Shirikisho
 la Mpira wa Miguu nchini TFF leo limezindua jezi mpya za timu za Taifa,
 zitakazokuwa zikitumika na timu za Taifa katika michuano mbali mbali 
itakayokua inazikabili.
Uzinduzi
 huo wa jezi mpya uliofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro jengo la 
Golden Jubilee uliambatana na uziduzi wa tovuti mpya ya shirikisho, 
uliongozwa na mgeni rasmi Mh. Said Mtanda, mbunge wa jimbo la Mchinga na
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya jamii.
Katika
 uzinduzi huo, kulizunduliwa jezi aina tatu, ambazo ni jezi za ugenini, 
jezi za nyumbani na jezi zitakazokuwa zikitumika kwa ajili ya mazoezi.
Ifuatayo
 ni hotuba ya Rais wa TFF , Jamal Malinzi aliyoisoma wakati wa uzinduzi 
wa jezi mpya za timu za Taifa, uzinduzi wa tovuti mpya ya TFF na 
kutunuku vyeti kwa viongozi mbalimbali, makocha, wachezaji na wadhamini.
Mh Said Mtanda Mbunge wa Jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii
Mzee Said el Maamry Mwenyekiti Msataafu wa FAT
Ndugu Leodeger Tenga Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya CAF na Rais mstaafu wa TFF
Ndugu wageni waalikwa
Ndugu waandishi wa habari
Mabibi na mabwana
Salam aleikum.
Nianze
 kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutufikisha hapa leo
 na kwa mafanikio mbali mbali ambayo tumekuwa tukiyapata.Ninakushukuru 
sana ndugu mgeni rasmi kwa kuacha shughuli zako kuja kujiunga nasi 
asubuhi hii katika shughuli hii.
Ndugu
 mgeni rasmi,tarehe 08 oktoba 1964 Tanzania ilipata uanachama rasmi wa 
shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA. TFF tuliona jambo zito kama 
hili hatuwezi kuliacha lipite hivi hivi.Hivyo mwaka jana tuliamua 
kuenzi  maadhimisho ya miaka 50 ya kujiunga na FIFA kwa kufanya mambo 
mambo matatu makubwa.
La
 kwanza ni kutoa vyeti maalum kwa watu binafsi na taasisi mbali mbali 
kwa kutambua mchango wao uliotukuka katika kuendeleza mpira wa miguu 
Tanzania.
Leo
 hii ndugu mgeni rasmi tutakuomba ukabidhi vyeti hivi kwa wawakilishi wa
 makundi kadhaa kwa niaba ya wenzao.Makundi haya ni pamoja na viongozi 
wa kitaifa wastaafu,mawaziri wa michezo wastaafu,viongozi waliopita wa 
TFF?
FAT,wakurugenzi
 wa idara ya michezo,wenyeviti na makatibu wa baraza la michezo la 
taifa,Timuya Taifa iliyocheza fainali za Afrika mwaka 
1980,waamuzi,makocha,wachezaji wa timu ya Taifa na watangazaji mahiri wa
 michezo.Jumla tumetunuku vyeti 194. 
Kiuhalisia
 idadi hii ni ndogo sana ukilinganisha na wingi na uzito wa michango ya 
wadau mbali mbali wa mpira katika miaka 50 iliyopita. 
Tunaomba
 Watanzania wenzetu watuelewe katika hili kuwa hawa tutakaowatunuku 
vyeti hivi ni wawakalilisha wa wadau wote wa mpira Tanzania. 
Ninaomba
 tusimame kwa muda mfupi tuwaombe ewadau wenzetu na viongozi wa mpira wa
 miguu ambao wako katika orodha hii na wametangulia mbele ya haki. 
Ndugu
 mgeni rasmi katika kuenzi miaka 50 ya Tanzania kujiunga na FIFA leo hii
 pia tutatoa mchango wa fedha kwa makundi yenye mahitaji katika jamii. 
Pesa
 hizi zinatokana na makusanyo mbali mbali ikiwemo makusanyo ya mechi ya 
ngao ya hisani ifanyikayo kila mwaka. Makundi haya ni pamoja na walemavu
 wa viuongo,walemavu wa ngozi na wasioona. 
Kitendo
 hii ni moja ya juhudi za TFF kurudisha katika jamii kile 
tunachokusanya. Kila kundi litapewa shilingi milioni tano na tunaendelea
 kupokea maombi toka makundi mbali ya kijamii na tukiyapitisha 
tutaendelea kugawa fedha hizi.
Jambo la tatu tutakalolifanya leo litakuwa ni kuzindua rasmi tovuti mpya ya TFF (www.tff.or.tz).
 Tumeamua kufanya jamabo hili katika kuenzi miaka hamsini ya kujiunga na
 FIFA ili kutoa msisitizo kuwa sasa TFF na sisi tunajiunga Na kuendeleza
 mpira kisasa kulingana na teknolojia iliyopo. 
Kupitia
 tovuti hii wadau wa mpira watapata fursa ya kuhabarishwana kuelimishwa 
nkuhusu masuala mbali mbali yahusuyo mpira wa miguu. 
Tovuti
 hii itakuwa pia na sehemu ya kumbu kumbu (archive) zihusuzo historia ya
 mpira wa miguu na matukio mbali mbali katika historia ya mpira wetu. 
Tunaomba
 wadau wenye kumbu kumbu mbali za mpira kama picha,takwimu,vipande vya 
magazeti ya zamani na kadhalika mtuletee ili viingizwe katika tovuti 
yetu.
Tunaamini tovuti hii itakuwa ndio chanzo kikuu cha taarifa na rekodi mbali mbali za sasa na za zamani  zihusuzo mpira wa miguu.
Ndugu
 mgeni rasmi shughuli ya leo tutaihitimisha kwa kuzindua jezi mpya ya 
timu ya Taifa. Jezi hizi zitakuwa ni mbili moja ya ugenini na nyingine 
ya nyumbani.Tunawapongeza watanzania wote walioshiriki katika kubuni 
jezi na mwisho tuliunganisha ubunifu tofauti na kupata jezi 
itakayozinduliwa leo.
Ubunifu
 huu tayari umetafutiwa hati miliki Brela hivyo TFF tutalinda hakii hii 
kwa kuwakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wale wote 
watakaodiriki kuchapisha na kuuza kwa magendo jezi hizi.Utaratibu 
unafanyika kumpata msambaji mmoja halali atakayesambaza jezi hizi nchini  kwa ajili ya wapenzi wa mpira wa miguu.Ukinunua jezi hii utakuwa umechangia maendeleo ya mpira wa miguu.
 TFF
 inawashukuru na kuwapongeza sana Tanzania Breweries ltd ambao ndio 
wazalishaji wa bia ya Kilimanjaro Lager kwa sapoti wanayoitia kwa timu 
ya Taifa na kutuwezesha kubuni na kuzalisha jezi hizi.Tunawashukuru 
sana.
Ndugu
 mgeni rasmi ninaomba nimalizie kwa kuzungumzia kwa kifupi program yetu 
ya mpira wa vijana.kwa kutambua umuhimu wa kuendeleza soka la vijana TFF
 tumejipanga vilivyo kwa mpambano wa hatua za awali za kucheza fainali 
za vijana za Afrika umri chini ya miaka 17 mwaka 2017. 
Mechi
 za ufaulu zitafanyika kati kati ya mwaka 2016.TFF tayari tumeunda 
kikosi cha awali cha vijana chini ya umri wa miaka 15 kujiandaa na 
michuano hii.Kikosi hiki kimetokana na michuano ya copa coca cola ya 
mwaka jana. 
Tunapenda
 tuchukue fursa hii kumshukuru Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete kwa 
kufanikisha nchi yetu ya Tanzania,kwa mara ya kwanza katika historia ya 
nchi hii,kupata uenyeji wa fainali za Afrika. Shirikisho la mpira wa 
miguu Afrika CAF limeipatia Tanzania uenyeji wa fainali za Afrika za 
vijana umri chini ya miaka 17 mwaka 2019.
Tunaomba
 Serikali itushike mkono katika hili ili tuweze kuandaa mashindano 
mazuri.Lakini haitakuwa vyema Tanzania kuandaa mashindano mazuri lakini 
tukatolewa hatua ya makundi.Siku ya jumapili tarehe 07/juni TFF 
tutazindua mashindano ya taifa ya vijana umri chini ya miaka 13 mjini 
mwanza.
 Wachezaji
 bora wa mashindano haya ndio wataunda kikosi cha awali cha Taifa kwa 
ajili ya kushiriki fainali za Afrika watoto umri chini ya miaka 17 mwaka
 2109. 
Tunaomba Serikali pamoja na wadau wote tushirikiane katika kukilea kikosi hiki ili mwaka 2019 tuwe na timu nzuri.
Tunamshukuru
 Mh Dr Fennela Mukangara na wizara nzima ya habari vijana utamaduni na 
michezo kwa ushirikiano wanaotupatia katika hatua hizi na katika 
shughuli nyingine za kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu.
Ndugu mgeni rasmi ninaomba sasa nikukaribishe uhutubie hafla  hii na pia utuongoze katika shughuli zitakazofuata.
Ahsate sana
Jamal Malinzi
Dar es salaam
03/juni/2015

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni