KINANA ZIARANI.

1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akilakiwa na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Bw. Ali Ame wakati alipowasili katika kata ya Nyakanazi wilayani Biharamulo mkoani Kagera wakati akianza rasmi ziara yake ya kikazi ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali.
Ziara hiyo itafanyika katika mikoa mitatu ya kanda ya ziwa ambayo ni Kagera yenewe, mkoa wa Geita na kisha atamalizia na mkoa wa Mwanza kwa kufanya mkutano mkubwa wa kuhitimisha ziara kutembelea nchi zima ikiwani mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar na majimbo yote ya uchaguzi nchi nzima, ambapo amekutana na wananchi na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi, kuzifuatilia na kuzipatia ufumbuzi ,
Wakizungumza katika mkutano wafugaji wa kanda ya Ziwa wamelalamikia wizara ya Maliasili na Utalii hasa askari wa wanyamapori ambapo wamesema wamekuwa wakikamata mifugo yao na kuwatoza faini kuanzia shilingi laki mbili mpaka milioni kumi, Mbaya zaidi wanapodai haki yao wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya kikatili kupita kiasi jambo ambalo linawakatisha tamaa ya maisha kabisa.
Wafugaji hao wameongeza kwamba vikao mbalimbali vimeshafanyika zaidi ya 17 kupitia ngazi zote za kitaifa kasoro kwa Mh. Rais tu ndiyo hatujafika, lakini vikao hivyo vyote havijazaa matunda. bado hali ni mbaya na manyanyaso yanazidi kuendelea, wamemuomba Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuwasaidia ili waweze kupata ufumbuzi wa suala hilo na wao waweze kuishi na kufanya shughuli zao kwa amani.
Katika ziara zake hizo Kinana amekuwa akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Nape Nnauye.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni