WAJASIRIAMALI DAR WANUFAIKA NA MAFUNZO KUHUSU FURSA MPYA KATIKA KILIMO BIASHARA

Margareth Nzuki - ESRF
Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Bi. Margareth Nzuki akiwasilisha malengo ya warsha kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida kufungua warsha hiyo.
Wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam wamefanikiwa kupata nafasi ya mafunzo yanayohusu fursa mpya zinazopatikana katika kilimo cha biashara katika warsha iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF).
Elimu ambayo wajasiriamali waliipata katika warsha hiyo ni elimu ya shamba kitalu na ujasiriamali, elimu ya kilimo cha foda na mbogamboga, elimu ya kilimo na kufuga samaki katika matanki, elimu ya ufugaji samaki katika mabwawa, elimu ya ufugaji samaki katika vizimba, kutazama fursa zilizopo katika ufugaji bora wa kuku na kupata elimu kuhusu Azolla ambayo inaweza kutumika kama chakula cha mifugo na pia kama mbolea.
Akizungumza katika warsha hiyo mmoja wa wawasilishaji mada, Dominic Haule alisema kilimo kina fursa nyingi lakini watu wengi wanashindwa kufanikiwa kutokana na kuwepo mambo mbalimbali ambayo yanayakwamisha.
Alisema changamoto hizo ni pamoja na kukosa elimu ya kilimo na kushindwa kupata taarifa sahihi za kiteknolojia kuhusu kilimo cha kisasa.
“Tunahitaji kutazama fursa zilizopo, zipo nyingi lakini bado tunakabiliwa na changamoto wakulima wanakosa elimu ya kilimo kujua hata mazao bora yanakuwaje, bado kuna shida ya pembejeo na mitaji inakuwa changamoto maana ili ufanikiwe unahitaji uwekezaji mkubwa,” alisema Haule.
Awali akitoa neno la ufunguzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida alisema Tanzania ina maeneo mazuri ya kufanyia kilimo na kinachohitajika ni wakulima kutambua njia za kufanya kilimo bora ili watakapoanza kulima waweze kupata matokeo mazuri kwa aina ya kilimo wanachofanya.
“Uchumi wa nchi unategemea kilimo, nchi yetu ina eneo zuri la kilimo lakini bado kuna changamoto kama mabadiliko ya hali ya nchi ni vyema kukutana na kujua njia bora za kutumia kabla ya kuanza kufanya kilimo,” alisema Dkt. Kida.
Tausi Kida - ESRF
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akifungua warsha ya siku moja yenye lengo la kutambulisha na kuelimisha zaidi wananchi kuhusu fursa mpya za kibiashara ambazo zinapatikana katika sekta ya Kilimo.
Kilimo Biashara Workshop by ESRF
Mshereheshaji katika warsha ya kutazama fursa mpya katika kilimo biashara, Abdallah Hassan.
Kilimo Biashara Workshop by ESRF
Mwakilishi wa Wizara ya Kilimo, Mifungo na Uvuvi , John Mapunda akielezea nafasi ya serikali kuwasaidia wajasiriamali ili kufikia malengo yao katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na ESRF.
Kilimo Biashara Workshop by ESRF
Pichani juu na chini ni umati wa washiriki kutoka mikoani na maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam waliohudhuria warsha hiyo iliyoandaliwa na ESRF.
Kilimo Biashara Workshop by ESRF
Kilimo Biashara Workshop by ESRF
Tausi Kida
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akifurahi jambo na mwakilishi wa Wizara ya Kilimo, Mifungo na Uvuvi, John Mapunda katika warsha hiyo.
IMG_7749
Dominic Haule kutoka chuo cha iMADS akielezea kuhusu shamba kitalu na ujasiriamali.
Abdullatif Mbulo
Bw. Abdullatif Mbulo kutoka Horti Ogranics Ltd, akielezea kuhusu kilimocha foda na mbogamboga, sambamba na ufugaji wa samaki katika matanki.
IMG_7857
Luteni Joseph Lyakulwa, kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) akizungumzia Ufugaji wa Samaki katika Vizimba katika warsha hiyo iliyohudhuriwa na wajasiliamali mbalimbali.
IMG_7770
Pichani juu na chini washiriki wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalamu wa Kilimo Biashara.
Kilimo Biashara Workshop by ESRF
IMG_7788
Kilimo Biashara Workshop by ESRF
Pichani juu na chini washiriki wakiuliza maswali kwa wawasilishaji mada katika warsha ya siku moja ya Kilimo Biashara iliyoandaliwa na ESRF.
Kilimo Biashara Workshop by ESRF
Tausi Kida
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akizungumza na waandishi wa habari.

FILIMBI ZAKATIZA KWA MUDA HOTUBA YA RAIS KENYATTA BUNGENI

Filimbi zimepulizwa na baadhi ya wabunge kabla ya rais Uhuru Kenyatta hajasimama kutoa hutuba yake mwaka kwa taifa bungeni.

Spika wa Bunge Justini Mururi alilazimika kuingilia kati ili kuleta utulivu na kusoma vifungu vya kanuni za bunge, hata hivyo rais Kenyatta alipoanza kuhutubia filimbi zikaibuka tena.

Kufuatia filimbi hizo wabunge Opiyo Wandayi, Millie Odhiambo, Simba Arati, John Mbadi, Gladys Wanga na Seneta Moses Kajwang waliamuriwa kutoka nje ya bunge.

TCRA WAIKABIDHI LESENI YA BIASHARA KAMPUNI YA AGANO SAFI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Ally Simba (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi, Iyaloo Ya Nangolo leseni ya biashara itakayoiwezesha kutoa huduma za mfumo wa malipo mbalimbali kwa kutumia mtandao 'malipo ya huduma anuai kwa njia ya kidigitali' (Digital Payment Services). 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Ally Simba (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi, Iyaloo Ya Nangolo leseni ya biashara itakayoiwezesha kutoa huduma za mfumo wa malipo mbalimbali kwa kutumia mtandao 'malipo ya huduma anuai kwa njia ya kidigitali' (Digital Payment Services). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fortunata Mdachi pamoja na Amos Shiyuka (kushoto) wakishuhudia.
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi inayokuja kuwekeza katika huduma za mfumo wa malipo mbalimbali kwa kutumia mtandao 'malipo ya huduma anuai kwa njia ya kidigitali' (Digital Payment Services). Leseni hiyo imekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba kwa kampuni ya Agano Safi huku akiikumbusha kufanya shughuli zake kwa kuzingatia vigezo na masharti ya leseni.

Akipokea leseni hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi Iyaloo Ya Nangolo alisema anaishukuru TCRA kwa kuwaamini na kuwakambidhi leseni ya kufanya biashara ya mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao, hivyo kampuni hiyo itahakikisha inafanya kazi kwa ufanisi na kushirikiana na vyombo husika ikiwemo BoT ili kuhakikisha jamii na taifa linanufaika na shughuli hizo.

Alisema kampuni hiyo inayoundwa na Wanamibia kwa ushirikiano na baadhi ya Watanzania imejipanga kuja na teknolojia ya kisasa katika mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao kwa kushirikiana na kampuni ya malipo ya MobiPay iliyojijengea heshima ya huduma zake katika nchi za Kusini mwa Afrika huku ikiwa na makao yake nchini Namibia.

Hafla hiyo ya makabidhiano imehudhuriwa pia na Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria ambaye amepongeza Agano Safi kufanikiwa kufanya biashara hiyo nchini Tanzania jambo ambalo linaongeza ushirikiano baina ya nchi hizo huku zikibadilishana teknolojia kwa masuala mbalimbali na ubunifu kibiashara
.
Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fortunata Mdachi (kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa MobiPay, Amos Shiyuka mara baada ya Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba kukabidhi leseni ya biashara kwa Kampuni ya Agano Safi itakayoiwezesha kutoa huduma za mfumo wa malipo kwa njia ya kidigitali' (Digital Payment Services). 
Picha ya pamoja baina ya viongozi wa pande zote mara baada ya zoezi la kukabidhiana leseni kukamilika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Agano Safi, Cuthbert Mhilu, Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria, Mkurugenzi Mtendaji wa MobiPay, Amos Shiyuka, Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi Iyaloo Ya Nangolo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba pamoja na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa TCRA, Fortunata Mdachi.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Agano Safi, Cuthbert Mhilu, Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria, Mkurugenzi Mtendaji wa MobiPay, Amos Shiyuka, Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi Iyaloo Ya Nangolo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba pamoja na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa TCRA, Fortunata Mdachi katika picha ya pamoja mara baada ya zoezi la kukabidhiana leseni kukamilika.
Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akizungumza katika hafla ya TCRA kuikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maofisa wa TCRA wakiwa katika hafla hiyo.
Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akizungumza katika hafla ya TCRA kuikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Agano Safi, Cuthbert Mhilu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MobiPay, Amos Shiyuka (kulia).
Baadhi ya maofisa wa kampuni ya Agano Safi (kulia) wakiwa na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla hiyo.
Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akipeana mkono na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa TCRA, Fortunata Mdachi mara baada ya zoezi la kukabidhiana leseni kukamilika.

PROFESA MDOE AIELEZA KAMATI YA BUNGE MIKAKATI KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA YA MADINI



 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe (katikati) akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Tanzanite, Emmanuel Mbise ulioko Kitalu B, Mirerani. Mgodi huo unamilikiwa na Mchimbaji Mdogo, Ester Ndosi.
 Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kaskazini, Elias Kayandabila, akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, walipotembelea Mgodi wa madini ya Tanzanite wa Franone uliopo Kitalu D, Mirerani. Wa kwanza Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe.
Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje (Kulia), akimwonyesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe (Kushoto), namna Kiberenge kinavyofanya kazi ya kushusha watu na vifaa chini ya ardhi kunakochimbwa madini ya Tanzanite, wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini katika Mgodi wa Tanzanite One uliopo Mirerani, hivi karibuni.

Na Veronica Simba - Mirerani 
Kuwepo kwa mitobozano ya mara kwa mara baina ya wachimbaji wadogo wenyewe kwa wenyewe na kati ya Mgodi wa Tanzanite One na wachimbaji wadogo wa Tanzanite katika vitalu B na D, kumeelezwa kuwa ni changamoto inayosababisha kukosekana kwa usalama katika eneo la machimbo ya Tanzanite, Mirerani kutokana na kutumika kwa silaha za moto na mabomu ya kutengenezwa kienyeji. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe aliyasema hayo hivi karibuni mkoani Arusha, wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kukagua Migodi mbalimbali inayochimba madini hayo eneo la Mirerani. 
Akielezea maana ya mitobozano, Profesa Mdoe alisema ni hali ya wachimbaji kuvuka mipaka ya leseni zao na  kuingia katika maeneo ya wachimbaji wengine wakiwa chini ya ardhi. 
Kutokana na tatizo hilo, Profesa Mdoe  alisema kuwa Serikali, kupitia Wizara ya Nishati na Madini, hususan Ofisi ya Madini Mirerani, inaendelea na juhudi za kuwaelimisha wachimbaji na wadau wote wa sekta ya madini katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria  za nchi ikiwemo Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na kanuni zake pamoja na Sheria ya Baruti ya mwaka 1963 na kanuni zake za mwaka 1964.
Akifafanua zaidi, Profesa Mdoe alisema kuwa, mbali na kuwataka wachimbaji kufuata sheria, pia kumekuwepo na juhudi za kuwakutanisha wachimbaji wa Kitalu C na Vitalu B na D  ili kuweka namna ambavyo uchimbaji unaweza kufanyika kwa kuepuka mitobozano. 
Aidha, alieleza kuwa Wizara ya Nishati na Madini imekuwa ikishirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara katika kudhibiti utoroshaji wa Tanzanite. 
Alisema, wataalam wa Wizara kupitia Ofisi ya Madini Mirerani, Mamlaka ya Udhibiti wa Madini Tanzania  (TMAA ) na Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO), wameongeza udhibiti wa Tanzanite kwenye maeneo ya uzalishaji chini mgodini. 
"Kazi hii inafanyika kwa kuhakikisha kuwa maafisa husika wanakuwepo wakati wa uzalishaji ili kufahamu kiasi kinachozalishwa, " alisema Profesa Mdoe. 
Vilevile, alieleza hatua nyingine zinazochukuliwa na Serikali kutatua tatizo hilo kuwa ni pamoja na kuandaa maonesho ya vito ya kimataifa ambayo hufanyika Arusha kila mwaka ambapo wanunuzi wa kimataifa kutoka nchi mbalimbali hukutana moja kwa moja na wauzaji wakubwa wa ndani hivyo kupunguza uwezekano wa wafanyabiashara kuendelea kutorosha Tanzanite. 
Alisema kuwa, Serikali imeanzisha masoko ya ndani yatakayokuwa yanafanyika Mirerani kila mwaka na ina mpango wa kuanza ujenzi wa soko kubwa Mirerani ili madini yote yatakayozalishwa yaweze kuuzwa, kukatwa na kusanifiwa Mirerani. 
Kwa upande wao, Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, waliitaka Serikali pamoja na mambo mengine, kuhakikisha migogoro iliyopo katika machimbo hayo ya Tanzanite Mirerani inatafutiwa ufumbuzi wa haraka na wa kudumu.

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AAPISHWA JANA

Balozi Seif Ali Iddi akipeana mkono wa hongera na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi kabla Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kumuapisha kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika  Ikulu Mjini Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipeana mkono wa hongera Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid baada ya kuapishwa kushika nafasi hiyo  Ikulu Mjini Zanzibar.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid akiwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu (kushoto) wakati wa kuapishwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kushika nafasi hiyo  Ikulu Mjini Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipitia hati ya kiapo kabla ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kumuapisha rasmi kushika nafasi hiyo aliyomteuwa,hafla ya kiapo ilifanyika  Ikulu Mjini Zanzibar(kushoto) Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi.
Washauri wa Rais wa Zanzibar wa mambo mbali mbali ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu Mjini Unguja.
Balozi Seif Ali Iddi akielekea sehemu ya kula kiapo kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar alipoapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika hafla iliyofanyika  Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Balozi Seif Ali Iddi kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika  Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akibadilishana mawazo na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baada ya kumuapisha rasmi  katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Mwanasheria Mkuu wa zanzibar Mhe,Said Hassan Said (kushoto) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu (katikati) na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid wakiwa katika hafla ya kuapishwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kushika nafasi hiyo  Ikulu Mjini Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi(kushoto) akiwa na Viongozi waliohudhuria kuapishwa kwake ,(wa pili kushoto) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mama Asha Suleiman Iddi baada ya kumuapisha Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar  katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar,(Picha na Ikulu.]

DK BENDERA ATOA MAAGIZO YA MADAWATI



 Na Mahmoud Ahmad,Manyara
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera amewaagiza viongozi wa Wilaya za mkoa huo, kuhakikisha hadi mwisho wa mwezi Aprili kusiwepo na wanafunzi wanaokaa chini kwa kukosa madawati ya kukalia.

Akizungumza  mjini Babati, Dk Bendera alisema japokuwa Rais John Magufuli amewaagiza wakuu wote wa mikoa kuondoa tatizo la ukosefu wa madawati  hadi Juni 30 mwaka huu, kwa Manyara mwisho ni Aprili 30.

Alisema Manyara haipaswi kusubiri hadi mwezi  Juni 30 ili imalize upungufu wa madawati hivyo, wakuu wa wilaya, wakurugenzi watendaji, wenyeviti wa halmashauri, viongozi na wananchi kwa ujumla kuhakikisha hilo linafanyika.

“Rais wetu Dk Magufuli baada ya kututeua hivi karibuni alituagiza wakuu wote wa mikoa kuhakikisha tunamaliza tatizo hilo hadi mwezi wa sita lakini mimi nataka kwangu Manyara ikifika mwezi wanne tumalize,” alisema Dk Bendera.

Kwa upande wake, katibu tawala wa mkoa huo Eliakim Maswi alisema kiwango cha elimu Manyara kimeporomoka kwa kuchangiwa zaidi na tabia ya wafugaji kuhama kutoka eneo moja hadi jingine kufuata malisho mazuri ya mifugo yao.

“Hali ni mbaya kwenye halmashauri zetu zenye wafugaji wengi kwani mkoa wetu umeendelea kuporomoka kuanzia ngazi ya elimu ya msingi na sekondari hivyo jitihada za dhati za kupambana na hili zinahitajika,” alisema Maswi.

Hata hivyo, aliwataka viongozi wa wilaya za mkoa huo kuhakikisha shule zote za sekondari ambazo hazijamaliza ujenzi wa vyumba vya maabara, wanamaliza haraka iwezekanavyo ili wanafunzi wapate elimu kwa njia ya vitendo.

UVUVI HARAMU VICTORIA TISHIO KWA UHIFADHI



Swala wapatikanao kwenye hifadhi ya Saanane kama walivykutwa na kamera ya matukio ya manyara leo jijini mwanza hivi karibuni

Na  Mahmoud Ahmad alivyotembelea ,Mwanza .

Uvuvi haramu wa kutumia sumu kali,pamoja na neti umekua ukitishia uhifadhi katika hifadhi ya Taifa ya Saa Nane na Lubondo ambazo zimepewa jukumu la kulinda mazalia ya samaki ili samaki hao wasipotee kwenye uso wa dunia.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake waliofanya ziara ya kutembelea hifadhi hiyo ya Saa Nane   iliyoko jijini Mwanza ,ziara iliyoratibiwa na Tanapa Mhifadhi Mkuu Donatus Bayona amesema kuwa changamoto inayowakabili ni uvuvi haramu na uvamizi wa maeneo ya hifadhi unaofanywa na wavuvi wanaojipatia kipato bila kujali kuwa wanaharibu mazalia ya samaki . 
Askari Wanyamapori katika hifadhi hiyo Aloyce  Mong`ee   amesema kuwa wamekua wakiimarisha doria katika mipaka ya hifadhi ili kuzuia shughuli hizo za uvuvi ambazo ni tishio kwa uhifadhi.
“Kuna mipaka ambayo tumeweka hakuna mtu anayeruhusiwa kufanya uvuvi ndani ya eneo la hifadhi ili kuhifadhi mazalia ya samaki” Alisema Askari huyo
Mhifadhi huyo amesema kuwa Hifadhi hiyo ambayo iko katikati ya jiji la Mwanza inaongoza kwa kuwa na watalii wengi wa ndani ambao ni asilimia 90% ya wageni wanaotembelea hifadhi hiyo.
Alisema Hifadhi ya Saa Nane ni moja kati ya hifadhi zilizopo kati kati ya miji hivyo kuvutia watanzania wengi kutembelea  eneo hilo ambali lina wanyama pori pundamilia,swala na sokwe weusi pamoja na madhari nzuri na maridhawa ambazo hutumika kama sehemu ya kujifunzia na kupumzikia.