HOTUBA YA NGELEJA KATIKA KUTANGAZA NIA YA URAIS WA TANZANIA YAJIBU MASWALI MENGI YA WANANCHI

 Mbio Za Uraisi 
Mbunge wa Jimbo la Sengerema na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja amekanusha taarifa za kukutwa na tuhuma za ufisadi uliopelekea kuvuliwa uwaziri.
Akizungumza wakati wa kutangaza rasmi nia ya kuwania urais, Ngeleja  
amesema wananchi wengi wamekuwa wakidhani kuwa aliondolewa katika wadhifa huo kwa kutumia madaraka vibaya jambo ambalo si sahihi. 

Ameongeza utaratibu uliofanyika kumuondoa ni utaratibu wa kawaida na kuwa unaweza kutumika hata bila ya kuwa na udhaifu katika uongozi.

Ameongeza kumekuwa na baadhi ya baadhi ya watu wanaoeneza habari hizo kwa leo la kumchafua.
Willim Ngeleja anaungana na viongozi wengine wa siasa kutangaza nia ya kugombea urais. BOFYA VIDEO JUU KUMSIKILIZA. Hebu tujiulize. Kwa nini Takwimu za uchumi nchini zinaonyesha Uchumi ukikuwa kwa wastani wa asilimia 7% takribani kwa muongo mzima wa takribani miaka 10 mfululizo lakini umasikini umekuwa ukipungua kwa asilimia 2% tu? BOFYA VIDEO JUU KUSIKILIZA

Ingawa nafasi ya Urais imeombwa na wanachama wengi, Ngeleja atoa fursa kwa watanzania kumtathimini, na si kwa maneno ya mtaani bali kwa takwimu za utendaji kazi ikiwa ni sambamba na kuifuatilia ripoti ya CAG na ESCROW kuisoma kurasa hadi kurasa.




































Hakuna maoni:

Chapisha Maoni