Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi akikagua gwaride maalum la wahitimu wa mafunzo ya JKT yaliyofanyika katika kikosi cha 825 JK Mtibila ambapo vijana 1140 walifuzu na kumaliza mafunzo hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi akipokea heshima kutoka kwa wahitimu.
Wahitimu wakipita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi akizungumza na wahitimu hao wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi akiangalia madawati yaliyotengenezwa na vijana hao wa JKT.
**************
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Col Martin Eliah Mkisi katika hotuba yake, amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya JKT Oparesheni Magufuli Kundi la nne Kwa Mujibu wa sheria, kuiamini, kuitekeleza na kuiishi kaulimbiu ya HAPA KAZI TU.
Amesema vijana hao waliobahatika kupata mafunzo ya JKT katika kambi ya 825 KJ Mtabila kuja na mbinu mbadala na mawazo chanya ktk kutatua changamoto mbalimbali za maisha badala ya kulalamika.
Amewataka kuwa kielelezo cha nidhamu na uzalendo ktk maisha yao ya vyuoni na mahali pa kazi hapo baadaye kama walivyofundishwa na Wakufunzi Mahiri wa JKT.
Aidha, Col Mkisi amelipongeza JKT kwa kutekeleza wajibu wake adhimu wa kuwalea na kuwafundisha vijana wa Tanzania, stadi za maisha, uzalenda na ujasiliamali.Vijana wapatao 1140 walifuzu mafunzo hayo yaliyochukua miezi mitatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni