Usiku mzuri wa jana kwa klabu ya Tottenham katika dimba la White Hart Lane uliisha kwa shari baina ya Andros Townsend ambaye alionekana akikwaruzana na kocha wa viungo Nathan Gardiner baada ya kumalizika mchezo huo.
Winga huyo wa kimataifa wa timu ya taifa ya Uingereza, ambaye alikuwa ni mchezaji wa akiba ambaye hakutumika wakati timu yake ya Tottenham kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Aston Villa.
Townsend alisugua benchi na kujikuta akiishia kuangalia kocha Mauricio Pochettino akimuingiza kiungo kinda Josh Onomah, kutoka benchi.
Andros Townsend akisukumana na kocha wa viungo Nathan Gardiner
Andros Townsend akijibizana na kocha wa viungo Nathan Gardiner
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni