Lukuvi atembelea eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex Pugu jijini Dar es Salaa


Mmoja ya Fundi gereji katika Mtaa wa Guluka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam Bw. Mohamed Ali akielezea sababu za wao kuvamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (hayupo pichani).
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsikiliza kwa makini Afisa Ardhi toka Manispaa ya Ilala Bw. Furaha Mwakapalila akielezea historia ya eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex ambalo kwa sasa limevamiwa na mafundi magari wa kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Afisa Tarafa wa Ukonga Bw. Jeremiah Makorere akifafanua jambo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa ziara ya waziri huyo kubaini migogoro mbalimbali ya ardhi katika eneo la Pugu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Guluka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ambao wamevamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Guluka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ambao wamevamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha nguo cha KiliTex.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Msimbazi kata ya Pugu Station jijini Dar es Salaam ambao wamevamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha matofali ya kuchoma cha Kisarawe Brick Factory (KIBRICO) wakati wa ziara ya Waziri huyo kubaini migogoro ya ardhi katika eneo la Pugu.
Mwenyekiti ya Kamati ya malalamiko ya wakazi wa Mtaa wa Msimbazi kata ya Pugu Station jijini Dar es Salaam ambao wamevamia eneo la Kilichokuwa kiwanda cha matofali ya kuchoma cha Kisarawe Brick Factory (KIBRICO) Bw. Deus King΄ung΄alo akisoma risala kwa niaba ya wakazi hao wakati wa ziara ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa ziara ya Waziri huyo kubaini migogoro ya ardhi katika eneo la Pugu.

STARTIMES YAANDAA SHINDANO LA KUKUZA VIPAJI VYA SAUTI DAR,ARUSHA NA ZANZIBAR KESHO

 Picha ikionyesha Tangazo la shindano la kukuza vipaji vya sauti lililoandaliwa na serikali na kampuni ya ving'amuzi ya Startimes ambapo shindano hilo linatarajiwa kufanyika kesho kwenye ukumbi wa Triple A  kwa mkoani Arusha.
  Meneja wa Kampuni ya Startimes Tawi la Arusha pichani akizungumza na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali ofisini kwake ambapo alizungumzia kampuni hiyo kwa kushirikiana na serikali wameandaa shindano la kukuza vipaji vya sauti hapa nchini shindano litakalofanyika katika mikoa Mitatu ya Arusha,Dar es Salaam na Zanzibar.
PICHA JUU NA CHINI  WAANDHISHI WA HABARI WAKIWA KAZINI KUAPATA MATUKIO MBALI MBALI KWENYE OFISI ZA STARTIMES JIJINI ARUSHA LEO .

 Pichani ni viongozi wa kampuni ya Startimes tawi la Arusha wakionyesha baadhi ya zawadi ambazo washiriki na washindi watajinyakulia hiyo kesho kwenye ukumbi wa Triple A jijini Arusha.

 Tv inayoonekana kwenye picha ni zawadi itakayonyakuliwa na washindi wa shindano hilo kesho katika mikoa mitatu ya Dar es salaam,Arusha na Zanzibar.

Picha ikionyesha Tangazo la shindano la kukuza vipaji vya sauti lililoandaliwa na serikali na kampuni ya ving'amuzi ya Startimes ambapo shindano hilo linatarajiwa kufanyika kesho kwenye ukumbi wa Triple A  kwa mkoani Arusha

Na Mahmoud Ahmad Arusha
StarTimes wameanda mashindano ya kusaka vipaji vya sauti kwa watanzania ambapo shindano hilo linaanza leo hapa jijini Arusha,Dar es Salaam na Zanzibar ambapo washindi watano kutoka kila mkoa wataungana  jijini Dar es salaam.
Akizungumza na wanahabari mbali mbali meneja masoko wa kampuni hiyo Ally ngozi alisema kuwa shindano hilo limeandaliwa na kampuni yao madhumuni yakiwa ni kukuza vipaji na kuwapatia ajira washindi.
Ngozi alisema kuwa kampuni hiyo kwa kushirikiana na serikali wameleta shindano hilo la sauti lengo likiwa ni kupunguza tatizo la ajira na kuibua vipaji ambapo mbali na ajira wahindi watajinyakulia Tv,Kingamuzi na simu za mkononi.
Alisema kuwa washiriki wa shindano hilo ni watanzania wote bila kujali umri wa jinsia ambapo kwa Arusha fomu zitatolewa kesho kwenye ukumbi wa Triple A uliopo sakina ambapo pia shindano litafanyikia hap siku hiyo
Aidha alisema kuwa washindi watano watakao patikana watakuwa wamejizolea ajira ya kufanyakazi katika kampuni hiyo.
“Nawasihi wakazi wa jiji la Arusha,Dar es salaam na Zanzibar kuachangamkia fursa hiyo ya kuwa mmoja wa washindi wa shindano letu la kukuza vipaji vya sauti” alisema Ally


MFUKO WA PSPF WATOA ELIMU YA KUJIUNGA KATIKA MFUKO WA KUJICHANGIA KWA HIARI KWA WANANCHI WASIO KATIKA SEKTA RASMIN ZANZIBAR

Afisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Fadhila akizungumza wakati wa Mkutano Taasisi zisizo rasmin za Wavuvi, Madereva wa gari za mchanga, Kifusi na Wakulima wa mbogamboga kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari ya Mfuko wa PSPF uliofanyika katika ukumbi wa Betilyamin Malindi Zanzibar.
Washiriki wa Mkutano huo wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano wakimsikiliza Afisa wa Mfuko wa PSPF akitowa maelezo kuhusiana na Mfuko huo. 
Afisa wa Idara ya Uvuvi na Maendeleo Zanzibar Ndg Mohammed Chum akitowa maelezo wakati wa mkutano huo na Mfuko wa PSPF kwa Wavuvi wa Zanzibar kujiunga na Mfuko huo.
Waziri wa Kilimo Maliasili Uvuvi na Mifugo Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed akifungua mkutano wa Wavuvi na Wananchi wasio kuwa katika Sekta Rasmin kujiunga na Mfuko wa PSPF katika Mafao ya Hiari ili kupata huduma muhimu za maendeleo kupitia mfuko huo. 
Waziri wa Uvuvi Mhe Hamad Rashid Mohammed akisisitiza jambo wakati wa kufungua Mkutano wa Wadau Wasiokuwa katika Sekta Rasmin kujiunga na Mfuko wa PSPF kupitia Michango ya Hiara ili kupata fursa mbalimbali zinazotolewa na PSPF kwa Wanchi wa Tanzania.
Afisa wa PSPF Zanzibar Bi Faidha Katavi akitowa maelezo kwa Waziri wa Uvuvi kujiunga na Mfuko huo baada ya kufungua mkutano huo wa kuwahamashisha Wananchi wasio kuwa katika Sekta rasmin kujiunga na Mfuko wa Kujichangia kwa Hiara Mafao yao na kupata fursa zinazotolewa na PSPF kwa Watanzania.  
Mhe Hamad Rashid akijaza fomu ya Kuchangia kwa Hiari Mfuko wa PSPF baada ya kuufungua Mkutano huo na Wavuvi.
Afisa wa PSPF Bi. Faidha Katavi akitowa maelezo jinsi ya kujiunga na Mfuko wa PSPF Kujichangia kwa Hiara Mafao katika mfuko huo.
Afisa PSPF Ndg. Hadji Jamadari akitowa maelezo jinsi ya kujiunga na Mfuko wa PSPF kwa mafao ya kujichangia kwa hiari kupitia mfuko huo kwa Wananchi wasio katika Sekta rasmin jinsi wanavyoweza kunufaika kupitia kuchangia mafao kwa hiari.
Afisa wa PSPF Ndg Hadji Jamadari akitowa maelekezo kwa Wananchi wanaojiunga katika Mfuko wa PSPF kupitia Michango ya Hiari wakati wa mkutano huo kutowa Elimu ya Mfuko kwa Wananchi wa Zanzibar wasio kuwa katika Sekta Rasmin. 
Afisa wa PSPF Ndg. Hadji Jamadari akitowa maelezo ya moja ya fomu ya kujiunga na Mfuko wa PSPF kupitia Michango ya Hiara kwa Wananchi wasiokuwa katika Sekta rasmin, mkutano huo umewashirikisha Wavuvi, Wachimba Mchanga, Magari ya Mizigo ya Mchanga na Kifunzi na Umoja wa Jumuiya wakulima wa mbogamboga Zanzibar. 
Picha ya Pamoja.

MAABARA ZA GST, TIRDO ZATEULIWA KUTHIBITISHA UBORA WA MAKAA YA MAWE

 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akifafanua jambo katika mkutano na wachimbaji pamoja na watumiaji wa makaa ya mawe (hawapo pichani) uliojadili changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo. Mkutano huo ulifanyika Agosti 24, mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe, akizungumza na wachimbaji pamoja na watumiaji wa makaa ya mawe (hawapo pichani), wakati wa Mkutano baina yao na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).  Mkutano huo ulifanyika hivi karibuni, Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe (kushoto kwa Waziri), wakifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea wakati wa Mkutano baina ya Wizara na wachimbaji pamoja na watumiaji wa makaa ya mawe, uliofanyika Agosti 24 wizarani, jijini Dar es Salaam.
Wajumbe mbalimbali walioshiriki Mkutano baina ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Wachimbaji pamoja na Watumiaji wa Makaa ya Mawe, wakifuatilia mijadala mbalimbali katika Mkutano huo uliofanyika Agosti 24 mwaka huu Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.

TEA KUFADHILI UJENZI WA NYUMBA ZA WALIMU KATIKA MAENEO YASIO RAHISI KUFIKIKA

Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Joel Laurent (wa kwanza kushoto) akijadiliana suala  na viongozi wa Halmashauri ya Kilosa, Mamlaka ya Elimu  Tanzania inatarajia kutekeleza na kufadhili mradi wa kujenga nyumba za walimu kupitia Watumishi Housing Ltd katika Ujenzi katika maeneo yasio rahisi kufikika, katika shule ya Sekondari Uleling'ombe iliyopo Wilaya ya Kilosa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania,Joel Laurent akiongea na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, kamati ya shule ya Uleling'ombe,uongozi wa kijiji cha Uleling'ombe wakijadilana utekelezaji wa Mradi wa kujenga nyumba za walimu katika maeneo yasio rahisi kufikika, katika shule ya Sekondari Uleling'ombe iliyopo Wilaya ya Kilosa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania,Joel Laurent akioneshwa eneo lililotengwa kwa ajili ya kujenga nyumba za walimu katika shule ya Sekondari Uleling'ombe mradi unaotekeleza na kufadhili na Mamlaka ya Elimu Tanzania ikiwatumia Watumishi Housing Ltd katika Ujenzi katika maeneo yasio rahisi kufikika.
Picha ya pamoja.

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Joel Laurent amesisitiza kuwa taasisi yake itaendelea kutafuta rasilimali ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanosoma katika maeneo ambayo ni magumu kufikika wanajengewa miundombuni ili kupata elimu bora.

Mkurugeni Mkuu huyo alisema hayo wilayani Kilosa wakati akikagua eneo la ujenzi wa nyumba ya walimu wa shule ya sekondari ya Uleling’ombe utakaogharimu zaidi ya 148m/- ambayo walimu sita watakaa katika nyumba hiyo.

Alisema mamlaka hiyo imetiliana saini mkataba na Watumishi Housing wa ujenzi wa nyumba za walimu 40 nchi nzima katika maeneo ambayo ni magumu kufikika ili kuhakikisha kuwa walimu wapya wanaopangiwa katika maeneo hayo ambao wengi wamekuwa wakikimbia kufundisha wanapata sehemu nzuri za kuishi.

Aliongeza kuwa katika mwaka huu wa fedha mamlaka yake imetenga bajeti ya kujenga nyumba 30 mwaka huu ambapo ujenzi wa kila nyumba ni miezi mitatu.
“Nyumba hii itakapokuwa tayari na tunategemea ikamilike ifikapo Desemba mwaka huu, itakuwa na uwezo wa kuwaweka walimu sita kuishi katika nyumba hiyo ila tunazitaka halmashauri kuangalia uwezekano wa kuwawekea samani za ndani” alisema.

 
Na pia alisisitiza juu ya umuhimu wa ushiriki wa wananchi na halmashauri hizo katika kuhakikisha kuwa ujenzi wa nyumba hizo unazingatia ujenzi ili ziweze kutumika kwa muda mrefu na hivyo kuwanufaisha wanafunzi wengi zaidi.

TEA ilibuni mradi huo baada ya kugundua kuwa kuna uhitaji maalum wa makazi ya walimu katika mazingira ambayo ni vigumu kufikika ambapo wengi ambao wamekuwa wakipangiwa kufundisha hutafuta uhamisho na hivyo wanafunzi wa maeneo hayo ufaulu wao umekuwa mdogo kutokana na kukosa walimu.

“Walimu wanaokusudiwa kuishi katika nyumnba hizi ni wale wanaoanza kazi ndiyo maana ni chumba na sebule kwa kila mwalimu kwani tunaamini baada ya muda watakuwa wameishazoea na kuweza kujipatia makazi uraiani pale watakapokuwa tayari kuanza familia” Alisema Bw Laurent.

Aliongeza kuwa mamlaka hiyo inajadiliana na wadau mbali mbali ili kuona kama wataweza kuwezesha upatikanaji wa internet na ving’amuzi katika sebule ya pamoja ya nyumba hizo ili wale watakaopangiwa maeneo hayo wasijione kuwa wamepangiwa katika mazingira ambayo si rafiki au wameonewa.

Akizungumza katika ukaguzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Bw Rwegerela Katabaro alisema kuwa wako tayari kushirikiana na TEA japo rasilimali fedha imekuwa ni changamoto kubwa.

Aliomba kuwa katika miradi mingine halmashauri zipewe taarifa za awali ili ziweke kutenga fungu katika bajeti zaona hivyo kuchangia katika juhudi za maendeleo.
Alimhakikishia Mkurugenzi Mkuu huyo juu ya ushiriki wa halmashauri kusimamia kwa karibu ujenzi wa nyumba hiyo ili kupata nyumba ambayo inalingana na thamani ya fedha zilizotengwa.

Aidha ili kuondoa mgongano alishauri TEA itoe muongozo ili kila taasisi ijue jukumu lake katika kuhakikisha kuwa ujenzi wa nyumba hiyo unakuwa bora na kwa viwango walivyokubaliana.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Uleling’ombe, Magashi Shimba alishukuru kwa kupatiwa mradi huo kwani walimu wengi wanaopangiwa huko huwa hawarudi kutokana na mazingira hasa upatikanaji wa makazi.

RC SIMIYU ATOA UFAFANUZI SAHIHI WA TAARIFA KUHUSU WALIMU WAKUU KUVULIWA MADARAKA

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthon Mtaka akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewwa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.

Na Stella Kalinga, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ametoa ufafanuzi wa agizo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata mkoani humo, ambalo Serikali ya Mkoa ililitoa tarehe 17 Agosti ,2016 katika kikao ambacho alipokea Vishikwambi (tablets) 637 kutoka EQUIP Tanzania (Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Nchini) kwa ajili ya Walimu wakuu na Waratibu wa Elimu Kata

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa ufafanuzi huo kufuatia kuwepo kwa taarifa za upotoshaji wa agizo hilo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii., kuwa Mkuu wa Mkoa ametangaza kuwavua madaraka Walimu wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata wote wa Mkoa huo; hali iliyopelekea baadhi ya Walimu wakuu na Waratibu kukosa ari ya kufanya kazi, kwa kigezo cha kusubiri kuvuliwa madaraka.
Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka, 
Mtaka amesema Mkoa ulipokea taarifa za takwimu za wanafunzi hewa, vyumba vya madarasa, idadi ya walimu na idadi ya madawati, baada ya kupokea taarifa hizo ulionekana utofauti mkubwa wa takwimu hizo ndipo Serikali mkoani humo, ikaahidi kupitia mapungufu ya udanganyifu wa takwimu hizo kwa kila shule na kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha Walimu wakuu na Wakuu wa Shule waliodanganya idadi ya wanafunzi.

Aidha, Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu umepata bahati ya kuwa na Mradi wa EQUIP Tanzania ambao umewawezesha waratibu kupata pikipiki na posho, walimu wakuu wamepewa vishikwambi kwaa jili ya utunzaji wa takwimu, hivyo Serikali inao wajibu wa kuangalia mahitaji ya Mkoa katika elimu ambapo alielekeza yafanyike mabadiliko ya Walimu wakuu Msingi, Sekondari na Waratibu wa mkoa mzima.
Katibu wa CWT Mkoa wa Simiyu, Said Mselema(kulia) akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii, kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka. 
“Nililisema mwanzo na leo nalirudia tutafanya mabadiliko makubwa kwa Wakuu wa Shule za Msingi, Sekondari na Waratibu Elimu kata kwa kujiridhisha na maendeleo ya shule zetu, idadi ya walimu waliopo,idadi ya wanafunzi, kiwango cha ufaulu wa wanafunzi na mazingira ya shule ; lakini tutatoa upendeleo kwa shule 10 bora katika kila wilaya kwa Mitihani ya Kitaifa ya Darasa la IV, VII Kidato cha II na IV , hiki ni kipimo kimojawapo cha walimu wa kuendelea nao. Nasisitiza hakuna mtu atakayeonewa wala kufedheheshwa”, alisema Mtaka.

Mtaka amesema azma ya Serikali ni kuibua vipaji vipya vya viongozi wa Elimu katika ngazi ya Wilaya ambapo alisema ameshaagiza Maafisa Elimu wa Wilaya kuwasilisha taarifa ya walimu waliojiendeleza katika ngazi shahada ya kwanza na shahada ya uzamili ili watakaokuwa na sifa waweze kuteuliwa katika nafasi za Walimu wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata ambao watafanyiwa upekuzi (vetting) na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) wa kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewwa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka. 
Sanjari na hilo , Mkuu huyo wa Mkoa amesema Walimu wakuu na Wakuu wa shule wa zamani ni tofauti na wale wa sasa, kwa kuwa sasa hivi wamekuwa maafisa masuuli wa shule zao ambapo wanapokea fedha za Elimu bila malipo kupitia akaunti za shule zao, hivyo ni lazima wapatikane watu waadilifu, wenye sifa na uwezo wa kuongoza shule na kusimamia fedha za Serikali.

Akichangia katika kikao hicho Afisa Elimu (Msingi) Wilaya ya Meatu, George Lowasa ameshauri Uchambuzi wa watu watakaoteuliwa ufanyike katika umakini mkubwa ili wapatikane watendaji wazuri na kuhusu utoaji wa takwimu sahihi alishauri kuwe na utaratibu wa kuziboresha kila (robo) baada ya miezi mitatu ili kuwa na takwimu sahihi pale zinapohitajika.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini amesema Uteuzi huo utazingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya uteuzi ambapo hakuna mtu atakayeonewa au atakayependelewa.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa amesema atawachukulia hatua Maafisa wale wanaolalamikiwa na walimu kwa kuwatolea lugha mbaya kila wanapotoa huduma kwa walimu hao katika Halmashauri za Mkoa huo.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii, kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.

Naye Katibu wa CWT Mkoa wa Simiyu, Said Mselema ameshauri baada ya mabadiliko ya wakuu wa shule na Waratibu wa Elimu Kata kufanyika wale ambao wataonekana hawana sifa za kuendelea kushika nafasi hizo waondolewe kwa staha, ambapo aliomba Serikali ngazi ya Wilaya na Mkoa ikishirikishe chama hicho katika masuala yote muhimu ya kuendeleza sekta ya Elimu, kwa kuwa wanamsaidia mwajiri katika usimamizi wa utendaji kwa walimu.

Kikao hicho cha wadau kilichofanyika mjini Bariadi na kimewahusisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, Maafisa Elimu kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Simiyu pamoja na Wenyeviti na Makatibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ngazi ya Mkoa na Wilaya.