Wanajeshi
nchini wametakiwa kutokuwa tayari kutumika kinyume na taratibu za  kijeshi na 
maadili ya kazi yao ili kuweza kuepuka uvunjifu wa amani iliyoko na
kuweza kutunza nidhamu ya jeshi iliyoko nchini.
Aidha  ameeleza kuwa endapo wanajeshi watakubali
kufanya vitendo kinyume na maadili yao wanaweza kusababisha hali ya hatari
nchini na kupoteza imani na jeshi la nchini.
Hayo
yameelezwa na Mkuu wa utumishi na wa jeshi la wananchi wa Tanzania  Meja Generali 
Mritaba Venanti wakati wa kufunga mafunzo ya kijeshi kwa askari wapya wa
jeshi la wananchi wa Tanzania yaliyofanyika katika kambi ya kijeshi ya jkt
oljoro iliyopo  kata ya Terati  katika wilaya ya Halamashauri ya jiji la
Arusha katika Mkoa wa Arusha.
Aliongeza
kuwa na kuwataka askari wake kuacha kujichukulia sheria mkononi na kufanya
vitendo ambavyo viko kinyume na kanuni na taratibu za kijeshi na hata katiba ya
nchi ili kuweza kuwa askari wa mfano wa kuigwa na kuweza kuendana na nidhamu
waliyopewa wakiwa katika mafunzo yao ya uaskari jeshini.
Na endapo
askari yeyote atangundulika akivunja maadili ya nchi sheria zitachukua mkondo dhidi
yake ili  kuweza kurudisha nidhamu
jeshini na kuweza kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi na mipaka ya
Tanzania na kuweza kudumisha amani iliyopo nchini.
‘’nawasihi
nyie maaskari tunzeni nidhamu ya jeshi jiepushe na mambo ya vurugu,uvunjifu wa
amani na endapo kuna atakayebainika anakwenda kinyume atachukuliwa hatua kali
za kijeshi bila kuona huruma ‘’alisema  Mritaba
Pia
aliongeza kuwa wanapaswa kutunza afya zao ili kuepuka kupata maambukizi ya ukimwi  ambayo yanaweza  kupunguza a nguvu kazi ya Taifa ili kuwa na
kizazi  ambacho hakina maambukizi na
kuongeza ufanisi katika kazi zao.
‘’Hivi sasa
kumekuwepo na baadhi ya watu wamekuwa hawako makini na afya zao hali
inayopelekea kupata maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi na kupunguza ufanisi wa
kazi zao na hasa utelekezaji  wa kujenga
taifa na usalama wa raia wao’’ alisema Mritaba
Kwa upande
wake Mkuu wa mafunzo ya awali ya Kijeshi Kihangaiko iliyopo  Kibaha Jijini Dar es salaam, Luten Kanali  Ramadhani Churi  alisema kuwa mafunzo haya ni kundi la 33 ya
askari wapya kwa kikosi cha 883 jk ambayo yataleta tija na ufanisi katika jeshi
la wananchi wa Tanzania  ambayo wamepewa
mafunzo ya vita na mbinu mbalimbali katika kupambana kwenye kazi za kijeshi.
Alisema
katika kipindi hicho wameonyesha nidhamu ya hali ya juu huku kila mmoja
akitambua wajibu wake uliomleta katika kambi  mbali na changamoto za baadhi yao kutoroka
mafunzo.
Hata hivyo mbali
na kufanikisha kwa kumalizika kwa mafunzo hayo bado kumekuwepo na changamoto ya
utawala na mafunzo kutokana na mazingira mapya ya mafunzo hayo .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni