Polisi nchini Misri wamepata miili
ya wahamiaji 15 wa Afrika ambao inaonekana walipigwa risasi na kufa
kaskazini mwa Penisula ya Sinai.
Pia wahamiaji wanane wamepatikana
hai lakini wamejeruhiwa. Haijafahamika kuwa nani alilishambulia kundi
hilo karibu na mji wa Rafah mpakani mwa Gaza.
Kumekuwa na hali ya hofo katika eneo
hilo, ambalo jeshi la Misri linapambana wanamgambo wa kundi la Dola
ya Kiislam (IS).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni