FREEDOM HOUSE YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI WA MITANDAO YA KIJAMII


1
Clerance Kipobota kutoka Shirika la Freedom House  ambaye amemwakilisha mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo akifungua semina ya (Alternative Media) kwa  waandishi wa habari za Mitandao ya kijamii (Online Platform Reporters) inayofanyika kwenye Hoteli ya  Flomi mjini Morogoro.
……………………………………………………………
Shirika la Kimataifa la Freedom House linaendesha mafunzo kwa waandishi wa habari wa  mitandao ya kijamii ‘bloggers’ kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu namna kuendesha vyombo vya habari mbadala.
Mafunzo hayo ya siku mbili ‘Julai 26 – 27,2018’ kuhusu Vyombo vya habari mbadala ‘Alternative Media’ yaliyoratibiwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari  Tanzania (UTPC) yanafanyika katika ukumbi wa Flomi Hotel mkoani Morogoro.
Awali akifungua mafunzo hayo,Mwakilishi wa Mkurugenzi wa shirika la Freedom House Clarence Kipobota alisema kupitia mafunzo hayo waendeshaji wa mitandao ya kijamii watajifunza mbinu mbalimbali kuhusu namna ya kuendesha mitandao yao.
“Tutajengeana uwezo na kujadili na kuunda jukwaa moja la waandishi ambao wanatumia Alternative Media”,alieleza.
4
Mwezeshaji wa semina hiyo Bw. Daniel Lema akitoa mada kwa waandishi wa habari katika semina inayofanyika katika hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
kadam
Mwezeshaji John Kaoneka akitoa mada katika semina hiyo kuhusu mitandao ya kijamii.
23
567  1011121314151617
Victor Maleko Afisa Mafunzo , Utafiti na Machapisho UTPC akiwa katika semina hiyo.
18
Picha mbalimbali zikionyesha washiriki wa semina hiyo
1920
9
Waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua semina hiyo.
9

WAZIRI KIGWANGALLA ATOA SIKU 90 KWA TAWIRI KUFANYA SENSA YA MAMBA ZIWA RUKWA NA TFS KUANDAA MPANGO WA KITAIFA WA UVUNAJI MISITU



Na Hamza Temba, Songwe
…………………………………………………………..
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa miezi mitatu kwa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kufanya utafiti na sensa ya mamba katika ziwa Rukwa ili kubaini idadi yake na hatimaye kuishauri Serikali namna ya kudhibiti madhara yanayosababishwa na mamba hao kwa wananchi hususan wa jimbo la Songwe ikiwemo kuwavuna kama idadi yao itabainika kuwa kubwa kupita kiasi.
 
Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana katika kijiji cha Maleza, kata ya Mbangala, wilaya ya Songwe mkoani Songwe alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kwa ajili ya kutatua mgogoro uliopo baina ya wananchi na Mamba wa ziwa Rukwa.
 
“Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori ambayo ipo chini ya wizara yangu, nawaagiza wafike hapa mara moja, ndani ya miezi mitatu wanipe majibu nini kifanyike kupunguza madhara yanayotokana na mamba kwenye ziwa Rukwa, wafanye sensa watuambie kuna Mamba wangapi lakini pia watushauri nini tufanye ili kudhibiti mamba hao wasiendelee kusababiaha athari kubwa kwenye maisha ya watu wanaoishi jirani, lakini pia wanaoutumia ziwa.
 
“Kwa sababu madhara yanaweza yakawa mengi, inawezekana mamba wameshakuwa wengi na samaki wamebaki wachache, kwahivyo hata mamba nao mwishowe wataanza kufa ama wataanza kutafuta chanzo kingine cha chakula pengine ndio maana wameanza kutafuta binadamu wanakwenda ziwani kwasababu wanakuwa na njaa, inabidi wasogee ufukweni wawinde chochote kinachosogea karibu na maji” alifafanua Dk. Kigwangalla. 
 
Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo kufuatia malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa kwake na mbunge wa Jimbo la Songwe, Phillipo Mulugo ambaye amesema kumekuwepo na matukio mengi ya mamba kushambulia na kuuwa wananchi wa vijiji jirani wanaofata huduma mwambao wa ziwa Rukwa. 
 
Katika hatua nyingine Dk. Kigwangalla ametoa miezi mitatu kwa Wakala wa Huduma za misitu Tanzania kuandaa mpango wa kitaifa kwa kila wilaya na vijiji nchini utakaoweka utaratibu maalum wa namna na sehemu wananchi watakayopata huduma ya kuni mkaa.
 
“Utaratibu uwekwe na muuweke nchi nzima, kila wilaya, kila kata, kila kijiji uwekwe utaratibu wananchi watapata wapi mkaa, watapata wapi kuni, kibali cha kuvuna kitapatikana wapi, utaratibu uwe wazi, sio kusubiri kwenye mageti unakamata, hapana weka utaratibu kwanza, ukishaweka utaratibu atakayevunja sheria hata ukimkamata ukimpeleka polisi utakuwa umemrahisishia OCD kazi. 
 
“Kwa sababu hata OCD atakuwa anajua kwamba katika hii wilaya ninayoiongoza hapa ndio mipaka ya mkaa, hapa ni mipaka ya kuni, wewe umetoa wapi, kibali chako kiko wapi, umevunja sheria, mahakamani” ameeleza Dk. Kigwangalla. 
 
Wakati huo huo, Dk. Kigwangalla ametangaza kutaifishwa kwa greda ambalo limekutwa likiwa limetelekezwa na watu wasiojulikana ambao walikuwa wakichimba mchanga wa dhahabu (makinikia) kinyume cha sheria ndani ya Hifadhi ya msitu wa Patamela wakati wa ziara yake wilayani Songwe.
 
Kufuatia tukio hilo, amemuagiza Kamanda wa Polisi wa wilaya hiyo kulinda eneo hilo na kutafuta dereva atakayeendesha greda hilo hadi kituo cha polisi kwa ajili ya kufuata taratibu za sheria za kulitaifisha na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Maleza kata ya Mbangala wilaya ya Songwe mkoani Songwe alipofanya ziara ya kikazi katika kijiji hicho jana kwa ajili ya kutatua mgogoro wa mamba wa ziwa Rukwa ambao wamekuwa wakidhiru wananchi wa kijiji hicho na vijiji jirani.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akitoa agizo la kutaifishwa kwa greda (pichani nyuma) lililokutwa ndani Hifadhi ya Msitu wa Patamela baada ya kutelekezwa na watu watu wasiojulikana waliokuwa wakichimba mchanga wa dhahabu (makinikia) kinyume cha sheria ndani ya Hifadhi hiyo katika wilaya ya Songwe mkoani Songwe jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akitoa maelekezo kwa uongozi wa wilaya ya Songwe kufuatia greda lililokutwa ndani Hifadhi ya Msitu wa Patamela ambalo limetelekezwa na watu wasiojulikana waliokuwa wakichimba mchanga wa dhahabu (makinikia) kinyume cha sheria ndani ya Hifadhi hiyo katika wilaya ya Songwe mkoani Songwe jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akishirikiana na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Songwe kuzima moto uliokutwa ukiwaka ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Patamela wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo jana.
Dk Hamisi Kigwangalla akishirikiana na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Songwe kuzima moto uliokutwa ukiwaka ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Patamela wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo jana.
Juhudi za kuzima moto zikiwa zinaendela.
Dk Kigwangalla akiwa anazungumza na wananchi wa kijiji Maleza.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Songwe, Philipo Mulugo alipokuwa akiwasilisha malalamiko ya wananchi wa jimbo lake ambao wamekuwa wakipata madhara makubwa ya mamba wa ziwa Rukwa.

MAMLAKA HIFADHI YA NGORONGORO KULIPENDEZESHA JIJI LA DODOMA


????????????????????????????????????
Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi na Kaimu Meneja Uhusiano Mamlaka Hifadhi ya Ngorongoro, Joyce Mgaya wakisaini hati ya makubaliano ya kuboresha mandhari ya mizunguko ya magari kwenye barabara kuu za jiji hilo. Kwenye uboreshaji huo wa mandhari Mamlaka Hifadhi ya Ngorongoro itaweka vivutio mbalimbali kutangaza utalii
……………………
Na: Abuu Kimario
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeingia makubaliano na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuboresha mandhari ya mizunguko ya magari (roundabout) kwenye barabara kuu za jiji hilo.
Makubaliano hayo yamefikiwa leo kwenye hafla ya fupi ya kutiliana saini ambapo jiji la Dodoma liliwakilishwa na Meya, Profesa Davis Mwamfupe na Mkurugenzi Mtendaji,  Godwin Kunambi na upande wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro iliwakilishwa na Kaimu Meneja Uhusiano, Joyce Mgaya kwa niaba ya Mhifadhi Mkuu wa mamlaka hiyo Dkt. Fredy Manongi.
Kwenye makubaliano hayo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imekubali kuifanyia ukarabati mizunguko mitatu ya magari ambayo ni mizunguko ya barabara kuu za Dar-es-Salaam (Shabiby), Singida na Arusha.
Akiwasilisha salamu za Mhifadhi Mkuu, Kaimu Meneja Uhusiano Mgaya amesema, uongozi wa jiji la Dodoma kuichagua mamlaka hiyo ni heshima kubwa na wanaipokea kwa mikono miwili na pia mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na halmashauri ya jiji kwenye kuibua fursa mbalimbali za kitalii.
Aidha, Mgaya ameongeza kuwa makubaliano hayo yaliyofikiwa ni fursa ya Halmashauri ya jiji la Dodoma na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kubadilishana uzoefu kwenye maeneo ya uhifadhi wa mazingira na kuboresha mandhari.  
Kwa upande wake Meya wa Jiji la Dodoma, Mstahiki Davis Mwamfupe amesema nia ya uongozi wa jiji la Dodoma ni kulifanya liwe jiji la mfano wa kuigwa na majiji mengine ya Tanzania, barani Afrika na duniani kwa kuwa na mazingira bora kuishi na mandhari yenye kuvutia.
Nae Mkurugenzi Mtendaji, Godwin Kunambi ameishukuru Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kukubali ombi la kutengeneza sanamu kubwa ya tembo kama ishara ya kuhifadhi historia ya chimbuko la jina la mkoa wa Dodoma. Kwa mujibu ya maelezo ya wenyeji wa mkoa huo jina Dodoma limetokana na neno la kigogo “idodomya” baada ya tembo kudidimia ardhini miaka mingi iliyopita.

DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA MOYO WA HEAMEDA MEDICAL CLINIC ATOA USHAURI NAMNA YA KUEPUKA MAGONJWA YA MOYO


1
DAKTARI Bingwa wa magonjwa ya moyo nchini kutoka Heamedia Medical Clinic Dk.Hery Mwandolela akimuelezea mwandishi wa habari mambo mbalimbali yanayosababisha watu kukumbwa na magonjwa ya moyo katika banda la Kliniki hiyo lililopo kwenye viwanja vya maonyesho vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
2
 DAKTARI Bingwa wa magonjwa ya moyo nchini kutoka Heamedia Medical Clinic Dk.Hery Mwandolela akionyesha mfano wa moyo wa binadamu.
3
DAKTARI Bingwa wa magonjwa ya moyo nchini kutoka Heamedia Medical Clinic Dk.Hery Mwandolela akifafanua jambo katika banda hilo kulia ni Julieth Mutabiilwa Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja Heameda Medical Clinic
4
DAKTARI Bingwa wa magonjwa ya moyo nchini kutoka Heamedia Medical Clinic Dk.Hery Mwandolela akizungumza na mmoja wa wananchi waliotaka kupata ufafanuazi mbalimbali wa magonjwa ya moyo alipotembelea katika banda hilo.
……………………………………………………………….
DAKTARI Bingwa wa magonjwa ya moyo nchini kutoka Heamedia Medical Clinic Dk.Hery Mwandolela amesema kuna umuhimu mkubwa wa kila mmoja wetu kuhakikisha anapima afya yake mara kwa mara huku akitaja sababu zinazosababisha ugonjwa wa moyo.
Pia amesema ni vema kila mtu akafahamu namba saba muhimu kwa afya yako na kusisitiza kitendo cha kuchelewa kutambua ugonjwa mapema kunasababisha gharama kubwa zaidi ya ungetambua mapema na kukika ugonjwa husika.
Dk.Hery Mwandolela amesema hayo leo kwenye mahojiano maalum wakati anazungumza kwenye  Maonesho ya Sabasabua  ya Bishara ya kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Amesema lengo la uwepo wake kwenye banda hilo kwanza unalenga kuwakumbusha wananchi mbalimbali kutambua umuhimu wa kupima afya mara kwa mara kwani inasaidia kupunguza gharama za matibabu.
Pia amesema yupo kwenye maonesho hayo kwasababu anataka kuwafahamisha Watanzania huduma bora na za kiwango cha juu katika kutibu magonjwa ya moyo ambayo yaafanywa na madaktari wabobezi waliopo Heameda Medical Clinic iliyopo mtaa wa Fubu maeneo ya Bunju B jijini.
Dk.Mwandolela amesema pamoja na kutoa huduma kwa kiwango cha hali ya juu wameweka gharama nafuu ambazo kila mmoja anaweza kumudu ukilinganisha na maeneo mengine.
Akifafanua zaidi kuhusu kupima afya mara kwa mara amesema magonjwa kama ya kupanda kwa shinikizo la damu na kisukari huweza kuja bila dalili yeyote na wakati mwingine yanagundulika baada ya mhusika kupata madhara makubwa.
“Njia pekee ya kukabiliana na magonjwa haya ni kujenga tabia ya kupima afya zetu hata kama hatusikii dalili zozote za ugonjwa, kwani hii itsaidia kugundua tatizo mapema na kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana nalo.
“Ugonjwa kama kupanda kwa shinikizo la damu hupewa jina muuaji kimya kimya kutokana na tabia yake ya kuwepo bila kuonesha dalili zozote za ugonjwa wakati ukiharibu viungo kama moyo, macho, figo na hata ubongo,”amesema Dk.Mwandolela.
Ameongeza unaweza kuwa na tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu bila kuwa na dalili zozote na njia pekee ni kupima shinikizo la damu.
Amesema kupanda kwa shinikizo la damu bila kudhibitiwa huweza kusababisha madhara makubwa katika moyo, mishipa ya ya damu, macho, figo na ubongo.
“Hivyo tupo hapa katika maonesho pamoja na kutoa ushauri wa masuala ya afya tunaenelimisha Watanzania umuhimu wa kupima afya zao.Ukipima afya mapema ni rahisi kutatatua tatizo kwa kupata dawa za kukinga ambazo gharama yake ni nafuu kuliko dawa za kutibu.
“Ukigundua tatizo mapema ni rahisi kwenda kwa hospitali ukiwa mwenyewe na hivyo hata gharama ya usafiri itakuwa ya kawaida lakini ukichelewa hadi tatizo litokee maana yake itabidi ubebwe na hautaweza kupanda hata daladala, hivyo gharama zitaongezeka.Ndio maana tunashauri upimaji wa afya wa mara kwa mara,”amesema Dk.Mwandolela
Kuhusu afya ya moyo wako , Dk.Mwakandolela amesema ni vema ukaonana na daktari ili kufanya vipimo vitakavyosaidia kufahamu hali halisi ya moyo wako.Endapo huna tatizo lolote ni vizuri kufanya vipimo vinavyokutaarifu kuhusu afya ya moyo na mishipa ya damu angalau kila baada ya miaka miwili.
Akizungumzia namna ya kufahamu namba saba muhimu kwa afya yako , amesema mhusika anatakiwa kufahamu uzito unaokubalika kwa afya bora, kufahamu shinikizo la damu , kufahamu ukubwa wa mzunguko wa kiuno chak na  kiwango cha sukari katika damu.
Pia kufahamu kiwango cha mafuta katika damu na kufahamu kiwango cha mapigo ya moyo wako
Amezungumzia umuhimu wa kufanya mazoezi angalau nusu saa kwa siku, au mara tano kwa juma na kwamba mazoezi hayo yanaweza kuwa ni kwa kutembea, kukimbia ,kuendesha baiskeli, kufanya kazi zinazotumia nguvu na kushiriki katika michezo.
Ametoa rai kwa Watanzania ni vema wakapata muda wa kupumzika, kukabiliana na msongo wa mawazo, kujumuika na unawapenda na kupunguza kiasi cha chumvi kwenye chakula.

MAKAMU WA RAIS KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA AFRIKA NCHINI MAURITANIA


16
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Afrika ya Binadamu na Watu Jaji Imani Mkwawa Aboud wakati wa mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika mjini Nouakchott, Mauritania.
21
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akichangia maoni ya Tanzania juu ya masuala ya Ulinzi na Amani katika nchi za Burundi, Congo DRC, na Sudan ya Kusini wakati wa mkutano wa kawaida wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU)mjini Nouakchott, Mauritania.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
……………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema “Tanzania chini ya Serikali ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli inajitahidi sana kupambana na rushwa pamoja na viashiria vyake”
Makamu wa Rais ameyasema haya wakati wa kujadili Kaulimbiu ya  Umoja wa Afrika kwa mwaka 2018 “Kushinda Vita dhidi ya Rushwa: Njia endelevu ya mabadiliko ya Afrika” katika Mkutano wa kawaida wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika unaomalizika leo mjini Nouakchott, Mauritania.
Makamu wa Rais amesema rushwa inaumiza watu hususani watu masikini na kudhoofisha ukuawaji wa uchumi hivyo ni vyema rushwa ipingwe kwa nguvu zote.
Aidha, Makamu wa Rais amesema Tanzania inatambua vita dhidi ya Rushwa inahitaji jitihada za pamoja katika ngazi zote ikiwemo Kitaifa, Kikanda na Bara zima.
Katika mkutano huo ambao umejadili mambo mbali mbali, Tanzania itaendelea kushiriki katika kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo

TANZIA: MBUNGE MAJIMAREFU AFARIKI DUNIA



MBUNGE wa Korogwe Vijijini (CCM) mkoani Tanga,  Steven Ngonyani maarufu Profesa Majimarefu amefariki dunia leo Jumatatu Julai 2,  2018 usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa za kifo cha mbunge huyo zimethibitishwa na ofisa uhusiano wa Muhimbili, Aminiel Eligaeshi.
Juni 20,  2018 Majimarefu alihamishiwa kwa ndege kutoka mkoani Dodoma kwenda MNH kwa matibabu huku ugonjwa uliokuwa ukimsumbua mbunge huyo haujawekwa wazi.
Juni 6,  2018 mbunge huyo alifiwa na mkewe,  Mariam aliyekuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali hiyo hiyo ya Muhimbili.

Naibu Waziri Mhe.Shonza Atoa Wito kwa Wasanii Nchini kuhamasisha Utalii wa Ndani


Pix 1
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Idara  ya Utalii Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara Bibi. Eva Mallya (kulia) baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara (Lake Manyara National Park) ikiwa ni hatua ya kuhamasisha utalii wa ndani chini ya uratibu wa taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network (TAGOANE)  Jijini Arusha.
Pix 2
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (wa kwanza kulia) akingalia ramani inayonyesha vivutio mbalimbali pamoja na wanyama wanaopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara jana Jijini Arusha  wakati wa ziara ya kutembele hifadhi hiyo, wengine ni Rais wa taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network (TAGOANE) Dkt. Godwin Maimu (katikati) na kulia ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara Bibi. Noelia Myonga.
Pix 3
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) akipokea cover ya tairi la gari lenye nembo  ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara Bibi. Noelia Myonga .
Pix 4
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akisikiliza maelekezo  kutoka kwa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara Bibi. Noelia Myonga kuhusu chemchem ya maji moto ambayo inapatikana katika hifadhi  hiyo alipofanya ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa wasanii na watanzania kwa ujumla lengo ni kuwa na utamaduni wa kutembelea vivutio hivyo .
Pix 5
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akiangalia uoto wa asili ambao hupatikana katika Hifadhi ya Taifa ya  ya Ziwa Manyara wakati wa ziara ya kutembelea hifadhi hiyo hapo jana Jijini Arusha chini ya uratibu wa Taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network (TAGOANE).
Pix 6
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akiwashukuru wasanii na wajasiriamali kutoka Jiji la Arusha ambao aliambatana nao katika ziara ya kuhamasisha  utalii wa ndani, iliyoratibiwa na Taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network (TAGOANE) lengo ikiwa ni kuwajengea watanzania utamaduni wa kupenda kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini ili kukuza uchumi wa nchi.  ( Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha)