RC GAMBO:WANANCHI LIPENI KODI ZA MAJENGO ILI KUONDOA USUMBUFU UNAOWEZA KUJITOKEZA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na waandishi wa habarimapema  leo ofisini kwake .Picha na mahmoud ahmad.



 Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha Pili Mbaruku akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mapema leo katika mkutano ulioitishwa na mkuu wa mkoa  kwa waandishi wa habari.


Na.Mahmoud Ahmad .Arusha
 
Wananchi wametakiwa kulipa kodi ya majengo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza baadae kutokana na Sera ya serikali inayisema kila mwananchi inayomraka takiwa kulipa kodi ya majengo.


Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake na kusema kuwa yapo makundi matatu yanayoaanishwa katika ulipwaji wakodi hizo


Hata hivyo amesema makundi hayo ni Pamoja na wale ambao nyumba zao hazijapimwa wala kufanyiwa tathimini,kundi la pili in wale ambao nyumba zao zimepimwa lakini hazijafanyiwa tathimini kundi la mwisho no wale ambao nyumba zao zimepimwa na kufanyiwa tathimini.


Hata hivyo amesema kundi la kwanza linatakiwa kulipa shilingi elfu 15,000kwa mwaka,ambapo kundi la pili wanatakiwa kulipa waendelee kulipa Kwa utaratibu waliokuwa wanautumia toka awali,kundi la tatu gharama zao zipo juu kulingana na tathimini mpya iliyofanyika mwaka 2015-2016.


Vilevile Gambo ametoa onyo kali Kwa wanasiasa wenye tabia ya kupita Kwa wananchi na kuwapotosha kuhusiana na ulipaji wa kodi hiyo amesema hatua Kali za kisheria zitachukuliwa endapo watambaini mmoja wapo.


Nae meneja wa TRA mkoa wa Arusha Pili Mbaruku amesema kuwa wamejiwekea utaratibu mzuri kuhakikisha wanashirikiana na watendaji wa mitaa ili zoezi la ukusanyaji liwe jepesi kwao badala ya kupanga foleni TRA jambo ambalo litawqchukulia muda wananchi.

Amewataka wananchi kujitokeza Kwa umoja ili kurahisisha zoezi hilo na kuweza kutekeleza agizo la serikali kulipa kodi

KAIMU JAJI MKUU AWAAGIZA MAJAJI KUZIPA KIPAUMBELE KESI ZENYE MASLAHI KWA UMMA

Na Lydia Churi- Mahakama, Arusha
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Prof.Ibrahim Juma amewaagiza Majaji wote nchini kuzipa umuhimu wa kipekee wa kuzisikiliza na kuzimaliza kwa haraka kesi zote zenye mvuto kwa jamii na zenye maslahi kwa Umma ili kuongeza imani ya wananchi juu ya Mahakama kama chombo cha utoaji wa haki.
Akifungua mafunzo ya Majaji wa Mahakama ya Rufani pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania alizitaja kesi zinazotakiwa kusikilizwa na kumalizwa kwa haraka kuwa ni zile zinazohusu dawa za kulevya, ujangili, ugaidi, Mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na mauaji ya vikongwe kwa imani za kishirikina.
Prof. Juma alizitaja kesi nyingine zinazotakiwa kupewa umuhimu wa kipekee kutokana na mvuto wake kwa jamii kuwa ni pamoja na kesi za rushwa kubwa, utakatishaji wa fedha, matumizi mabaya ya madaraka kwa viongozi, na kesi zinazohusu changamoto za ukuaji wa demokrasia na uendeshaji wa masuala ya siasa.
Kesi nyingine zilizotajwa na Jaji Mkuu katika kupewa umuhimu wa kipekee ni  zile zinazohusu miradi mikubwa kama Reli, mashamba makubwa ya uwekezaji, gesi, ujenzi wa barabara, kesi za mabenki na kesi zinazohusisha kundi kubwa la watu zinazogusa migogoro ya umiliki wa ardhi na migogoro ya wakulima na wafugaji.
“Tukichukua hatua za dhati kuhakikisha kesi hizi zinaisha kwa wakati tutakuwa tumetoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi na kuongeza imani ya wananchi kwa Mahakama”, alisema Kaimu Jaji Mkuu.
Alisema ni Jambo muhimu kwa Mahakama kuzipa umuhimu wa kipekee kesi hizi hasa katika kipindi hiki  ambacho Serikali inatekeleza mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano (2016/17-2021) ambao kauli mbiu yake ni “kujenga uchumi wa viwanda  ili kuchochea mageuzi ya uchumi na Maendeleo ya watu”.
Aidha, Kaimu Jaji Mkuu pia amewataka Majaji kuangalia namna ya kutoa huduma kwa haraka kwenye makundi yenye mahitaji maalum kama vile wazee, walemavu na wajane hususan wakati huu ambapo Mahakama inaelekeza nguvu zaidi katika kuondosha mlundikano wa mashauri mahakamani.
Aliwakumbusha Majaji hao kupanga kesi kwa siku kwa kuzingatia masaa kama njia ya kuwaepusha wananchi wenye kesi mahakamani na adha ya kusubiria kwa muda mrefu kesi zao kuitwa.
Akizungumzia usikilizwaji wa kesi Mahakamani, Prof. Juma alisema kwa mwaka 2016, Mahakama kuu ya Tanzania pamoja na divisheni zake zote ilifanikiwa kumaliza kesi kwa idadi sawa na zilizosajiliwa. Alisema, jumla ya kesi 276,147 zilisajiliwa na kwamba kesi 278,226 zilimalizika. Kesi 57,326 zilibaki mahakamani.
Alisema bado kuna changamoto ya mlundikano wa kesi kwenye Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ambapo lengo kuu la Mafunzo hayo kwa Majaji ni kujadili namna ya kumaliza mlundikano wa kesi kwenye Mahakama hizi.
Aliongeza kuwa Mahakama za Mwanzo pekee ndizo zenye mafanikio makubwa ya kutokuwa na mlundikano wa kesi. Mpaka kufikia Desemba 2016,  Mahakama za Mwanzo zilimaliza kesi zote zenye umri unaozidi miezi sita mahakamani.

Majaji wa Mahakama ya Rufani na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wanaendelea na Mafunzo ya siku tano mjini Arusha ambapo wanajifunza mambo mbalimbali yanayohusu utendaji wao wa kazi likiwemo suala la kuondosha mlundikano wa kesi kwenye Mahakama zote nchini. 

GAMBO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA KENYA OFISINI KWAKE JIJINI ARUSHA

MAHAKAMA YA KENYA YAZUIA KUAJIRI MADAKTARI NJE YA KENYA


Mahakama ya Kazi nchini Kenya imeweka zuio la muda dhidi ya serikali ya nchi hiyo kuajiri madaktari kutoka nje ya nchi hiyo.


Jaji Nelson Abuodha wa Mahakama hiyo ametoa amri hiyo baada ya Madaktari watano wa Kenya kufungua malalamiko ya kuitaka serikali kusitisha mpango wake wa kuajiri madaktari 500 kutoka Tanzania wakidai kuna madaktari wengi nchini humo ambao hawajaajiriwa.


Madaktari hao wameitaka Mahakama itoe amri inayoitaka serikali kuajiri madaktari 1,400 ambao hawana ajira ambao wamefuzu katika taaluma ya utabibu na iizuie serikali kuacha kabisa kuajiri madaktari na wataalam wengine wa afya kutoka nje.


Hatua hiyo imekuja baada ya Rais Magufuli kukubali ombi lilitolewa na Rais Uhuru wa kuipatia Kenya madaktari katika kusaidia utoaji tiba baada ya kutokea kwa mgomo wa madaktari nchini humo wenye lengo la kushindikiza waboreshwe maslahi yao.

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AMALIZA ZIARA NCHINI TANZANIA

Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ethiopia Mhe. Hailemariam Dessalegn ameondoka nchini leo kurejea nchini mwake Ethiopia baada ya kumaliza ziara yake rasmi ya kiserikali hapa nchini aliyoifanya kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Mhe. Hailemariam Dessalegn ameagwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli aliyeongozana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.


Akiwa nchini Mhe. Hailemariam Dessalegn amefanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam, amehudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mhe. Dkt. Magufuli kwa heshima yake na leo asubuhi ametembelea bandari ya Dar es Salaam ambapo amesema nchi yake ipo tayari kuitumia bandari hiyo sambamba na kuanzisha kituo cha huduma za usafirishaji wa mizigo kwa ndege (Cargo Hub) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kupitia shirika lake la ndege la Ethiopia Airline.


Emmanuel Buhohela
Kaimu Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi

Dar es Salaam

Rais Magufuli aiapisha kamati kuchunguza mchanga unaoshikiliwa kwenye makontena

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 01 Aprili, 2017 amewaapisha wajumbe wa kamati maalum ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya makontena yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
 
Hafla ya kiapo kwa wajumbe wa kamati hiyo imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Harold Nsekela na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
 
Kamati hiyo ya wanasayansi 8 walioteuliwa na Mhe. Rais Magufuli tarehe 29 Machi, 2017 inaongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Abdulkarim Hamis Mruma na itafanya kazi ya uchunguzi kwa siku 20 kisha kuwasilisha ripoti yake kwa Mhe. Rais.
 
Akizungumza baada ya kuwaapisha, Mhe. Rais Magufuli amesema ameamua kuunda kamati hiyo yenye wasomi waliobobea katika masuala ya jiolojia, kemikali na uchambuzi wa kisayansi ili wawawakilishe Watanzania zaidi ya Milioni 50 ambao wanataka kujua ukweli kuhusu rasilimali yao ya madini.
 
“Hivi sasa duniani kuna vita nyingi na vita mojawapo ni vita ya uchumi, kwa hiyo tunawatuma nyinyi mwende mkapigane vita hii katika sekta hii ya madini, mkawawakilishe Watanzania zaidi ya Milioni 50, mkapate ukweli wote na wala msikubali kuyumbishwa na mtu yeyote, tumieni utaalamu wenu, busara zenu, uzalendo wenu kwa Taifa na upendo wenu kwa Watanzania hasa masikini wenye shida nyingi” amesema Mhe. Rais Magufuli.
 
Mhe. Dkt. Magufuli amewahakikishia kuwa Serikali itatoa kila aina ya ushirikiano kufanikisha kazi hiyo na ametaka wawe huru kutumia vitendea kazi vyovyote vinavyohitajika zikiwemo maabara mbalimbali za taasisi za Serikali na nyinginezo.
 
“Nendeni popote mnapohitaji kufanya kazi tutawapa ushirikiano, fungueni makontena popote yalipo, chukueni sampuli na mkazipime mjue kilichomo na naviagiza vyombo vya dola vihakikishe hakuna mtu atakayewakwamisha”amesisitiza Mhe. Rais Magufuli
 
Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amesema baada ya kuunda kamati hii ya wanasayansi ataunda kamati nyingine ya wachumi na wanasheria kwa ajili ya kufanya tathmini na kuiangalia sera na sheria ya madini kwa lengo la kupata taarifa zaidi juu ya biashara ya madini hapa nchini.
 
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Kihindu ya BAPS Swaminarayan Sanstha Duniani Mtukufu Mahant Swami Maharaj ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku 7.
 
Pamoja na kumshukuru kwa ujio wake hapa nchini, Mhe. Rais Magufuli amemhakikishia kuwa Serikali ya Tanzania itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Jumuiya hiyo na amewaalika wafanyabiashara walio chini ya Jumuiya hiyo kuja nchini Tanzania kuwekeza katika viwanda, kilimo na shughuli nyingine za biashara na uwekezaji.
 
“Nimefurahishwa sana na ujio wako Mtukufu Mahant Swami Maharaj, sisi Tanzania tumekuwa tukishirikiana na Jumuiya ya Hindu tangu miaka mingi, nitafurahi kama mtaungana na juhudi za Serikali ya Tanzania kujenga viwanda, njooni mjenge viwanda na Serikali itawapa ushirikiano wowote mtakaohitaji” amesema Mhe. Rais Magufuli.
 
Mtukufu Mahant Swami Maharaj ambaye amefanya dua ya kuliombea Taifa na Rais, amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kukutana nae na amemhakikishia kuwa uhusiano na ushirikiano kati ya Jumuiya hiyo na Tanzania ulioanzishwa tangu enzi za utawala wa Awamu ya Kwanza ya Tanzania unaendelezwa na kukuzwa zaidi.
 
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
01 Aprili, 2017

Home kitaifa Kairuki: Serikali Haitamvumilia Mtumishi Mwenye Cheti Feki Kairuki: Serikali Haitamvumilia Mtumishi Mwenye Cheti Feki

Inakadiliwa kuwa watumishi 4,300 wapya wanataajiriwa kuajiriwa katika kada ya elimu na wasanifu wa maabara ambapo ajira hizo mpya zinakuja bada ya kukamilika kwa zoezi zima la kuhakiki watumishi hewa.

Hayo yamebainishwa mkoani Tabora na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma Mh. Angela Kairuki, wakati akizungumza na watumishi na wanachuo, ambapo amesema kuwa, kwa muda mwingi taifa limekuwa likikabiliwa na changamoto ya watumishi hewa huku likipoteza fedha nyingi.

Aidha Mhe. Kairuki amesema kuwa kamwe serikali haitamvumilia mtumishi ambaye atabainika kuwa na vyeti feki, huku akiwataka watanzania kutambua madhara ya vyeti hivyo kuwa ni kutopatikana kwa huduma stahiki huku akiwataka wahitimu katika kada mbali mbali kutowaonea haya watu ambao wanataka kupora ajira za wenzao.