Mke
wa Mbunge wa Kitope Mama Asha Suleiman Iddi akiwanasihi wazazi
kuendelea kuwaonyesha njia watoto wao wakati akizungumza kwenye mkutano
wa ccm wa Matawi ya Kumbaurembo na Cairo katika Kijiji cha Kiwengwa
ndani ya Jimbo la Kitope.Kulia ya Mama Asha ni Mbunge wa Jimbo la Kitope
ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar akimjuilia Hali Muwasisi wa ASP na
Muanzilishi wa CCM Bibi Fatma Suleriman Sio Katika Kijiji cha Kiwengwa.
Balozi
Seif ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kitope akimsalimia Mzee Haji
Muhidini katika Mtaa wa Kumburembo Kiwengwa akiwa katika ziara ya
kuwajulia hali Wazee waasisi wa Afro Shirazy Party.
Balozi
Seif akisalimiana na Mzee Muasisi wa Afro Shirazy Party Bwana Rashid
Khalfan wa mtaa wa Cairo ndani ya Kijiji cha Kiwengwa Wilaya ya
Kaskazini “ B “. Picha na –OMPR – ZNZ.
Mbunge
wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba kazi kubwa
inayowakabali wana wa Chama cha Mapinduzi katika kipindi hichi
kinachoelekea kwenye maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka
huu ni kuhakikisha kwamba Chama hicho kinashinda na kuendelea kuongoza
Dola.
Alisema
sababu za ulazima wa kushinda huko kunatokana na kwamba amani na
utulivu wa Taifa la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania umo ndani ya mikono
ya Chama cha Mapinduzi .
Balozi
Seif Ali Iddi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya
Taifa ya CCM alisema hayo wakati akizungumza na wanachama wa chama cha
Mapinduzi wa Matawi ya Kumbaurembo na Cairo yaliyomo ndani ya Kjiji cha
Kiwengwa katika Mikutano tofauti.
Alisema
Vijana wengi katika baadhi ya maeneo Nchini wamekumbwa na wimbi la
Tabia za baadhi ya watu kukashifu wenzao na hata viongozi wa Kitaifa kwa
kuwaita majina yasiyostahiki ambayo hata katika maandiko na maamrisho
ya Dini hayamo.
Balozi
Seif aliwatanabahisha Vijana ambao ndio walio wengi Nchini kuendelea
kuwaamini wazazi wao walioshuhudia uchungu na madhila ya Utawala wa
Kikoloni pamoja na utamu wa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka
1964.
Akigusia
suala la ajira Balozi Seif ambar pi ni Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar alisema Nyanja ya ajira bado inaendelea kuwa ngumu si kwa
Zanzibar na Tanzania pekee bali hata kwa Dunia nzima kwa ujumla.
Alisema
uhimili wa ajira Serikalini bado ni mdogo na ndio maana Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar ikaweka mkazo na mipango ya kuimarisha mafunzo ya
amali ili vijana wanaomaliza masomo yao ya sekondari wapate fursa za
kujiajiri wenyewe.
Mapema
Sheha wa Shehia ya Kiwengwa Bwana Maulid Masoud Ame alisema Shehia
hiyo imekumbwa na tatizo kubwa la ukosefu wa huduma za maji kutokana na
baadhi ya wawekezaji kushindwa kutekeleza vyema mikataba waliyofunga
kati yao na wananchi hao.
Sheha
Maulid alisema kumekuwa na ujanja unaoonekana kufanywa na baadhi ya
wawekezaji hao baada ya kushindwa kuendesha miradi yao jambo ambalo
limetoa mwanya kwa baadhi ya watu kuharibu miundo mbinu iliyopo ya
usambazaji wa huduma hiyo baada ya kusita kwa muda mrefu.
Naye
Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi aliwakumbusha
wazazi kuendelea kuwaelekeza watoto wao katika kufuata maadili mema
yanayokubalika katika jamii na imani za Dini. Mama Asha alisema Watoto
wengi hasa katika maeneo tofauti ya uwekezaji wamekuwa wakibadilika
tabia siku hadi siku kiasi kwamba hata zile mila na silka zao
zinaonekana kuendelea kupotea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni