Waziri Mkuu
Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za wanachama 33,780 wa CCM
Mkoa wa Kilimanjaro, waliomdhani ili aweze kupata ridhaa ya Chama chake
katika kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa
kufanyika Oktoba 25, 2015. Anaekabidhi fomu hizo ni Katibu wa CCM Wilaya
ya Moshi Mjini, Loth Ole Nesele.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
Waziri Mkuu
Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza na Umati wa WanaCCM pamoja na
Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro leo Juni 18, 2015, wakati shukrani kwa
udhamini wa kishindo alioupata kutoka wa WanaCCM hao, ili aweze kupata
ridhaa ya Chama chake katika kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi
Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amepata
udhamini wa wanaCCM 33,780.
Umati wa
wanaCCM wa Mkoa wa Kilimanjaro, ukimshangilia kwa furaha, Waziri Mkuu
Mstaafu, Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani) wakati alipopanda jukwaani
kuwashukuru wa kumdhamini kwa kishindo. Mh. Lowassa amepata udhamini wa
wanaCCM 33,780.
Sehemu ya
WanaCCM na wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa wamefurika katika eneo
la uwanja wa Ofisi ya CCM Mkoa huo wakifatilia kwa majini maelezo ya
Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani) wakati alipokuwa akitoa shukrani kwa
udhamini wa kishindo alioupata leo Juni 18, 2015.
Mh. Lowassa akisomewa Dua na Sheikh wa mji wa Moshi mara baada ya kupewa udhamini wa Kishindo katika Safari yake ya Matumaini.
Mchungaji akitoa maombi.
Wadau wakipata taswira ya Mh. Lowassa wakati akiondoka kwenye Uwanja wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro.
Vijana wa CCM wa Mji wa Muheza wakiuongoza Msafara wa Mh. Lowassa kwenye eneo hilo la Muheza kwa lengo la kuzumza nao.
Vijana wa
CCM Mji wa Muheza wakimshangilia Mh. Lowassa wakati walipomzimamisha ili
aongee nao, alipokuwa safarini kuelekea Mkoani Kilimanjaro.
Ujumbe wa Vijana wa Muheza.
Ni furaha tupu.
Mh. Lowassa
akiwasalimia wananchi wa Mji wa Muheza sambamba na kuwatakia Heri ya
Mfungo Mtukufu wa Mwezi wa Ramadhani, wakati akiwa safarini kuelekea
Mkoani Kilimanjaro kusaka wadhamini watakamuwezesha kupata ridhaa ya CCM
kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika
Juni 18, 2015.
Baada ya
kuwasalimia wanaCCM wa Mji wa Muheza, Mh. Lowassa alipata wasaa wa
kwenda kuhani msiba wa Baba Mzazi wa Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe,
Mh. Adadi Rajab, Marehemu Mzee Rajab nyumbani kwao Muheza, Mkoani
Tanga. anaezungumza na Mh. Lowassa ni Mama Mzazi wa Mh. Adadi Rajab, Bi.
Fatuma Omar.
Mbunge wa
Jimbo la Korogwe Vijijini, Mh. Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu"
(katikati) pamoja na wananchi wa Korogwe wakiwa wamefunga barabara
kuuzuia msafara wa Mh. Lowassa ili aweze kuzungumza nao, huku wakimuuga
mkono katika safari ya Matumaini.
Mh. Lowassa alishuka garini na kuungana na wananchi hao.
Mh. Lowassa akiwasalimia wananchi wa Mji wa Korogwe wakati akiwa safarini kuenekea Mkoani Kilimanjaro.
Shangwe tupu kwa wananchi wa Korogwe.
Kwaherini wana Korogwe.
Alipofika Mombo
Mh. Lowassa akikata nyama ya mbuzi katika moja ya Majiko eneo hilo la Mombo.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mh. Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu" akitoa neno.
Mh. Lowassa akitoa neno la shukrani kwa wakazi wa Mombo.
Mh. Lowassa akiwasalimia WanaCCM na Wananchi wa mji wa Hedaru.
Same.
Waziri Mkuu
Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mmoja wa Wananchi wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Leonard Minja wakati alipofika kumpongeza kwa udhamini
anaoendele kuupata.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni