Na Mahmoud Ahmad Arusha
Wajasiriamali kote nchini wametakiwa kujitokeza kupata elimu ya ujasiriamali ilikuendana na kauli ya mh.raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dkta John Magufuli ya Tanzania ya viwanda ambapo wametakiwa kujiongeza na kutafuta masoko ya bidhaa sanjari na kutengeneza bidhaa zenye ubora.
Kauli hiyo imetolewa kwenye Kata ya Muriet na katibu tawala wa wilaya ya Arusha mjini Polycarp Laurent wakati wakitoa vyeti kwa washiriki wa semina ya wajasiriamali zaidi ya 60 iliyoandaliwa na Taasisi ya Zebra Promotion yenye maskani yake jijini Arusha.
Alisema kuwa ili kuendana na kauli hiyo ifike mahali watanzania na wajasiriamali kujiongeza kwa kutafuta na kutengeneza bidhaa zenye ubora utakaoendana na soko la hapa nchini na nje ya nchi ambapo elimu ndio itakayowafanya kutoka eneo moja kwenda jingine.
“Watendaji na wenyeviti wa serikali ya mtaa wenye dhamana ya kuhakikisha ahadi ya mh raisi inafanikiwa kwa kutoa ushirikiano kwa kampuni zenye nia ya dhati ya kutoa elimu ya ujasiriamali kwa watanzania na yeyote atakayekaidi ahadi ya rais ataenda na maji” alisema Laurent.
Akawataka watendaji kushirikiana na taasisi mbali mbali zinazotoa elimu mbali mbali kwa jamii na waache kufanyakazi kwa mazoea na kudai malipo ya kushiriki katika kupatiwa elimu wa wananchi hilo ni kosa kisheria na linaweza kuwapeleka katika vyombo vya sheria nawasihi muache mara moja tabia kama hizo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Zebra Promotion Zuberi Mwinyi alisema kuwa jamii ya watanzania itajitegemea iwapo kutakuwa na sera nzuri kama hili ya hapa kazi tu nao watashirikiana na serikali katika kuhakikisha sera hiyo inafanikiwa kwa vitendo na kuomba ushirikiano wa serikali.
Mwinyi alisema kuwa mafunzo wanayotoa yana misingi ya kuwaunganisha wajasiriamali katika vikundi ambavyo vinaweza kukopesheka kwa taasisi za kifedha na kuweza kujiinua katika kutengeneza viwanda vidogo vidogo na baadae vya kati ambapo mafunzo hayo yanalenga kuinua sera na kauli ya mh.Magufuli kwa kila kaya kutoa mjasiriamali mmoja.
“Mafunzo yetu yanaenda sambamba na kauli mbiu yetu ya Tanzania ya viwanda inaewezekana, ambapo mafunzo yetu yatatolewa katika mkoa wote wa Arusha zikiwemo wilaya za ArushaMjini,Monduli,Longido,Karatu,Arusha Dc,Meru na Ngorongoro na baadae Tanzania kwa ujumla”alisema Mwinyi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni