Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisani moja ya fomu za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, wakati alipofika Makao Makuu ya CCM mkoani Dodoma leo Juni 4,
2015 kwa ajili ya kuchukua fomu hizo. Kushoto ni Katibu wa NEC Idara ya
Oganaizesheni , Seif Khatib.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akionyesha mkoba wenye Fomu za kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, baada
ya kukabidhiwa mkoba huo na Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni , Seif
Khatib, kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM mkoani Dodoma leo, Juni 4,
2015.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akionyesha mkoba wenye Fomu za kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, wakati
akiwasili kwenye Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma leo kwa ajili
ya kuzungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa Fomu hizo.
Kulia ni Mzee wa Chama cha Mapinduzi, Ramadhan Suleiman Nzori.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Makao Makuu ya CCM
mjini Dodoma, baada ya kuchukua fomu, leo Juni 4, 2015. Kulia ni Mzee wa
Chama cha Mapinduzi, Ramadhan Suleiman Nzori.
Baadhi ya wana CCM waliohudhuria Mkutano wa Makamu wa Rais Dkt. Bilal. alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipunga mkono kuwaaga wanachama wa CCM na wanahabari, wakati akiondoka
kwenye Ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, baada ya kuzungumza
na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu za kuwania urais.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi Fomu za kusaka wadhamini, mmoja kati ya vijana waliojitolea
kusambaza fomu za kutafuta wadhamini, Saada Ilasi, baada ya mkutano na
waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma. Picha
na OMR
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni