MBUNGE MUFINDI KASKAZINI MAHMOUD MGIMWA ATOA MSAADA WA AMBULACE JIMBONI KWAKE



MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi
MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi huku wananchi wakiwa kwa pembeni

MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akifurahia jambo na viongozi wa wilaya ya mufindi
MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa na viongozi wa wilaya ya mufindi wakiangalia muonekano wa wa gari hilo la kubebea wagonjwa
na hii ndio sehemu ya ndani ya gari la kubebea wagonjwa alilokabizi mbunge wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi.

na fredy mgunda,iringa 


Gari la kubebea wagonjwa [Ambulance] lenye thamani ya mill.80 lakabidhiwa katika kwa mkurugenzi na mkuu wa wilaya wa Mufindi na MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa ametoa msaada wa gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa iliyopo katika jimbo lake hilo.

Mgimwa alikabidhi gari hilo ikiwa ni moja ya ahadi yake aliyoitoa wakati akiomba kura kwa wananchi wa jimbo la mufindi kaskazini katika kampeni ya uchaguzi mkuu 2015,ambapo alisema kutokana na changamoto ya uhaba wa gari ya kubebea wagonjwa katika zahanati na vituo vya afya katika jimbo hilo, endapo atapewa ya kuwa mbunge atahakikisaha gari ya wagonjwa linapatikanaili wagonjwa waweze kufika hospital kwa wakati.

Akizungumza na wananchi wakati wa kukabidhi gari hilo,mbunge Mgimwa alisema muda wa kupiga siasa umeshapita na kazi iliyopo hivi sasa ni kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuwatatulia changamoto zinazowakabili.

Alisema pamoja na kuongeza gari ya wagonjwa atahakikisha anaboresha vituo vya Afya vilivyopo katika jimbo lake ili kupunguza wimbi kubwa la msongamano wa wagonjwa wanaokuja kutibiwa katika Hospitalini ya wilaya.

‘’’Nipo kwenye mchakato wa kuboresha vituo vyote vya Afya ndani ya jimbo langu,na nitahakikisha huduma muhimu zinapatikanaikiwa pamoja na dawa za kutosha na vifaa mbalimbali vinavyohitajika ili wananchi wangu waweze kuhudumiwa bila usumbufu katika vituo hivyo,hii itasaidia kupunguza msongamano katika hospitali ya wilaya’’’’’alisema Mgimwa

Aidha katika mkutano huo mbunge alisisitiza swala la uaminifu kwa watumishi waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi wahakikishe wanajikinga na vitendo vinavyoashiria rushwa ,vinavyoweza kuwaharibia sifa ya utendaji kazi zao na kushindwa kuwajibika ipasavyo katika majukumu yao.

‘’’Sisi wabunge,madiwani na mtumishi yeyote aliyepewa dhamana na wananchi anatakiwa ajiepushe na swala zima la rushwa ili aweze kutenda haki kwa kuwatatulia changamoto wananchi wake waliomchagua. Tunatakiwa tuwatumie wananchi kuwaletea maendeleo ipasavyo na si vinginevyo’’’alisema

Jamhuri William ni mkuu wa wilaya ya Mufindi,akipokea msaada wa gari hilo kutoka kwa mbunge Mgimwa alisema gari hilo litaweza kusaidia kuokoa vifo vya wanamufindi hasa mama na mtoto ambapo hapo awali kuliwa na gari moja tu.

Williamu alisema kutokana na uwingi wa wagonjwa wanaoenda kutibiwa katika hospitali ya wilaya kwa mwezi ni zaidi ya 500 aliosimia kubwa ni akina mama wajawazito na wengi wao wanafikishwa wakiwa katika hali mbaya kutokana na gari la wagonjwa kuwa moja na kushindwa kumudu.

“Tunamshukuru mbunge kwa kuliona hili na na kuokoa maisha ya watu hasa mama na mtoto ingawa bado hitaji lipo kutokana na uwingi wa wagonjwa endapo tutapata gari la tatu itasaidia sana”alisema

Williamu ameongeza kwa sasa gari hilo litahudumiwa na wilaya kuanzia kuwalipa wafanyakazi wa gari hilo,kulifanyia marekebisho ya gari hilo endapo litatokea kuharibika kwa aina yoyote ile.

Wananchi nao walitoa malalamiko yao kwa mbunge Mgimwa,ambapo Markusi Chusi alimuomba mbunge aweze kusiomamia swala la utapikananji wa vibali vya kuvuna miti,kwa kumtaka ahakikishe wazawa wa eneo husika wanapewa kipaumbele ili waweze kunufaika mali alisi hiyo ilipo kwako.

‘’’’Tumelia kwa muda mrefu,sisi tunanyanyasika kwa kuwapendelea wageni na kutuacha sisi wenyeji tuliopo hapa.Nimeomba mara tano hivi sasa na ukizingatia mimi ni mjane lakini naachwa na pesa yangu inaliwa wageni wanapewa hali inayotukatisha tama wananchi tuliouzunguka msitu huu.’’’’alisema

MKUU WA WILAYA YA KASULU AFUNGA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA KAMBI YA MTABILA 825KJ KASULU KIGOMA

 Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi akikagua gwaride maalum la wahitimu wa mafunzo ya JKT yaliyofanyika katika kikosi cha 825 JK Mtibila ambapo vijana 1140 walifuzu na kumaliza mafunzo hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi akipokea heshima kutoka kwa wahitimu.
 Wahitimu wakipita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima.
 Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi akizungumza na wahitimu hao wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi akiangalia madawati yaliyotengenezwa na vijana hao wa JKT.
**************
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Col Martin Eliah Mkisi katika hotuba yake, amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya JKT Oparesheni Magufuli Kundi la nne Kwa Mujibu wa sheria, kuiamini, kuitekeleza na kuiishi kaulimbiu ya HAPA KAZI TU. 

Amesema vijana hao waliobahatika kupata mafunzo ya JKT katika kambi ya 825 KJ Mtabila kuja na mbinu mbadala na mawazo chanya ktk kutatua changamoto mbalimbali za maisha badala ya kulalamika.

 Amewataka kuwa kielelezo cha nidhamu na uzalendo ktk maisha yao ya vyuoni na mahali pa kazi hapo baadaye kama walivyofundishwa na Wakufunzi Mahiri wa JKT. 

Aidha, Col Mkisi amelipongeza JKT kwa kutekeleza wajibu wake adhimu wa kuwalea na kuwafundisha vijana wa Tanzania, stadi za maisha, uzalenda na ujasiliamali.Vijana wapatao 1140 walifuzu mafunzo hayo yaliyochukua miezi mitatu.

WAJASIRIAMALI KUENDELEA KUPATA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWENYE KATA ZOTE ZA JIJI LA ARUSHA BILA MALIPO

Afisa Kilimo wa Halmashauri ya jiji la Arusha  akiaandaa somo kwa wajasiriamali lililohusu kitalu Nyumba(GREEN HOUSE)pembeni yake ni mkurugenzi wa duka la vitabu la Kasse Bookshop Fanuel Kagengere ambao ndio wadhamini wa semina hiyo ya wajasiriamali iliyoandaliwa na Taasisi ya Zebra Promotion yenye maskani yake jijini Arusha picha zote na mahmoud ahmad wa globu ya jamii Arusha


Sehemu ya wajasiriamali waliojitokeza kupata mafunzo ya ujasiriamali katika kuitikia kauli mbiu ya Mh.rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuli ya Tanzania ya viwanda hapa wakifuatilia utengenezaji wa sabuni ya unga na maji chini ya mratibu wa mafunzo hayo Zuberi Mwinyi wa Zebra Promotion


Afisa wa mikopo wa Benki ya Posta Tanzania Rafael Maganga akitoa maelezo jinsi benki hiyo inavyufanyakazi na utoaji wa mikopo kwa wajasiriamali kwa riba nafuu kwenye semina ya wajasiriamali iliyofanyika jijini Arusha 


Mratibu wa semina hiyo kutoka taasisi ya Zebra Promotion Zuberi Mwinyi akiwa na Mkurugenzi wa Duka maarufu la Vitabu Kasse Store Ltd Fanuel Kagengele ambao pia ni wadhamini wa semina hizo zitakazokuwa zikiendelea kutolewa kwenye kata mbali mbali za jiji la Arusha


Pichani ni Meza Kuu wakifuatilia mafunzo yalivyokuwa yanatolewa kwa wajasiriamali hawapo pichani, kabla ya mafunzo hayo hayajafungwa rasmi na Afisa Tarafa wa jiji la Arusha Felician Rutahengerwa mwenye tai ambapo wenye flana ni maofisa wa kampuni ya Zebra Promotion kulia na Omar Lugendo almaarufu chai Jaba na Novatus Temba ambaye pia ni mkufunzi wa masomo katika semina hiyo wmishoni na maafisa kutoka kitengo cha masoko na mikopo wa Benki ya Posta tawi la Arusha na pia Wadhamini wa semina hizo kwa kata zote za jiji la Arusha,picha na mahmoud ahmad wa globu ya jamii arusha.


Mkufunzi wa mafunzo ya sabuni Novatus Temba akitoa somo jinsi ya utengenezaji wa bidhaa bora za sabuni ya maji na Unga kwa wajasiriamali walioshiriki katika semina inayotolewa na kampuni ya Zebra Promotion jijini Arusha.


Pichani ni Meza Kuu wakifuatilia mafunzo yalivyokuwa yanatolewa kwa wajasiriamali hawapo pichani, kabla ya mafunzo hayo hayajafungwa rasmi na Afisa Tarafa wa jiji la Arusha Felician Rutahengerwa mwenye tai ambapo wenye flana ni maofisa wa kampuni ya Zebra Promotion kulia na Omar Lugendo almaarufu chai Jaba na Novatus Temba ambaye pia ni mkufunzi wa masomo katika semina hiyo wmishoni na maafisa kutoka kitengo cha masoko na mikopo wa Benki ya Posta tawi la Arusha na pia Wadhamini wa semina hizo kwa kata zote za jiji la Arusha.


Afisa Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na Mikopo wa Benki ya posta Tawi la Arusha Rafael Maganga akieleza nini benki hiyo inavyofanyakazi katika kuwasaidia wajasiriamali wa Tanzania kupata mikopo na benki hiyo inaptikana wapi hapa nchini ambapo alisema ni benki rahisi katika kuwafikia watanzania wa hali za chini popote hapa nchini na ikiwa na viwango vya chini vya riba katika mikopo yao.


Afisa Masoko na Mikopo wa Benki ya Posta Tanzania tawi la Arusha Bruno Lanya akijibu maswali magumu kuhusu taratibu za upataji wa mikopo na jinsi gani wajasiriamali watafanikiwa kwenye masoko yao ya ndani na nje ya nchi.


Washiriki wakifuatilia mafunzo yaliokuwa yakitolea kwenye semina hiyo




Wakinadada na wamama kata ya Muriet jijini Arusha wakifuatilia semina ya mafunzo ya ujasiriamali ambayo mafunzo hayo yanatolewa bure kwenye kata zote 25 za jiji la Arusha na kampuni ya Zebra Promotion chini ya Mratibu wake Zuberi Mwinyi picha na mahmoud ahmad arusha.


WAJASIRIAMALI WAKIWA DARASANI WAKIPATA MAFUNZO KWA NADHARIA NA BAADAE VITENDO.


Vijana na kinababa wakifutilia kwa ukaribu mafunzo kwa wajasiriamali yalioandaliwa na kampuni ya Zebra Promotion kwenye kata ya Muriet jijini Arusha
Afisa Tawala wa wilaya ya Arusha Polycarp Laurent ambaye alimwakilisha mkuu wa wilaya ya Arusha kwenye semina ya mafunzo ya ujasiriamali iliyoandaliwa na Zebra Promotion katika kata ya Muriet jijini Arusha pichani akiangaliwa bidhaa iliyotengenezwa na wajasiriamali mara baada ya mafunzo picha na mahmoud ahmad wa globu ya jamii arusha.


Pichani ni Mratibu wa semina ya wajasiriamali kwa kata zote za jiji la Arusha kupitia kampuni ya Zebra Promotion Zuberi Mwinyi akiwa na Afisa Tawala wa Halmashauri ya jiji la Arusha Polycarp Laurent wakihakiki vyeti kabla ya kuwakabidhi wajasiriamali hawapo pichani kwenye kata ya Muriet ikiwa ni muendelezo wa semina kama hizo bila malipo kwa wakazi wa jiji la arusha picha zote na mahmoud ahmad  globu ya jamii arusha.





Na Mahmoud Ahmad Arusha
Wajasiriamali kote nchini wametakiwa kujitokeza kupata elimu ya ujasiriamali ilikuendana na kauli ya mh.raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dkta John Magufuli ya Tanzania ya viwanda ambapo wametakiwa kujiongeza na kutafuta masoko ya bidhaa sanjari na kutengeneza bidhaa zenye ubora.

Kauli hiyo imetolewa kwenye Kata ya Muriet na katibu tawala wa wilaya ya Arusha mjini Polycarp Laurent wakati wakitoa vyeti kwa washiriki wa semina ya wajasiriamali zaidi ya 60 iliyoandaliwa na Taasisi ya Zebra Promotion yenye maskani yake jijini Arusha.

Alisema kuwa ili kuendana na kauli hiyo ifike mahali watanzania na wajasiriamali kujiongeza kwa kutafuta na kutengeneza bidhaa zenye ubora utakaoendana na soko la hapa nchini na nje ya nchi ambapo elimu ndio itakayowafanya kutoka eneo moja kwenda jingine.

“Watendaji na wenyeviti wa serikali ya mtaa wenye dhamana ya kuhakikisha ahadi ya mh raisi inafanikiwa kwa kutoa ushirikiano kwa kampuni zenye nia ya dhati ya kutoa elimu ya ujasiriamali kwa watanzania na yeyote atakayekaidi ahadi ya rais ataenda na maji” alisema Laurent.

Akawataka watendaji kushirikiana na taasisi mbali mbali zinazotoa elimu mbali mbali kwa jamii na waache kufanyakazi kwa mazoea na kudai malipo ya kushiriki katika kupatiwa elimu wa wananchi hilo ni kosa kisheria na linaweza kuwapeleka katika vyombo vya sheria nawasihi muache mara moja tabia kama hizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Zebra Promotion Zuberi Mwinyi alisema kuwa jamii ya watanzania itajitegemea iwapo kutakuwa na sera nzuri kama hili ya hapa kazi tu nao watashirikiana na serikali katika kuhakikisha sera hiyo inafanikiwa kwa vitendo na kuomba ushirikiano wa serikali.

Mwinyi alisema kuwa mafunzo wanayotoa yana misingi ya kuwaunganisha wajasiriamali katika vikundi ambavyo vinaweza kukopesheka kwa taasisi za kifedha na kuweza kujiinua katika kutengeneza viwanda vidogo vidogo na baadae vya kati ambapo mafunzo hayo yanalenga kuinua sera na kauli ya mh.Magufuli  kwa kila kaya kutoa mjasiriamali mmoja.

“Mafunzo yetu yanaenda sambamba na kauli mbiu yetu ya Tanzania ya viwanda inaewezekana, ambapo mafunzo yetu yatatolewa katika  mkoa wote wa Arusha zikiwemo wilaya za ArushaMjini,Monduli,Longido,Karatu,Arusha Dc,Meru na Ngorongoro na baadae Tanzania kwa ujumla”alisema Mwinyi



WATANZANIA WALIVYOTUMIA FURSA YA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA KUFANYA BIASHARA NA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII.


Wafanyabiashara wa tikiti maji wakitumia tukio la kupatwa kwa jua katika mji wa Rujewa wilayani Mbarali kuuza matunda hayo kwa wananchi waliofika katika eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa Jua.
Wafanyabiashara wa Mchele wao pia hawakubaki nyuma wakatumia fursa hiyo kuuza Mchele kwa wananchi waliofika kushuhdia tukio hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amosi Makala,(katikati) ,Mkuu wa Mkoa wa Songwe ,Chiku Galawa na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) Pascal Shelutete wakitizama tukio la kupatwa kwa jua ka kutumia miwani maalumu za kutizamia.
Hatua ya mwanzo ya tukio la kupatwa kwa jua ,baada ya mwezi kuanza kupita mbele ya Jua na kuanza kuzuia mwanga usifike katika uso wa Dunia.

Mama lishe pia hawaubaki nyuma kuhakikisha wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo .
Benki ya NMB pia walitoa huduma ya kufungua Akaunti kwa wananchi waliofika katika eneo hilo kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua.
Umati mkubwa wa wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yaiendelea katika eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ,Amosi Makala akizungumza juu ya fursa za kiuchumi zilizojitokeza kutokana na tukio la kupatwa kwa jua katika mji wa Rujewa wilayani Mbarali.
Mkuu wa Mkoa wa Songe Luteni Mstaafu ,Chiku Galawa akizungumza na wananchi waliofika katika eneo hilo kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA ,Pascal Sheluetete akizungumza na wanahabari ambapo shirika hilo limetangaza kufungua lango la Ikoga kwa ajili ya kuingia Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa upande wa Bonde la Ihefu.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Songwe,Luteni Mstaafu ,Chiku Galawa walipokutana kwa ajili ya kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua.
Mwezi ukiwa umebakiza kipande kidogo wakati ukipita mbele ya jua.
Mwezi ukiwa katikati ya jua na kutengeneza kipete.
Mwezi ukiwa umeanza safari ya kuliachia jua.
Baadhi ya wananchi wakitizama tukio hilo .
Wengine walilazimika kutumia miwani maalumu kwa ajili ya kuchomea vyuma kutizama tukio hilo.


Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Mbarali ,
Mbeya.

MAMIA KWA MAELFU WAANDAMANA KATIKA JIJI LA CARACAS NCHINI VENEZUELA


Mamia kwa maelfu ya watu wameandamana katika Jiji la Caracas nchini Venezuela katika maandamano ambayo yanayohusisha pande mbili hasimu.

Wafuasi wa upinzani wamefanya maandamano makubwa kwa miaka miwili, ya kushinikiza rais
Nicolas Maduro aondoke madarakani kutokana na mgogoro wa uchumi.

Wanaomuunga mkono rais Maduro, nao wamefanya maandamano makubwa wakiwatuhumu wapinzania kwa kutaka kufanya mapinduzi.
               Waandamanaji wakikimbia mabomu ya machozi yaliyorushwa na polisi

          Baadhi ya waandamanaji walikamatwa na polisi kama inavyoonekana hapa