Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na kufanya mazungumzomna Spika wa Bunge
la nchi ya Finland Mhe Maria Lohela siku alipotembelea bunge la nchi
hiyo.
Jakaya Mrisho Kikwete akigonganisha glasi na Mari Kiviniemi, Waziri wa
Masuala ya Nje wa Finland wakati wa dhifa iliyoandaliwa kwa hashima yake
jijini Helsinki.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mabalozi wa sasa na wa zamani waliopata kuiwakilisha Finland nchini Tanzania.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watanzania waishio Finland. Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyabiashara wa Finland pamoja
na washirika wao wa Tanzania baada ya mkutano wao jijini Helsinki,
Finland Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo alipotembelea kiwanda cha METSO
cha kutengenezea vipuli vya mitambo ya gesi na mafuta katika jiji la
Helsinki, Finland.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Sweden alipokutana nao Alhamisi jijini Stockholm.
Jakaya
Mrisho Kikwete akipata maelezo ya mchoro kutoka kwa Msanii wa Kimataifa
wa Kitanzania aishiye Sweden Bw. Charles Njau alipokutana na
Watanzania waishio Sweden alipokutana nao Alhamisi jijini Stockholm.Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akilakiwa na Mfalme Carl Gustav wa
16 wa Sweden katika kasri la Mfalme jijini Stockholm, Sweden.Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mtaalamu wa kimataifa wa mambo ya
mapishi aishiye Sweden Chef Issa Kipande ambaye mwaka jana alikuwa
katika tiu ya taifa ya Sweden kwenye mashindano ya kombe la dunia la
mapishi walikoibuka na medali ya dhahabu. Chef Issa, ambaye pia
anaedeesha hoteli Mtwara, hivi karibuni amefungua mgahawa mkubwa mkubwa
kuliko yote wa Ki Afrika katika Ulaya yote mjini Trolhattan, nje kidogo
ya jiji la Stockholm, wenye uwezo wa kuchukua watu 400 kwa wakati mmojaRais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa jumuiya ya watanzania waishio nchii Sweden jijini Helsinki.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa SIDA Bw. Torbjorn Petterson
makao makuu ya shirika hilo la maendeleo la Sweden jijini Stockholm.Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wafanyakazi wa SIDA katika makao
makuu ya shirika hilo la maendeleo la Sweden jijini Stockholm. Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Spika wa Bunge la Sweden Mhe Urban
Ahlin alipotembelea Bunge la nchi hiyo jijini Stockholm.
PICHA NA IKULU
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni