AFRICA ENERGY FORUM-LONDON


                                                                                                By Ayoub Mzee-London
The critical role of acces to enrgy and power in economic growth is perhaps one of the few core elements of economic development that all economists can agree upon.There are few resources that can benefit the public as a broadly and as effectively as access to power .

From Schools to hospitals and homes to offices,the existence of plentiful,affordable and reliable power is the cornerstone of growth in Africa

MAKAMU WA RAIS AFUTURU NA WATOTO YATIMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Nasaha maalum mara baada ya kumaliza kufuturu na watoto Yatima kwenye viwanja vya Karimjee iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi television cha Mboni Show.
Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Mhe. Ally Hapi (kushoto) akiwa kwenye dua pamoja na wageni waalikwa wengine.
Watoto Yatima wakiswali wakati wa tafrija ya kufuturisha watoto Yatima iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi cha televisheni cha Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kufanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kushoto) akisalimiana na Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kulia) mwingine pichani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess inayotengenezakipindi cha television cha Mboni Show Bi. Mboni Masimba wakati wa tafrija ya kufuturisha watoto yatima iliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee.
Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess kinachoandaa kipindi cha The Mboni Show akizungumza wakati wa kufuturisha watoto yatima .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza kwenye tafrija ya kufuturisha Watoto Yatima iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa na kipindi cha television Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
                                                     Watoto wakipewa juisi wakati wa Tafrij ya Futari.
      Naibu Mufti Mkuu Sheikh Hamid Jongo akizungumza kwenye tafrija hiyo.

MASHINDANO YA ORYX ENERGIES RALLY OF TANZANIA 2016 KUTIMUA VUMBI JULAI 08 - 10, BAGAMOYO PWANI

Viongozi wakuu na waandaaji wa mashindani ya mbio za Magari wakiwa katika mkutano huo wa waandishi wa habari leo Juni 30 Jijini Dar es Salaam katika hotel ya Southern Sun.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania, Bwana Mohamed Kiganja azungumza katika mkutano huo
Rais wa chama cha Magari Tanzania (AAT), Bwana Nizar Jivani akizungumza katika mkutano huo
Bwana Satinder Birdi ambaye ni mwandaaji wa shindano hilo akizungumza katika tukio hilo
Sehemu ya waandishi wa Habari.

Kamishna Msaidizi wa jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda Fortunatus Musilimu akizungumza katika mkutano huo ambapo alimwakilisha Kamanda Mpinga. Jeshi hilo limebainisha kuwa watazingatia sheria za usalama barabarani
Meneja Masoko na mauzo wa kampuni ya Radio Wave Communications, Bi. Suraiya Ismail ambao pia ni wadhamini wa mashindano hayo ya magari akizungumza katika tukio hilo. Kushoto ni Meneja mauzo wa Mkoa wa kampuni ya Utrack Africa Ltd, Bi.Mary Cassian
Meneja Masoko na mauzo wa kampuni ya Radio Wave Communications, Bi. Suraiya Ismail akizungumza katika tukio hilo.
Waandaaji Wakuu wa shindano hilo kampuni ya Oryx Energies, Mkurugenzi Mkazi Tanzania, Bwana Nick McAleer akizungumza katika tukio hilo. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

Mashindano ya magari yanayojulikana kwa jina la Oryx Ernegies Rally of Tanzania 2016 yanatarajiwa kufanyika Julai 8 mpaka 10 mwaka huu huko Bagamoyo Mkoani Pwani huku jumla ya magari 25 yatashindana.

Wakitambulisha rasmi tukio hilo kwa vyombo vya Habari, Waandaaji Wakuu wa shindano hilo kampuni ya Oryx Energies kupitia kwa Mkurugenzi Mkazi Tanzania, Bwana Nick McAleer amebainisha kuwa kampuni yao yao hiyo imejiandaa vyema kupitia mashindano hayo na yatakuwa ni ya aina yake siku hiyo hivyo wananchi waendelee kutumia bidhaa za Oryx ikiwemo mafuta, virainishi vya magari, gesi na bidhaa zingine kutoka kampuni hiyo ambayo vinapatikana hapa Tanzania.

“Mashindano ya Oryx Energies Rally of Tanzania 2016 ni miongoni mwa michezo bora na mizuri yenye kuvutia. Hivyo jamii itapata nafasi ya kushuhudia michuano hii mwishoni mwa wiki kuanzia Julai 8 hadi 10 mwaka huu katika viunga vya Bagamoyo” alieleza Mkurugenzi Mkazi huyo, Bwana Nick McAleer.

Kwa upande wake Bi. Surayia kutoka kampuni ya U track and Radio Wave ambao wanahusika na masuala ya vifaa vya mawasiliano na ulinzi katika magari ambao pia ni miongoni mwa wadhamini kwenye mashindano hayo wamesema kuwa vifaa bora na vya kisasa vitatumika wakati wa mashindano hayo ikiwemo kubaini gari lililopotea njia ama kuharibika na kutoa msaada wa haraka katika mashindano hayo.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania, Bwana Mohamed Kiganja akizungumza kwa upande wa Serikali amesema kuwa, ametaka kuona vyama vya michezo vinasonga mbele na kuacha kufanya kazi kwa mazoea licha ya kukabiliwa na changamoto za uendeshaji.

Kiganja amebainisha kuwa, chama cha mbio za magari kimekuwa kikijitahidi kufanya shughuli zake mbalimbali hivyo kuwa na maendeleo tofauti na vyama vingine ambavyo vilitakiwa kuiga mfano huo.

“Tuache mazoea hizi sasa ni zama za Hapa Kazi tu. Vyama vya michezo vijikite kufanya shughuli za kijamii ili zionekane kwani ndio majukumu yao na sio kusubiria mashindano tu, Sasa kama hakuna mashindano nini kitafuata?, si ndio mwanzo wa kuanza kugombana maana vyama hivi vikipataa pesa tu ugomvi unaingia” alibainisha Kiganja.

Kiganja pia alipongeza mashindano hayo ya Mgari na kubainisha kuwa, mchezo huo wa Magari ni miongoni mwa michezo bora kabisa hapa nchini hvyo inatakiwa kuungwa mkono na pande zote kama michezo mingine huku akiwataka waandaaji wake kuhakikisha wanaipeleka mbio hizo za magari katika mikoa mingine ya Tanzania ikiwemo Mwanza ambapo wageni mbalimbali wanaweza kushiriki hasa kutoka nchi za jirani.

Kwa upande wake, Rais wa chama cha Magari Tanzania (AAT), Bwana Nizar Jivani amesema kuwa, mashaindano hayo yamezingatia viwango vyote ambapo jumla ya magari 25 yatashiriki ambapo kati ya magari hayo, Magari 4 yatatoka Uganda, 2- Zambia, Kenya (1), Falme za Kiarabu (1). Na kwa magari ya kutoka Tanzannia ni 17.

Magari hayo 17 ya Tanzania ambapo Dar es Salaam magari 10, Arusha (3), Moshi (3), na Tanga (1). Aidha, magari hayo yanatarajiwa kushindana katika umbali wa kilometa 246 kwa siku ya kwanza.

Uzinduzi huo unatarajiwa kuzinduliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye katika hoteli ya Southern Sun Dar es Salaam, siku hiyo ya Julai 8.

UMOJA WA KIJAMII (UKI) CHUO CHA SMMUCo WATEMBELEA KITUO CHA KULEA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM CHA KILIMANJARO ORPHANAGE CENTRE

Baadhi ya watoto wanaoishi na kulelewa katika kituo cha Kilimanjaro Orphanage Centre
Wanaumoja wakiwa katika picha ya pamoja katika lango kuu la kuingia chuoni hapo kwa kampasi ya mjini kabla ya kuelekea kituoni
Wana UKI wakikaribishwa na kupewa maelezo ya awali kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo hicho Bw.Lazaro Edward mara tu walipowasili
Wana UKI wakicheza na watoto wa Kilimanjaro Orphanage Centre
Watoto wakiteta jambo huku nyuso zao zikiwa na tabasamu la kutembelewa na wageni

Kulia ni mwenyeketi wa UKI Bw. Msiyaki Kuruchumila akikabidhi zawadi kwa watoto hao
Mwenyekiti wa vijana CCM mkoa wa Kilimanjaro Juma Raibu (Kushoto) akiwa na Rais wa Serikali ya wanafunzi SMMUCo Edgar Nziku ambao wote  ni wana UKI wakiwa na watoto kituoni hapo.
 
Umoja wa Kijamii (UKI) ulioanzishwa na wanafunzi wa chuo kikuu cha Stefano Moshi Memorial University wenye lengo la kuitumikia jamii kwa kujitolea kupunguza changamoto za ukali wa maisha katika jamii ulipata fursa ya kukitembelea kituo cha kulea watoto yatima na wenye mahitaji maalum cha Kilimanjaro Orphanage Centre kilichopo kata ya Pasua wilaya ya Moshi mjini  mkoa wa Kilimanjaro.
 Akizungumzia historia yao, Mkurugenzi wa kituo hicho Bw. Lazaro Edward alisema kituo hicho kinachopokea watoto kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea kwasasa kinalea watoto wapatao 79 huku watano kati yao wakiwa ni waathirika wa virusi vya Ukimwi kueleza kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni idadi ya vitanda pamoja udogo wa eneo lakini wanatarajia kukihamisha kituo hicho baada ya ujenzi wa kituo rasmi kukamilika.

Wanaumoja wa UKI wanaosoma kozi mbali mbali walikuwa na wasaha mzuri wa kucheza , kuongea pamoja na kuwakabidhi zawadi watoto hao zenye thamani ya shilingi laki tatu.
 Akieleza lengo la kukitembelea kituo hicho mwenyeketi wa umoja huo Bw. Msiyaki Kuruchumila mwanafunzi wa Elimu na Usimamizi wa Bishara alisema kuwa hii ni sehemu ya muendelezo wa  majukumu yao kama Umoja wa Kijamii na hivyo bado safari yao kuelekea kujitoa kwa jamii bado ni ndefu.
 Mwandishi wetu alipotaka kujua kwanini kuhusu umoja huu kuwa umejikita zaidi katika chuo cha SMMUCo na je yapo malengo zaidi ya kuutanua,Bw. Kuruchumila alisema kuwa wapo katika mchakato wa kuuneza katika vyuo vyote katika mkoa wa Kilimajaro na wanajitahidi hili liwe limekamilika kabla ya mwezi wa kumi na moja mwaka huu. 
"Sisi kama SMMUCo peke yetu hatuwezi kwa kuwa jamii inamahitaji mengi na baada ya kuridhika kuhusu uimara wetu ndani ya SMMUCo tumeanza mchakato kuhakikisha UKI inasambaa katika vyuo vyote hapa Moshi ikiwa ni MOCu, KCMC,MWECAU na MWEKA" alihitimisha.

Akizungumzia ziara hiyo mmoja kati ya wanaumoja huo Godilisten Mnuo alisema kuwa amejifunza mambo mengi hasa upendo kutoka kwa watoto hao na kutoa wito kwa wadau mbali mbali kuwa na tamaduni ya kudumisha uhusiano na wenye mahitaji kwa moyo wa dhati katika jamii ili kwani hii ndio sifa bora machoni pa Mungu na wanadamu.

TAASISI YA METDO YAHIMIZA WAZEE WANAOLELEWA KATIKA KITUO CHA BUKUMBI KUSAIDIWA.

Ashraph Omary (wa pili kushoto) akizungumza jambo kwa niaba ya Wanachama/Wafanyakazi kutoka Taasisi ya METDO (Mining and Environmental Transformation For Development Organisation iliyopo Kahama mkoani Shinyanga, walipotembelea Kituo cha Wazee Bukumbi kilichopo Misungwi mkoani Mwanza.

Wafanyakazi wa METDO wakiambatana na Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa daladala Kanda ya Ziwa, Hassan Dede pamoja na Wanafunzi wa Geita International School, waliwakabidhi wazee wanaolelewa katika kituo hicho msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula.

Taasisi ya METDO kupitia kwa msemaji wake, Ashraph Omary, iliwahimiza wanajamii kwa kushirikiana na taasisi za serikali na binafsi kuwasaidia wazee wanaoishi katika kituo hicho ili kuondokana na changamoto zinazowakabiri ikiwemo ukosefu wa mavazi, chakula, matibabu pamoja na ujenzi wa uzio kituoni hapo ikiwa ni miongoni mwa changamoto zilizoanishwa kuwakabiri wazee hao.
Imeandaliwa na BMG

MAMLAKA ZA JIJI LA LAGOS ZAFUNGA MAKANISA NA MISIKITI KWA KELELE

Mamlaka za Jiji la Lagos nchini Nigeria imeyafunga makanisa 70 na misikiti 20 kwa katika mikakati yake ya kupunguza kiwango kikubwa cha kelele jijini humo.

Kampeni hiyo ya kukabiliana na kelele pia imezikumba hoteli 10 pamoja na klabu za starehe, katika Jiji la Lagos lenye watu milioni 20.

Serikali imeahidi kuhakikisha inataka kulifanya Jiji hilo la Lagos kuwa halina kelele ifikapo mwaka 2020, kwa kudhibiti kelele za mziki, honi za magari na kutoka kwenye makanisa na misikiti.

MAREKANI YATOA TAHADHARI KWA RAIA WAKE NCHINI KENYA

                         Wapiganaji wa kundi la al-Shabaab wakifanya mazoezi

Raia wa Marekani waliopo nchini Kenya wametahadharishwa kuepuka kutembelea maeneo ya Lamu Mombasa, Eastleigh Nairobi pamoja na kaunti za maeneo ya kaskazini mashariki mwa Kenya.

Tahadhari hiyo ya Marekani vilevile imewataka raia wa Marekani kutembelea tu mji wa Mkongwe wa Mombasa wakati wa mchana na kuepuka kutumia kivuko cha Likoni, Mombasa kwa usalama wao.

Taarifa ya tahadhari hiyo inakumbushia pia mashirika ndege ya Marekani kuwa waangalifu na uwezekano wa mashambulizi ya makombora ya kurushwa kutokea aridhini.