NDOA ZA UTOTONI BADO ZIPO MKOANI IRINGA

Hawa ni baadhi ya wananchi wa kabila la kimasai ambalo linakaliwa na tuhuma za kuozesha wasicha wenye umri mdogo.


 

Hili ni jengo la shirika lisilo la kiserikali la Ilula Ophan program (IOP)



Na fredy mgunda,Iringa
 


Shirika lisilo la kiserikali la Ilula Ophan program (IOP) limeendelea kukemea na kutoa elimu juu ya ndoa za utotoni kwa kuwa zinarudisha maendeleo nyuma ya wasichana wa jamii ya kimasai.



Akizungumza na blog hii Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Ilula Ophan program (IOP) Edson Msigwa alisema kuwa tatizo la ndoa za utotoni katika kabila la wamasai bado ni kubwa.



Msigwa alieleza jinsi gani wanavyofanya shughuli za kukemea na kutoa elimu juu ya ndoa za utotoni katika jamii ya wamasai



“Tunajitahidi kuwafikia jamii zote za wilaya ya kilolo mkoani iringa kwa lengo la kutoa elimu lakini tunakumbana na changamoto kutoka kwa wazazi ambao bado wana mila potofu hasa huku umasaini”alisema Msigwa



Aidha Msigwa alisema kuwa kila siku ndoa za utotoni zinaongezeka huko vijijini  na kuitaka serikali kukubali takwimu wanazozitoa kwa kuwa zinaukweli.



“Sisi hapa Ilula Ophan program (IOP) tunaishi na wasichana wa kabila la kimasai wafanikiwa kukimbia kuozeshwa wakiwa na umri mdogo hebu mwangalie huyo motto joyce alivyo alitakiwa aolewe na umri huu wa miaka kumi nan ne je unafikiri ni haki jamiii inatakiwa kubadili na serikali inatakiwa kuongeza juhudi kulitatua hili”alisema Msigwa



Naye mmoja wa wasichana wa kimasai aliyekimbia kuolewa akiwa na umri mdogo Joyce Hassani alisema kuwa msichana wa kimasai wakimaliza elimu ya msingi wanalazimishwa kuolewa na familia yake.



“Mimi na mwenzangu tumemaliza shule tu wametupeleka kucheza ngoma kisha kutaka kutuozesha lakini mungu mwema tulifanikiwa kukimbia na kufika hapa Ilula Ophan program (IOP) japo kuwa wanaume wa kimasi wanakuja hapa kituoni mara kwa mara kutaka kutuiba turudi kule umasaini ili tukaolewe hasa kaka zangu”alisema joyce



Joyce ameiomba serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kusaidia kupambana na mila potofu zinazowapotezea malengo wasichana wa kimasai.



“Angalia tunavyoteseka saizi tunaishi kama watoto yatima wakati wazazi wetu wapo na wana afya zuri kabisa lakini tatizo kubwa sisi wasichana wadogo wa kimasai tunaolewa tukiwa na umri mdogo sana tunaomba jamii iamuke na kutusaidia kutatua tatizo hilo.”alisema Joyce



Zipo sababu nyingi na ushahidi mwingi wa kisayansi, unaonyesha kuwa, ndoa na mimba katika umri mdogo ni hatari kwa afya na mstakabali wa maisha yake na mtoto wake.



Wasichana wanaopata ujauzito na kujifungua katika umri mdogo wengi wao pia hupata tatizo la fisitula - Vescovaginal fistula.



Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na chama cha waandishi wahabari wanawake (TAMWA) umeonesha kuwa katika mwaka 2012-2013 matukio 228 ya mimba na matukio 42 ya ndoa za utotoni yaliripotiwa nchini tanzania.

HAWA NDIO VIGOGO WATATU WA TANESCO WALIOSHUSHWA VYEO

Vigogo  watatu ambao ni wakurugenzi katika Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), makao makuu Dar es Salaam, wameshushwa vyeo huku mmoja akiamua kuacha kazi mwenyewe.

Hatua hiyo imekuja siku nne tangu Rais Dk. John Magufuli atengue uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi Felchesmi Mramba.

Mramba alitenguliwa uteuzi wake siku chache baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), kutangaza kuridhia ombi la Tanesco la kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 8.5 kutoka 18 waliyoomba.

Wakurugenzi hao wamesimamishwa jana kupisha uchunguzi, huku chanzo cha kusimamishwa kwao kikiwa hakijaelezwa.

Taarifa kutoka ndani ya Tanesco ambayo ilithibitishwa na Kaimu Mkurugenzi mpya wa shirika hilo, Dk. Tito Mwinuka kwa simu jana, ilieleza kusimamishwa kwa vigogo hao ambao walikuwa wasaidizi wa karibu wa Mramba katika utendaji.

“Ni kweli wamesimamishwa, lakini kwa kuwa sikuwa ofisini ngoja niisome vizuri taarifa iliyopo mezani kisha niwatumie taarifa iliyokuwa sahihi kuhusiana na hilo.

“Hapa nilipo nipo ofisini na ofisa habari wangu (hakumtaja jina) tunaandaa taarifa ya pamoja, kwa maana kila mmoja anapiga simu kutaka taarifa, hivyo siwezi kuzitoa nusu nusu,’’ alisema Dk. Mwinuka.

Taarifa zinaeleza kwamba wakurugenzi watatu wameshushwa vyeo na kuhamishiwa katika Chuo cha Mafunzo cha Tanesco (TSS) kwa madai kuwa shirika linaboresha ufanisi wake.

Walioshushwa vyeo ni pamoja na Declan Mhaiki ambaye alikuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji aliyekuwa anashughulikia usambazaji wa umeme.

Hata uamuzi huo unachukuliwa inaelezwa kuwa Mhaiki alikuwa kwenye msiba wa kaka yake mkoani Ruvuma, marehemu Kapteni Keenan Mhaiki.

Kapteni Mhaiki aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), alifariki dunia mapema wiki hii.

Wengine walioshushwa vyeo na kuhamishwa ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uzalishaji na Huduma kwa Mteja, Mhandisi Sophia Mgonja na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uzalishaji Umeme, Nazir Kachwamba.

Wakati hao wakipigwa na panga hilo, Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu, Watson Mwakyusa, aliamua kuandika barua kuacha kazi mwenyewe.

Januari Mosi mwaka huu, Rais Magufuli alimteua Dk. Mwinuka kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, baada ya kumng’oa aliyekuwa mkurugenzi wa shirika hilo, Mhandisi Mramba.

Kabla ya uteuzi huo, Dk. Mwinuka alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Akiwa mjini Bukoba kwenye ibada ya Mwaka Mpya, Rais Magufuli alisema amekerwa na kusikitishwa na vitendo vya baadhi ya watumishi wa umma kujitokeza hadharani na kutangaza au kuzungumzia mambo ya kitaifa kama uamuzi wa Serikali bila kushirikisha viongozi wao wa ngazi za juu.

Kutokana na hali hiyo, alisema watendaji hao ni miongoni mwa majipu yanayostahili kutumbuliwa.

Hatua ya kutumbuliwa kwa Mramba ilikuja siku moja baada ya Ewura kutangaza kuridhia ombi la Tanesco la kupandisha bei ya umeme.

Lowassa, Maalim Seif kushambulia jukwaa Dimani



Dar es Salaam. Vigogo wawili wa siasa za upinzani nchini, Edward Lowassa na Maalim Seif Sharif Hamad kesho watapanda jukwaani katika Skuli ya Fuoni, Zanzibar kumnadi mgombea ubunge Jimbo la Dimani kwa tiketi ya CUF, Abdulrazaq Khatib Ramadhan.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Lowassa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani na Maalim Seif aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika Serikali iliyopita, waligombea urais wa Jamhuri ya Muungano na Zanzibar, mtawalia.

Uchaguzi huo wa Dimani, utafanyika Jumapili Januari 22, kujaza nafasi iliyoachwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Hafidh Ally Tahir aliyefariki dunia Novemba 11, mwaka jana katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

Chini ya ushirikiano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), jana Chadema kilitangaza utaratibu jinsi vigogo wake watakavyoshiriki kampeni za uchaguzi huo kwa staili tofauti ili kuhakikisha mshirika wake CUF anaibuka kidedea.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu alisema jana kwamba kesho, Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu, atakuwa kiongozi wa kwanza wa Chadema kuhudhuria kampeni hizo akishirikiana na Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF.

PICHA ZIKIONYESHA JENGO LA BILLCANAS YA MBOWE LINAVYOBOMOLEWA LIVE NA NHC




Shirika  la Nyumba la Taifa (NHC) limeanza kubomoa jengo la iliyokuwa Klabu Bilicanas na ofisi za Free Media inayomiliki gazeti la Tanzania Daima zinazomilikiwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe, lililopo makutano ya barabara ya Mkwepu na Indira Gandhi lenye kitalu namba 725-726/24 na hati namba C. T No. 186018/15 and C. T No. 186018/10.

Ubomoaji huo ulioanza jana unafanyika wakati Mbowe ameingia katika mgogoro na NHC baada ya kampuni ya udalali ya Poster and General Traders kumtolea vyombo nje mwanzoni mwa Septemba, mwaka jana kwa kudaiwa Sh bilioni 1.2 ambayo ni deni la pango ya miaka 20.

Mwanzoni mwa Septemba, mwaka jana NHC kwa kushirikiana na Kampuni ya Poster and General Traders, ilifika katika jengo hilo kwa maelekezo ya kutoa  thamani mbalimbali zilizokuwa katika ofisi za jengo hilo na kumpa Mbowe siku 14  kulipa deni analodaiwa na kuweza kugomboa mali hizo.

Mpango huo ulisimamiwa na Meneja wa Ukusanyaji Madeni wa NHC, Japhet Mwanasenga na alisema Mbowe alikuwa na muda wa wiki mbili kwa wakati huo kulipa fedha hizo kabla ya vifaa vyake kupigwa mnada.

Mwanasenga alisema taratibu zote zilifuatwa kabla ya kumwondoa mteja huyo ikiwamo notisi na kwamba vifaa hivyo vitashikiliwa kwa muda huo na endapo akishindwa kulipa jengo hilo atapangishwa mtu mwingine.

Alisema shirika hilo linahitaji fedha kwa ajili ya ujenzi na uendelezaji wa majengo yake hivyo mteja anayedaiwa ajiandae kuondolewa wakati wowote huku baadhi ya watu wakilihusisha tukio la Mbowe kuondolewa katika ofisi hizo na masuala ya siasa.

Hata hivyo, Mwanasenga, alisema uamuzi wa kumwondoa katika ofisi hizo hauna uhusiano na masuala ya siasa.

Kutokana na hali hiyo, Mbowe kupitia Mawakili wake, John Malya na Peter Kibatala, walifungua shauri la kupinga kuondolewa katika jengo hilo Mahakama Kuu ya Tanzania na kutaka kurudishwa katika jengo hilo.

Hata hivyo, maombi hayo yalitupiliwa mbali Oktoba 17, mwaka jana na Jaji Sivangilwa Mwangesi na kusema kuwa mahakama hiyo imechukua uamuzi huo baada ya kujiridhisha na hoja kuu tatu kuwa hakuna mkataba wa ubia uliopo baina ya NHC na Mbowe Hotels Limited na kuwa uhusiano pekee uliosalia ni wa mpangaji na mpangishaji.

Pia Jaji Mwangesi alisema mahakama imejiridhisha kuwa NHC imefuata taratibu zote katika kuiondoa Mbowe Hotels Limited kwa kutoa ilani ya siku 30 na baadaye siku 14 kabla ya kumtoa mteja wao huyo.

Kuhusu kusajiliwa au kutosajiliwa kama dalali rasmi wa mahakama wa kuendesha mchakato wa kumhamisha Mbowe katika jengo hilo, alisema hiyo nayo haikuwa hoja yenye mashiko na kwamba waombaji walitakiwa kuwasiliana na Msajili wa Mabaraza ya Ardhi.

Katika shauri hilo, NHC iliongozwa na Wakili Kiongozi, Aloyce Sekule na Ipilinga Panya na mawakili wake wengine waliojikita katika kujibu hoja zilizokuwa zikitolewa na wateja wao.

UVCCM LONGIDO YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA

 Kushoto ni Katibu  wa UVCCM wilaya ya Longido Isaya Karakara, Katibu Hamasa wa UVCCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel  na Mjumbe Baraza Kuu  UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko w akikabidhi msaada kwa Mmiliki wa kituo cha kulelea Watoto yatima cha Masai Foundation  Joyce Kabati


 Kushoto ni Katibu  wa UVCCM wilaya ya Longido Isaya Karakara, Katibu Hamasa wa UVCCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel  na Mjumbe Baraza Kuu  UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko w akikabidhi msaada kwa Mmiliki wa kituo cha kulelea Watoto yatima cha Masai Foundation  Joyce Kabati




  habari picha na Mahmoud Ahmad,Arusha.



Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Longido umetembelea kituo cha Watoto yatima na Wanaoishi katika mazingira magumu cha Masai Foundation kilichopo mji mdogo wa Namanga na kutoa msaada wa vyakula pamoja na vifaa mbalimbali.





Mjumbe Baraza Kuu  UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko Amesema kuwa wameamua kushirikiana na jamii katika kusaidia watoto ikiwa ni moja kati ya michango wanayoitoa ili kutosheleza mahitaji muhimu yanayohitajika katika kituo hicho.





Robert Amesema kuwa jukumu la kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ni la kila mwanajamii hivyo jamii inapaswa kujitoa kusaidia watoto hao.





Katibu Hamasa wa CCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel amesema kuwa vijana hao wameamua kujitoa kutoa msaada kwa jamii ili kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hivyo ameiomba jamii kujitokeza kwa wingi kuwasaidia watoto hao.





“Hawa ni watoto wetu sote kila mtu anapaswa kuona kuwa ana jukumu la kuwasaidia hawa watoto ili waweze kufanikisha ndoto zao”  Neema





Katibu  wa UVCCM wilaya ya Londigo Isaya Karakara na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya Tulli Lemanga aliyejitolea kuwakatia bima ya afya watoto wanaolelewa katika kituo hicho wamesema  kuwa vijana hao wataendelea na utamaduni huo mara kwa mara katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua changamoto za watoto.





Mmiliki wa kituo hicho Joyce Kabati amewashukuru vijana hao kwa kutembelea watoto hao jambo ambalo linaleta faraja kwa watoto hao ambao na wanamahitaji mbalimbali ambayo yamewasilishwa na vijana hao.

WAFAHAMU WALIONYAKUA TUZO MZA WACHEZAJI AFRIKA

               
(1)Mchezaji bora wa mwaka wa Afrika  Riyad MAHREZ (Algeria & Leicester City). nafasi ya pili ni Pierre-Emerick AUBAMEYANG (Gabon & Borussia Dortmund),na Sadio MANE (Senegal & Liverpool) anashika nafasi ya tatu.

(2)Mchezaji bora wa mwaka wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza barani Afrika ni Denis ONYANGO (Uganda & Mamelodi Sundowns).

(3)Mchezaji bora wa mwaka wa Afrika upande wa wanawake ni Asisat OSHOALA (Nigeria & Arsenal Ladies)
(4)Mchezaji bora kijana  anayechipukia.Kelechi IHEANACHO (Nigeria & Manchester City)
(5)Mchezaji bora kijana Alex IWOBI (Nigeria na Arsenal)
(6)Kocha bora wa mwaka Pitso MOSIMANE (Mamelodi Sundowns)
(7)Club bora ya mwaka ni Mamelodi Sundowns.
(8)Timu bora ya taifa ni Uganda
 (9)Timu bora ya taifa upande wa wanawake ni Nigeria
(10)Mwamuzi bora wa mwaka ni Bakary Papa GASSAMA (Gambia)  
(11)Kiongozi bora wa mpira ni Manuel LOPES NASCIMENTO, Raisi wa shirikisho la mpira la Guinea Bissau
(12)Tuzo za heshima kwa magwiji wa zamani zimekwnda kwa
Laurent POKOU -mchezaji wa zamani wa  Cote d’Ivoire na Emilienne MBANGO - mchezaji wa zamani wa Cameroon.
(13)Tuzo ya Platinum imekwenda kwa
Mheshimiwa  Muhammadu Buhari, Raisi  wa  Nigeria



(14)Kikosi cha kwanza cha mwaka cha Afrika.

Golikipa:
 Denis ONYANGO (Uganda & Mamelodi Sundowns)

Walinzi: 
Serge AURIER (Cote d’Ivoire & Paris Saint-Germain), Aymen ABDENNOUR (Tunisia & Valencia), Eric BAILLY (Cote d’Ivoire & Manchester United), Joyce LOMALISA (DR Congo & AS Vita)

Viungo: 
Khama BILLIAT (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns), Rainford KALABA (Zambia & TP Mazembe), Keegan DOLLY (South Africa & Mamelodi Sundowns),

Washambuliaji:
 Pierre-Emerick AUBAMEYANG (Gabon & Borussia Dortmund), Sadio MANE (Senegal & Liverpool), Riyad MAHREZ (Algeria & Leicester City)

Wachezaji wa akiba
Aymen MATHLOUTHI (Tunisia & Etoile du Sahel), Kalidou KOULIBALY (Senegal & Napoli), Salif COULIBALY (Mali & TP Mazembe), Islam SLIMANI (Algeria & Leicester City), Mohamed Salah (Egypt & Roma), Kelechi IHEANACHO (Nigeria & Manchester City), Alex IWOBI (Nigeria na Arsenal)

Wakuu wa wilaya za Arusha wabebeshwa mzigo mzito.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza kulia) akizungumza katika kikao cha maandalizi ya Bajeti 2017/2017 na mapitio ya Bajeti 2015/2016.
Na Mahmoud Ahmad, Arusha
Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Arusha wameagizwa kusimamia Halmashauri zao kujibu hoja zote zilizowasilishwa na  Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa  Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 kabla ya kufika mwisho wa juma lijalo.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo  wakati wa Kikao  cha maandalizi ya Bajeti ya mwaka 2017/2018 na mapitio ya bajeti ya nusu mwaka wa Fedha 2016/2017 kilichohusisha Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha  na wataalam toka Ofisi ya Mkaguzi wa hesabu za Serikali.
Akitoa Agizo hilo Mhe. Gambo alisema “Nataka kila Halmashauri ikamilishe ujibuji wa Hoja kwa wakati na kwa majibu sahihi sio kufanya majibu ambayo yanaibua hoja zaidi au hayajitoshelezi na kwa Halmashauri ambayo ilipata Hati Chafu au Hati ya Mashaka kwa mwaka uliopita ianishe wataalamu waliopelekea Halmashauri kupata Hati hizo ili waweze kuchukuliwa hatua Stahiki”.
Wakuu wa Wilaya mshiriki Kikamilifu kuhakikisha hoja zinajibiwa ipasavyo na wale waliosababisha hoja hizo kwa kipindi cha nyuma wanachukuliwa hatua ili kuleta nidhamu ili kuongeza umakini katika zoezi zima la ujibuji wa Hoja alisema Gambo.
Aliongeza kuwa “Sitamueleza Mkuu wa Wilaya ambaye Halmashauri yake itapata Hati Chafu au ya Mashaka kwa hesabu za mwaka ulioisha, Mkasimamie Halmashauri zenu kwa nguvu zenu zote na katika hili sitamuonea mtu haya”.
Katika mapitio ya Bajeti ya inayoendelea alizitaka Halmashauri ambazo hazijatoa asilimia kumi ya mapato yao kama mikopo kwa vikundi vya wananwake na vijana zikatoe Fedha hizo kabla ya mwisho wa Januari ili kuweza kuinua uchumi wa makundi haya yaliyoainishwa kwa mujibu wa Sera na Maelekezo.
“Katika hili napenda kuwapongeza Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kukamilisha utoaji wa mikopo  zaidi ya Mil 600 kwa robo ya kwanza naya Pili kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 lakini halmashauri zingine zote hazijakamilisha utoaji wa Mikopo inayotakiwa kwa kipindi cha nusu mwaka.”
Awali katika Kikao hicho akiwasilisha mapitio ya Bajeti 2015/2016 na Mpango wa Bajeti 2016/2017 Katibu Tawala Msaidizi huduma za Mipango Bi. Grace Mbaruku alisema Halmashauri zote zinatakiwa kuandaa Bajeti Mpya kwa kuzingatia vipaumbele vilivyowekwa katika muongozo wa Bajeti.
 Halmashauri haitazingatia vigezo vilivyowekwa inaweza kupelekea bajeti yao kukwama katika ngazi za juu hivyo zingatieni vigezo kama kutenga Fedha za Lishe kwa ajili ya kutokomeza udumavu kwa Watoto alisema Bi. Mbaruku.
Akiwasilisha Taarifa ya Changamoto zinaowakabili katika Usimamizi wa Halmashauri Katibu Tawala Msaidizi anayesimamia Serikali za Mitaa Bi. Susane Mnafe aliainisha ucheleweshaji wa uwasilishaji wa Taarifa toka Halmashauri mara zinapohitajika, kutofuata mfumo elekezi wa uwasilishaji wa Taarifa.
Aliongeza kuwa kutokua na kanzidata ya vyanzo vya mapato na uandaaji wa Bajeti ya Halmashauri kabla ya Sheria ndogo mpya kupitishwa huchangia kukwamisha ukusanyaji wa mapato kwa kutumia viwango vipya.