTEMVU CUP

Aliyekuwa Makamu wakwanza wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Athumani Nyamlan (mwenye tai) akikagua timu ya mpira ya  Mtoni na Azimio wakati wa mashindano ya robo fainali  ya kwanza ya Mtemvu Cup katika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam  Mtoni ilishinda mabao 4-3. 
 Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu  akisalimia mmoja wa kiongozi wa timu hizo baada ya aliyekuwa  Makamu wakwanza wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Athumani Nyamlan kukagua timu hizo Dar es Salaam viwanja vya Mwembeyanga.
 Aliyekuwa Makamu wakwanza wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Athumani Nyamlan (watatu kulia) akizungumza na wachezaji baada ya kukagua timu hizo
  Athumani Nyamlan akizungumza na waandishi (hawapo pichani) baada ya kukagua timu hizo
 Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu akizungumza na waandishi wa Habari  baada ya ukaguzi wa timu
 Mlinda mlango wa timu ya  Azimio Jafary Iddy akimdhibiti  mchezaji wa timu ya mtoni Nyaka Abuu wakati alipofika langoni kwake wakati wa mashindano ya robo fainali  ya kwanza ya Mtemvu Cup katika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam  Mtoni ilishinda mabao 4-3. 
 
Mashabiki wakifatilia mpambano huo.
Washabiki wakitoa burudani wakati timu hizo zilipokuwa zikichuana.
 Wadau Mbalimbali wakifatilia mpambano huo
 Wasanii Mbalimbali nao walijitokeza akiwemo Mkurugenzi wa Wakubwa na Wanae Saidi fera (kulia) na katikati teacher Bonge ambaye ni Promota na anaye fatia ni Ispectar Harooni Babu  wakati wa mashindano ya robo fainali  ya kwanza ya Mtemvu Cup katika
viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam  Mtoni ilishinda mabao 4-3. 
 (PICHA ZOTE  NA KHAMISI MUSSA)

KAMPUNI YA MATANGAZO YA RIGHT HERE YA HAPA NCHINI YAPATA MWEKEZAJI MPYA NA KUINGIA UBIA NA KAMPUNI KUBWA YA KIMATAIFA

Mwekezaji mkuu wa  kampuni ya RIGHT HERE TANZANIA, Gerard Govaeas akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari katika Ukumbi wa mikutano kwenye Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam leo, Kushoto ni Copywriter wa kampuni ya RIGHT HERE TANZANIA, Asnath Heriel na kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa RIGHT HERE TANZANIA Jenny Woodier.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhurika katika mkutano wa kampuni ya RIGHT HERE TANZANIA mkutano uliofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam leo.
………………………………………
Kampuni ya matangazo ya FLAMETREE iliyojikita Afrika mashariki sasa imezinduliwa upya na kupewa jina jipya la RIGHT HERE TANZANIA, mabadiliko haya yametokana na kuingia kwa mwekezaji mpya wa kimataifa ambaye ameonyesha nia ya dhati ya kuwekeza kwenye kampuni hii kufuatia utendaji mzuri aliouona kwenye kampuni hiyo na kuamua kuongeza nguvu zaidi katika kuinua utendaji, uwekezaji huu unatarajiwa kuongeza tija na muamko wa wafanyakazi na wateja wao.
Kufuatia mabadiliko haya sasa kampuni ya RIGHT HERE itaweza kuhudumia wateja wake kwa viwango vya juu zaidi huku idadi ya wabunifu na vitendea kazi vikiongezwa.
RIGHT HERE imechaguliwa kuwa mwakilishi kwa Tanzania wa kampuni kubwa ya matangazo ya PUBLICIST ambayo ni moja kati ya makampuni makubwa manne duniani kama WPP, Interpublic na Omnicom.
Akizindua jina hilo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwekezaji huyo Bwana Gerald Govaerts amesema, “nia na madhumini ya uzinduzi huu ni kuitambulisha kampuni hii kwa upya kwa watanzania, licha ya kuwapo hapa nchini kwa zaidi ya miaka mitatu.
Gerald aliendelea kusema “soko la Tanzania kwa sasa linakua kwa kasi na sekta ya ushirikiano inazidi kukua kwa viwango vya juu, hivyo umuhimu wa kutangaza masoko na bidhaa zinazozalishwa ni mkubwa mno, kwa kufanya hivi tunatoa nafasi kwa makampuni mengine kutambua uwepo wetu hapa Tanzania na Afrika mashariki na wao kuweza kuzitambua kazi tunazozifanya. 
”Kufuatia uwekezaji huu mpya na ubia kwa kampuni ya kimataifa, nia kubwa ni kukuza sekta ya masoko kwa Afrika mashariki huku tukifanya kazi kwenye viwango vya kimataifa. Tunayofuraha kubwa kwa uwekezaji huu kwani utaongeza tija kwa watanzania wenye vipaji.
Kampuni ya RIGHT HERE inatoa huduma mbalimbali kama kuandaa matangazo ya biashara kwa niaba ya wateja, kununua nafasi za matangazo kwenye vyomba vya habari,kuandaa mikakati ya jinsi ya kukuza bidhaa yako, kuwatangazia wateja bidhaa zao kwenye mitandao mbalimbali na kuwashauri hali halisi ya masoko na ushindani ilivyo duniani kwa sasa.
“Ni furaha kubwa kuitambulisha kwenu kampuni ya RIGHT HERE” alisema Bi Jenny Woodier, meneja mkuu wa RIGHT HERE Tanzania, huku tukijivunia timu yenye wafanyakazi bora na kazi nzuri ambazo tumeshazifanya mpaka sasa kwa wateja wetu,licha ya kuandaa kazi nzuri zilizoendana na soko la wateja wetu lakini pia tumeonekana kimataifa na kupata nafasi ya kuwa wawakilishi wa kampuni kubwa yenye nia ya kuwekeza hapa Tanzania kwa hapo baadaye. Ubia huu na kampuni ya Publicis Africa Group utakuwa na manufaa makubwa kwa wateja wetu na kutuwezesha sisi kama RIGHT HERE kupanua wigo wetu wa kufanya kazi kimataifa.
Dhamira yetu ni kuona ushindani wa matangazo ya bidhaa kwa Tanzania unakua na kufikia viwango vya kimataifa. Mpaka sasa tumeweza kushinda tuzo mbali mbali za kimataifa.
Bi Jenny aliendeela kusema “Kama kampuni tumefanya kazi hapa Tanzania kwa miaka mitatu na makampuni ya ndani na nje ya Tanzania ikiwamo makampuni ya simu, benki, taasisi zisizo za kiserikali,kampuni za samani za ndani, kampuni za sola na nyingine nyingi. Kwa miaka hiyo michache ya kufanya kazi kwa bidii na kutambulika kimataifa,kampuni ya RIGHT HERE sasa inasababu ya kujivunia ujuzi wa kufanya kazi za wazawa huku tukizifanya kwa viwango vya kimataifa. Kama wadau wa matangazo tunaamini ubunifu bora unaleta ushindani katika soko na kuweza kuifikisha bidhaa kwenye viwango vya kimataifa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni