Ofisa
 Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo, 
 Benjamin Majoya akikata utepe kuzindua rasmi kisima cha maji 
kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa gharama 
ya sh. mil 56, katika Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang'anda, 
Mkuranga, Mkoa wa Pwani. Kushoto ni Diwani wa Kata hiyo, Karu Karavina  na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo (wa pili kulia).
 Ofisa
 Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo, 
 Benjamin Majoya (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa
 Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto kwake) pamoja na 
Diwani wa Kata ya Kiparang'anda, Karu Karavina (kushoto) wakifurahi 
baada kukabidhi mradi wa  kisima cha maji kwa wananchi wa Kijiji cha 
Magoza, wilayani Mkuranga mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa
 msaada wa TBL gharama ya sh. mil. 56.
 Akina mama wakicheza kwa furaha wakati wa hafla ya kukabidhiwa kisima chas maji na TBL
 Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu akitoa utambulisho wakati wa hafla hiyo
 Ofisa
 Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo, 
 Benjamin Majoya akimtwisha ndoo ya maji Mama mkazi wa Kijiji cha 
Magoza, Kata ya Kiparang'anda, wilayani Mkuranga, Pwani, wakati wa hafla
 ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi msaada wa kisima cha maji 
kilichojengwa kwa gharama ya sh. mil. 56 kijijini hapo. Makabidhiano 
hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki.
 Mmoja wa akina mama akifurahia baada ya kuteka maji kwenye kisima hicho
 Mkurugenzi
 wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo akielezea mikakati ya 
kuisaidia jamii katika uboreshaji wa sekta ya maji nchini kutoka  sehemu
 na faida inayopatikana katika mauzo ya vinywaji vyao
Diwani wa Kata ya Kiparang'anda, akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwapatia msaada huo wa kisima.
 Wakifunua pazia kuzindua mradi huo wa kisima
 Mgeni rasmi, Benjamin Majoya akifungua maji ya bomba badaa ya kuzindua kisima hicho
 Steve Kilindo wa TBL, akinywa maji baada ya kuzindua kisima hicho
Akina
 mama wakazi wa Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang'anda,Mkuranga, 
wakiwa wamebeba ndoo za maji waliyoteka katika Kisima cha maji 
kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika Kijiji 
hicho kwa gharama ya sh. mil. 56. Hafla ya TBL kukabidhi kisima hicho 
cha maji ilifanyika mwishoni mwa wiki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni