Serikali yahamasisha wawekezaji viwanda vya kuongeza thamani

Serikali imewataka wawekezaji wa ndani na nje kutumia fursa zilizopo Tanzania hasa katika eneo la kuongeza thamani ya malighafi mbalimbali.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru alipokuwa akiongea na maafisa kutoka kampuni ya nchini Ufaransa ya Endel Engie mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Maafisa wa kampuni hiyo walikuwa nchini na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali waandamizi wa serikali kueleza nia yao ya kuwekeza Tanzania na kujua fursa zilizopo nchini.

Endel moja ya makampuni ya Engie Group yenye mapato yanayofikia Euro milioni 700 kwa mwaka na waajiriwa 6,000 nchini Ufaransa.

Baadhi ya shughuli za kampuni hiyo ni katika maeneo ya sayansi za anga, viwanda vya vyakula, reli, gesi, ujenzi wa meli, nishati ya nyuklia na viwanda vya chuma miongoni mwa vingine.

Kwa bara la Afrika, kampuni hiyo inafanya kazi katika nchi za Afrika ya Kusini, Angola na Congo DRC.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano huo, Dkt. Meru alisema eneo la kuongeza thamani bado halijafanyiwa kazi na lina fursa kubwa kwa watu wanaotaka kuwekeza katika viwanda vya aina hiyo.

“Kama serikali tunaweka mazingira mazuri ya kuhakikisha kuwa watu wanawekeza kwa faida ya pande zote mbili,” alisema.

Aliwaambia maafisa wa kampuni hiyo kuwa utulivu wa kisiasa na amani iliyopo Tanzania vinaifanya kuwa eneo bora la kuwekeza katika ukanda huu wa Afrika.

Kampuni hiyo iko katika mchakato wa kutafuta fursa na vivutio vya kuwekeza katika nchi za Tanzania, Kenya na Msumbiji.

Aliyataja maeneo mengine yenye fursa za kuwekeza kama madini, Kilimo, utafutaji wa gesi na mafuta na uzalishaji nishati miongoni mwa nyingine.

Makamu wa Rais, Maendeleo ya Kimataifa, Endel Engie, Bw. Olivier Rousseau alisema wamevutiwa na hali ya amani, utulivu na raslimali katika eneo hili la Afrika na hasa Tanzania.

“Tuko katika ziara ya kujifunza,” alisema.

Kwa mujibu wa afisa huyo, mwezi wa Kumi mwaka huu, wawakilishi wa kampuni hiyo, watarudi Tanzania na mapendekezo rasmi ya maeneo watakayokuwa wanataka kuwekeza hapa nchini.

Mbunge mstaafu wa jimbo la Mbinga Magharibi ambaye aliambatana na wawekezaji hao, Bw. Gaudence Kayombo alisema huu ni wakati wa kuitikia kwa vitendo azma ya serikali ya kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda.

Alisema uwekezaji katika maeneo hayo utasaidia kuleta teknolojia, mitaji na uzoefu Tanzania.

Serikali imedhamiria kuwa ifikapo mwaka 2020, asilimia 40 ya ajira zote  na asilimia 15 ya pato la Taifa vitokane na sekta ya viwanda.

MASAUNI ASISITIZA USAFI WA MAZINGIRA KIKWAJUNI ZANZIBAR

 WANANCHI wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar, wametakiwa kujenga tabia ya kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kuepuka maradhi ya kipindupindu yanayoathiri maeneo mbali mbali nchini.

Wito huo umetolewa kwa nyakati tofauti na Mbunge wa jimbo la Kikwajuni, Muandisi Hamad Yussuf Masauni alipokuwa akifanya usafi wa mazingira katika maeneo mbali mbali ya jimbo hilo Mjini hapa.

Alisema maeneo mengi ya jimbo hilo hasa katika Majumba ya Maendeleo ya Michenzani ni machafu sana  hali inayoweza kusababisha maradhi ya miripuko yakiwemo kipindupindu na kichocho.

Masauni ambaye pia ni Naibu Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, alieleza kuwa wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa mazingira na kupelekea uharibifu wa miundombinu ya kusafirisha maji taka ikiwemo mitaro kuziba.

“ Nachukua fursa hii kuwakumbusha wananchi wa kikwajuni kuwa suala la usafi wa mazingira halina itikadi za kisiasa ni lazima wananchi sote tuungane bila ya kujali tofauti za kisiasa.

Pia nakuombeni wananchi hasa mnaoishi katika majumba ya michenzani mbadilike kwa kujali mazingira yenu kwani mjue kuwa endapo eneo hili litapata maradhi ya mripuko kuna hatari ya wananchi wengi kupoteza maisha kwa maradhi ambayo tuna uwezo wa kuyazuia.”, alisema Masauni huku akisisitiza umuhimu wa kufanya usafi wa mara kwa mara katika maeneo hayo.

Alisema viongozi wa jimbo hilo kwa sasa wanapanga kuanzisha kikundi maalum cha vijana wa kufanya usafi katika maeneo ya jimbo hilo, ambapo kila kaya(nyumba) watakuwa wanachangia kiasi cha shilingi 200 kila siku ili fedha hizo ziweze kuwasaidia watu wanaofanya usafi huo.

 “Aibu kubwa kuona ndani ya jimbo la kikwajuni panaanza kupatikana wagonjwa wa maradhi ya kipindupindu kwani ni jimbo lenye sifa ya usafi na ukaribmu toka enzi na enzi tena lipo mjini, lazima tushirikiane kufanya usafi katika maeneo yetu.” Alisema Masauni.

Aidha aliishauri Manispaa ya Zanzibar kuanza mara moja utafti wa kubaini mifumo ya maji machafu na masafi inayoingiliana katika maeneo hayo ili kuifanyia matengenezo kwa haraka kabla hapajatokea maafa ya maradhi ya miripuko na kusababisha athari kwa wananchi wa maeneo hayo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salum Ali(Jazeera) aliwapongeza wananchi wa jimbo hilo waliojitokeza kufanya usafi wa mazingira kwa lengo la kuweka maeneo yako katika hali ya usafi.

Jazeera alisema kwamba kinga ya maradhi ya mripuko hasa kipindupindu ni usafi wa mazingira hivyo kila mwananchi anatakiwa kutekeleza wajibu wake bila ya kulazishwa na mtu.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Zanzibar, Aboud Hassan Serenge alisema kila mwananchi ana jukumu la kufanya usafi wa mazingira katika maeneo anayoishi kwa lengo la kuweka mji wa Zanzibar katika hali ya usafi.

Serenge alifafanua kwamba kuna baadhi ya wananchi wamekuwa wakichafua mazingira ya mji kwa makusudi huku wakidai kuwa Manispaa ipo na ndiyo yenye dhamana ya kufanya usafi jambo ambalo sio sahihi kwani kila mtu suala la usafi linamuhusu.

Mkurugenzi huyo alieleza kuwa endapo wananchi wa manispaa ya Zanzibar wataendelea kushirikiana vizuri na mamlaka hayo katika kuweka mjini wa Zanzibar katika hali ya usafi, basin chi itarudi katika historia ya haiba na usafi uliotukuka kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Alisema Manispaa ina mpago wa kufanya marekebisho katika maeneo mbali mbali ya mji wa Zanzibar yanayoonekana kuwa na tatizo la kuziba kwa mitaro na mifereji ya maji machafu inayopita chini kwa chini ili kuzuia uchafu unaosambaa katika maeneo mbali mvali ya mji huo.

LUBUVA AKABIDHI MIKANDA,VIRUNGU VYA ULINZI NA MAKOTI YA MVUA KWA WANAKIKUNDI CHA ULINZI SHIRIKISHI OYSTERBAY JIJINI DAR.

 Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva awakabidhi mikanda, virungu na makoti ya kujikinga na mvua kwa wanakikundi cha ulinzi shirikishi cha mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Pia alizungumza na wananchi wa mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam ili kujua changamoto za wananchi wa mtaa huo katika nyaza za ulinzi, usalama na Usafi wa mazingira.

 Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva akifafanua jambo alipokuwa akisoma ripoti ya Mtaa wake katika ulinzi , usalama na usafi wa mazingira ya mtaa wa Oyster bay jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Oysterbay, Achema Kalembo akisoma taarifa ya mapato na matumizi ya Mtaa wa Oysterbay mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati  Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva alipokuwa akizungumza na wanamtaa huo ili kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wake.
Baadhi ya wananchi wakichangia maada katika mkutano wa  wananchi wa  Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva akiwakabidhi Virungu, Mikanda na Makoti kwa wanakikundi cha ulinzi shirikishi wa mtaa wa Osyterbay mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  
 Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Oysterbay, Achema Kalembo  akizungumza na mwandishi wetu mara katika mkutano wa wananchi wa mtaa wa Oysterbay  walipokuwa wakizungumza na   Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Meza kuu wakisikiliza hoja za wananchi. 
 Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva akizungumza na mwandishi wetu mara baada ya kukabidhi mikanda, virungu na makoti kwaajili ya mvua kwa wanakikundi cha Ulinzi shirikishi wa mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Timu ya Bunge Sports Club kucheza na timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kesho

Timu ya Mpira wa miguu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania Bunge Sports Club inatarajiwa kushuka dimbani kucheza mchezo mkali na wa aina yake ambao ni wa kwanza na timu ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.


Mapema leo Aprili 25.2016 timu hiyo ilishuka katika dimba hilo la Amani na kupasha misuli maalum kwa hiyo mchezo huo wa hiyo kesho ambapo kwa mujibu wa viongozi wa timu hiyo ya Bunge wametamba kuibuka na ushindi wa kishindo.
Kocha wa timu hiyo ambaye pia Mbunge Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mh. Venance Mwamotto ametamba kwa timu yake kuibuka na ushindi mnono katika mchezo huo kwani wana mazoezi ya kutosha na pia wamejiandaa kuonyesha uwezo.
“Tunawaomba wabunge wote kutuunga mkono katika mchezo huu kwani tmu imejindaa vya kutosha kuhakikisha tunashinda. Mchezo huu ni maalum kwa ajiri ya kuimalisha Muungano wetu tukufu hivyo tutaendelea kuuenzi na kuukumbatia na sote kwa pamoja tuzidishe Amani” alieleza Mh. Mwamotto.
Kwa upande wake Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Mh. Steven Ngonyani 'Maji Marefu' ambaye ni miongoni mwa viongozi wa msafara wa timu hiyo ya Bunge ametamba timu yake kuibuk na ushindi mnono kwani wamejiandaa kisaikolojia na mazoezi ya kimichezo.
Naye Mbunge wa Nzega Vijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla viongozi wa timu hiyo ya Bunge amebainisha kuwa, mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya Saa 12 Jioni kesho Aprili 26.2016 katika uwanja huo wa Amani.
“Mechi kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Utachezwa kesho ni siku ya Kuadhimisha Muungano wa Nchi ya Jamhuri ya Tanganyika Na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Tunawaomba watu kujitokeza kwa wingi kuuona mchezo huu ambao utakuwa wa aina yake kwa timu zote mbili.” Alieleza DK. Kigwangalla.
Timu hiyo ya Bunge yenye wachezaji Zaidi ya 19 imejiandaa vya kutosha katika kuakikisha inapata ushindi mnono na ipo Visiwani hapa kwa maandalizi ya mchezo huo tokea jana na leo imeweza kufanya mazoezi ya awali asubuhi na mengine wakitarajia kufanya hapo jioni.
Timu ya Bunge ikifanya mazoezi yake mapema leo Aprili 25 kuajiandaa na mchezo huo utakaochezwa keshi Jioni uwanja wa Amani.
Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Mh. Steven Ngonyani 'Maji Marefu' akisimamia mazoeszi hayo kwa muda wakati wsa asubuhi ya leo
mazoezi hayo yakiendelea..
Mazoezi yakiendelea
Kocha wa timu hiyo ambaye pia Mbunge Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mh. Venance Mwamotto (kati) akitoa maelezo ya mazoezi hayo.
Benchi la ufundi likiwa tayari katika mazoezi hayo.
Mbunge William Ngeleja akijaribu kutaka kuchukua mpira kwa Naibu Waziri wa Afya Dk. Hamisi Kigwangalla.
Mazoezi moto moto yakiendelea..
Mazoezi makali ya timu ya Wabunge yakiendelea katika uwanja wa Amaan, Unguja leo Aaprili 25.2016. Timu hiyo kesho Aprili 26 inatarajia kucheza mchezo wao dhidi ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. (Picha zote na Andrew Chale, Zanzibar).

KURASA ZA MAGAZETI YA HARDNEWS NA BURUDANI JUMATATU APRILI 25,2016


20160425_045601
20160425_045615
20160425_045624
20160425_045637
20160425_045647
20160425_045655
20160425_045704
20160425_045714
20160425_045731
20160425_045740
20160425_052303
20160425_052312
20160425_052335
20160425_052345
20160425_052355
20160425_052403
20160425_052414
20160425_052517
20160425_052547
20160425_052615
20160425_052700
20160425_052711

ALI HASSAN MWINYI HANDS OVER UGANDA ELECTION OBSERVATION REPORT TO EAC SECRETARY GENERAL

H.E. Ali Hassan Mwinyi, Former President of the United Republic of Tanzania and Amb. Dr Richard Sezibera, EAC Secretary General in discussion
L-R; Hon Peter Mathuki, EALA MP, H.E. Ali Hassan Mwinyi and Dr Richard Sezibera display EAC Observer Mission Report 

H.E. Ali Hassan Mwinyi, Former President of the United Republic of Tanzania, over the weekend presented Amb. Dr Richard Sezibera, the EAC Secretary General, with the final observation report from the recently concluded General Elections held in 18th February 2016, in the Republic of Uganda. The ceremony took place at the residence of the Former President in Dar es salaam, Tanzania.

“I was very happy to observe the patience and orderliness with which the people of Uganda conducted her General Elections," said H.E. Ali Hassan Mwinyi. “These and many other things that have also been highlighted in the report, can be used as benchmarks for which other countries can borrow good practices from,” he added.

While receiving the Report, the Secretary General thanked the Former President for his leadership and commitment to the EAC Elections Observers Mission, adding that, “the cooperation between the EAC and other stakeholders led to sustainable peace in the country."

The report consists of recommendations to streamline and improve the electoral process for future in the Republic of Uganda. The EAC Observer Mission Report will be submitted to, among others, the Electoral Commission of Uganda, through the EAC Council of Ministers for consideration and implementation.