NDUGU WANAHABARI, KWA MUDA WA SIKU MBILI MKOA WA ARUSHA
UMEFANYA OPERATION AMBAYO ILIKUWA INAJUMUISHA TAASISI MBALIMBALI ZIKIWEMO
POLISI, USALAMA WA TAIFA, TRA , KIKOSI DHIDI YA UJANGILI, IDARA YA MADINI NA
UHAMIAJI.
OPERATION HIYO ILILENGA KUKAMATA WAHAMIAJI HARAMU, MAGARI YA
WIZI, MADAWA YA KULEVYA, SILAHA HARAMU, USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU, WIZI
WA MIUNDO MBINU YA TANESCO, UWINDAJI HARAMU WA NYARA ZA SERIKALI, UTOROSHAJI WA
MADINI NJE YA NCHI NA MAKOSA MBALIMBALI.
OPERATION HII YA JANA NA LEO IMEONYESHA MAFANIKIO MAKUBWA
BAADA YA KUKAKAMATA GUNIA 122 ZA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI, MISOKOTO 700
YA MADAWA HAYO PAMOJA NA KUTEKETEZA HEKARI 15 ZA MADAWA HAYO.
MBALI NA MATUKIO HAYO PIA JUMLA YA KILOGRAMU 28 ZA MADAWA YA
KULEVYA AINA YA MIRUNGI ZILIKAMATWA , POMBE HARAMU YA MOSHI LITA 453
ILIPATIKANA PAMOJA NA MAGARI MAWILI
YANAYODHANIWA KUWA NI YA WIZI YALIPATIKANA AMBAYO NI AINA YA TOYOTA
HILUX DOUBLE CABIN NA TOYOTA MARK II.
KATIKA OPERATION HIYO JUMLA YA WATUHUMIWA 14 KUTOKA WILAYA
MBALIMBALI ZA MKOA HUU WAMEKAMATWA NA WANAENDELEA KUHOJIWA KWA MAKOSA
MBALIMBALI WAKIWEMO WATUHUMIWA WANNE WA KOSA LA KUFANYA BIASHARA BILA LESENI
PAMOJA NA MHAMIAJI MMOJA.
AIDHA MTUHUMIWA MMOJA AITWAYE NOEL S/O MESEYEKI MIAKA 20 MKAZI
WA MTAA WA SEURI ALIJERUHIWA KWA RISASI KATIKA PAJA LAKE BAADA YA KUPAMBANA NA
ASKARI POLISI KWA KUTAKA KUMKATA KWA PANGA WAKATI WAKIENDELEA KUFANYA OPERATION
YA MADAWA YA KULEVYA.
MPAKA HIVI SASA NINAVYOZUNGUMZA NANYI OPERATION HIYO BADO
INAENDELEA HIVYO NITAZIDI KUWAPA TAARIFA ZAIDI. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA
POLISI MKOA WA ARUSHA,
NAIBU KAMISHNA WA
POLISI
(DCP) LIBERATUS SABAS
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni