Mahmoud
Ahmad Arusha
Serikali na wadau wa maendeleo wametakiwa kuzingatia
usawa,haki,sheria ilikutimiza wajibu wao wa kutoa huduma kwa jamii yenye
ulemavu wa ngozi sawa na kufuata haki za binadamu ili kufikia malengo ya
milenia.
Kauli hiyo
imetolewa na mkurugenzi mkazi wa umoja wa mataifa hapa nchini Alvaro Rodrigues
wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya kilele cha siku ya walemavu duniani
yaliofanyika kitaifa mkoani hapa.
Rodrigues
alisema kuwa tunaposherehekea siku hiyo ya kupata ufahamu juu ya watu wa jamii
yenye ulemavu wa ngozi(ALBINO)tunawaji kujua kuwa jamii hiyo inahitaji nini na
je mahitaji yao yanapatikana ikiwemo kupewa ulinzi wa maisha yao kama
usawa,haki na sheria.
Alisema kuwa
Angependa kuzungumzia mambo makubwa matatu yatakayo wakumbusha jamii kwa kuwa
ni kweli kuna maendeleo katika kuboresha haki za binadamu hapa nchini katika
makundi yote hivyo umoja huo ulikishirikiana na serikali na wadau wa maendeleo
utambue wajibu wao kwa watu wa jamii hiyo kwani hiyo ni moja kati ya haki za
binadamu.
Aidha
aliwataka kufanyaikazi kwa nia ya dhati na kuzuia na kukomesha ukatili dhidi
yao kwa watu wenye ulemavu wa ngozi bila kusahau kuwa watu wa jamii hiyo
wamekuwa hawana uwezo wa kumudu gharama mbalimbali zikiwemo dawa,hivyo wapewe
kipaumbele kwani ni haki yao ya kimsingi.
“Umoja wa
mataifa unaendelea kufanyakazi kwa pamoja na serikali na jamiii kwa ujumla
kuboresha utawala wa sheria katika kila mwelekeo pamoja na watu wenye ulemavu
wa ngozi hapa lazima tuipongeze serikali kwa kufuatilia kwa ukaribu mauaji ya
jamii hii ila tuwapende tuwatunze kwani binadamu waote ni sawa”alisema Rodrigues
Nao jumuiya
ya ulaya katika taarifa yao kwa vyombo vya habari wamaepinga mauaji ya jamii
hiyo na kuitaka serikali kuchukua hatua stahiki kuwalinda na kuheshimu haki za
binadamu kwa kuwapatia mahitaji stahiki jamii hiyo kwani imekuwa inakumbana na
changamoto kubwa katika maisha yao ya kila siku.
Kwa upande
wake raisi wa taasisi ya social Protection Association Hassan Abdulrahman alisema
kuwa wao wameandaa Bonanza la kupinga mauaji ya albino litakalofanyika jijini
Dar es salaam sanjari na kongamano kwa wanafunzi wa vyuo 10 mkoani humu.
Alisema kuwa
hiyo yote ni katika kuahakikisha masuala ya mauaji ya watu wenye ulemavu hapa
nchi yanakuwa historian a watu wanajali haki za binadamu wenzao kwani ukatili
huo unatisha na unawanyima haki yao ya kuishi.
Alisema
wanatarajia kwa kila chuo kuwafikia wanafnzi zaidi ya mia mbili na baadae kutoa
elimu kwa jamii ya watanzania wote kufahamu madhila wanayopata wenzao katika
maisha yaoa ya kila siku na kuwa bonanza na kongamano vitafanyika mwishoni mwa
mwezi huo na mwezi ujao.
Wakati huo
huo umoaj wa waganga wa jadi hapa nchi umepinga vikali sula la upigaji ramli
kwa waganga wa jadi katika kuhakikisha dhana potofu ya kuwa viungo vya watu
wenye ulemavu wa ngozi vinaleta utajiri.
Akizungumza
na gazeti hili Mratibu wa umoja huo Julius Juju alisema kuwa changamoto kubwa
wanayokumbana nao kwenye majukumu ya kazi yao ni upigaji wa ramli nah ii ndiyo
sababu kubwa inayopelekea mauji hayo nao wanayapinga kwa nguvu zao na kuwa
watashirikiana na serikali kwa ukaribu kuhakikisha wale wote wenye dhna potofu
wanaingia kwenye mikono ya serikali.
Akatanabaisha
kuwa wamekuwa wakipata changamoto kutoka kwa waratibu wa afya wa serikali ambao
wamekuwa wakichelewesha ushirikiano wao na serikali katika kufikia malengo na
kuondoa tatizo.
“Hapa
ikumbukwe kuwa kutetea hai za binadamu wengi sanjari na uedeshaji wa kupiga
ramli ndio changamoto kubwa katika mauaji ya jamii sisi kama uwawa tunapinga
mauaji na tunapenda kutambulika kisheria katika serikali yetu na tutatoa
ushirikiano kuhakikisha wenzetu wachache wanaotuchafua sheria inachukuwa mkondo
wake”alisisitiza Juju
Mwisho…………………………………………………………………………..
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni