Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Libarata Mulamula akizungumza katika kikao chake cha kwanza na Watumishi
wote wa Wizara tangu alipoteuliwa na Rais hivi karibuni kuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Mkutano huo
ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere,
Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Juni, 2015. Pamoja na mambo mengine
Balozi Mulamula aliwahimiza Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje kufanya
kazi kwa bidii, kuwa na utii, nidhamu pamoja na unyenyekevu ili kufikia
malengo katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni