Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alipokutana na viongozi wa dini mbali mbali katika Ofisi ya Mufti Zanzibar, kuendeleza mazungumzo ya kumaliza mkwamo wa kisiasa Zanzibar (Picha na OMKR)
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alipokutana na viongozi wa dini mbali mbali katika Ofisi ya Mufti Zanzibar, kuendeleza mazungumzo ya kumaliza mkwamo wa kisiasa Zanzibar (Picha na OMKR)
MVUA ILIYONYESHA JIJINI MWANZA YASABABISHA MAAFA IKIWEMO VIFO NA UWANJA WA NDEGE KUFUNGWA KWA MUDA.
posted on
Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Kanda ya Ziwa ikiwemo JijiniMwanza, zimesababisha Uwanja wa ndege wa Jiji hili kufungwa kwa muda wa masaa matano kutokana na kujaa maji.
Meneja wa Uwanja huo Easter Madale alisema kuwa shughuli za usafirishaji uwanjani hapo, hii leo zilikwama kuanzia majira ya saa tatu asubuhi hadi saa nane mchana, baada ya maji ya mvua kujaa katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la kukimbilia ndege.
Alisema kuwa tatizo la maji kujaa uwanjani hapo halikusababishwa na ubovu wa miundombinu, bali ni kutokana na uwanja huo kuzungukwa na vilima vipatavyo saba ambavyo wakati wa mvua za masika hutiririsha maji ambayo huingia hadi uwanjani.
Madale alibainisha kuwa mara ya mwisho maji kujaa uwanjani hapo ilikwa mwaka 2012 na kwamba tatizo hilo lilishughulikiwa kwa kujengewa mifereji mikubwa kwa ajili ya kuzuia maji kuingia katika uwanja huo huku akiongeza mvua iliyonyesha leo imesababisha mifereji na mitarokuharibika.
Baadhi ya wasafiri wamelalamikia hali hiyo kwa kile walichoeleza kuwa ni ratiba zao za kusafiri kwa ajili ya shughuli zao kukwama na hivyo kuingia kupata usufumbu mkubwa.
Katika hatua nyingine,Mvua hiyo zimesababisha athari mbalimbali kwa wakazi wa Jiji la Mwanza wakiwemo wakazi wa Kihewa, baada ya nyumba zao kujaa maji na hivyo baadhi ya kaya kuhifadhiwa katika shule ya Msingi Kilimahewa.
Kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza Charles Mkumbo, mvua hiyo imesababisha vifo vya watu wawili, mmoja akifahamika kwa jina la Zainab Shaban (18) ambae alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya SekondariNyamanoro aliesombwa na maji wakati akijaribu kuwahi kwenye mtihani wa kuhitimu
kidato cha nne pamoja na dereva pikipiki ambae jina lake halikufahamika mara moja.
Alfajiri ya leo Jiji la Mwanza lilikumbwa na mvua ambayo ilidumu kwa zaidi ya masaa matano, hali iliyosababisha adha mbalimbali kwa wakazi na wageni wa Jiji hili.
Hata hivyo Meneja wa Mamlaka ya hali ya hewa Kanda ya Ziwa Augustino Duganda amebainisha kuwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa itaendelea kuwa na mvua nyingi hadi kufikia mwezi wa 12 mwaka huu hivyo ni vyema wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi ikiwemo yenye mafuriko na mkondo wa maji wakahama kutoka kwenye maeneo hayo ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.
Kidume mmoja mwenye tabia ya kulala kila anapozidiwa na kilevi huko Swansea nchini Uingereza, amepewa dawa ya kutosinzia wala kulala tena kwenye baa pale anapokuwa amelewa.Dawa aliyopewa kidume huyo na rafiki zake, ni kuchorwa tatoo ya miwani aina ya Ray-Ban kwa wino maalumu wa kuchorea tatoo ambao haufutiki kwa sabuni wala dawa nyepesi za kuondoa michoro mwilini.
Kabla ya kadhia hiyo, ambayo imemfanya njemba huyo kupandwa na hasira na kumtafuta kisirisiri rafiki yake aliyemchora tatoo hiyo, jemba huyo na rafiki zake walitoka na kwenda kwenye baa moja ili kupata kilevi cha jioni.
Ni baada ya kupata glasi mbili tatu za kilevi ndipo kidume huyo kama kawaida akapitiwa na usingizi na hapo mmoja wa rafiki zake akaamua kumchora tatoo ya miwani ya Ray-Ban usoni na kumfanya aonekane kama aliyevaa miwani.
Ilibidi kidume huyo atumie kiasi kikubwa cha fedha ili kuondoa wino wa tatuu hiyo kwenye kliniki moja ya urembo huko Swansea na sasa ameacha kunywa na kundi la marafiki huku akimtafuta kimyakimya rafiki aliyemchora tatoo.
Usiku mzuri wa jana kwa klabu ya Tottenham katika dimba la White Hart Lane uliisha kwa shari baina ya Andros Townsend ambaye alionekana akikwaruzana na kocha wa viungo Nathan Gardiner baada ya kumalizika mchezo huo.
Winga huyo wa kimataifa wa timu ya taifa ya Uingereza, ambaye alikuwa ni mchezaji wa akiba ambaye hakutumika wakati timu yake ya Tottenham kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Aston Villa.
Townsend alisugua benchi na kujikuta akiishia kuangalia kocha Mauricio Pochettino akimuingiza kiungo kinda Josh Onomah, kutoka benchi.
Andros Townsend akisukumana na kocha wa viungo Nathan Gardiner
Andros Townsend akijibizana na kocha wa viungo Nathan Gardiner
Kundi la wapiganaji wa Kiislam la Boko Haram limetoa picha zinazoonyesha wakiwa na kiwanda cha kutengeneza makombora ya roketi kaskazini-mashariki mwa Nigeria.
Kundi hilo limekuwa likitumia makombora ya roketi katika mashambulizi yake siku za nyuma na Wanaigeria wengi walikuwa wakihoji Boko Haram wanaizitoa wapi silaha hiyo..
Picha hizo zinaashiria kuwa wapiganaji wa Boko Haram wanaujuzi wa kutengeneza makombora ya roketi katika kiwanda hicho.
NAIBU KATIBU MKUU MPYA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AANZA KAZI RASMI NA KUWATAKA WATUMISHI KUTEKELEZA KAULI MBIU YA “HAPA KAZI TU”
posted on
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi aliyeteuliwa hivi karibuni, John Mngodo, akijitambulisha kwa Watumishi mara baada ya kuanza kazi rasmi katika Wizara hiyo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Lilian Mapfa na kushoto ni Mwenyekiti wa TUGHE, Obedi Mbaga.
MSIMAMIZI WA PROGRAMU YA AFRICAN DREAM KUTOKA SHIRIKISHO LA MCHEZO WA WAVU AFRIKA (CAVB) ATEMBELEA WIZARA YA HABARI
posted on
Msimamizi wa Programu ya “African Dream” kutoka CAVB ( Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Wavu Afrika) Paul Bitok wa pili kutoka kulia akimuuliza jambo Katibu Mtendaji wa Chama cha Mpira wa Wavu nchini ( TAVA) Bw. Allen Alex alipotembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kujadiliana juu ya maendeleo ya mchezo huo nchini,Wa kwanza kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Olimpiki Tanzania Bw. Muharam Mchume Picha na Benjamin Sawe
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Juliana Yassoda wa pili kutoka kushoto akimuelezea Msimamizi wa Programu ya “African Dream” kutoka CAVB ( Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Wavu Afrika) Paul Bitok jinsi Serikali inavyoshirikiana na Chama cha Mpira wa Wavu nchini katika kukuza mchezo huo.Picha na Benjamin Sawe
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Olimpiki Tanzania Bw. Muharam Mchume wa kwanza kushoto akimuelezea Msimamizi wa Programu ya “African Dream” kutoka CAVB ( Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Wavu Afrika) Paul Bitok wa pili kutoka kulia jinsi wanavyoshirikiana na Serikali katika kukuza mchezo huo.Msimamizi yupo nchini kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya mchezo huo. Picha na Benjamin Sawe
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Juliana Yassoda wa pili kutoka kushoto akimuelezea Msimamizi wa Programu ya “African Dream” kutoka CAVB ( Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Wavu Afrika) Paul Bitok jinsi Serikali inavyoshirikiana na Chama cha Mpira wa Wavu nchini katika kukuza mchezo huo.Picha na Benjamin Sawe
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)






