Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
ametangaza kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri na kufanya
mabadiliko ya muundo wa serikali yak e kufuatia kugubikwa na rushwa.
Katika mabadiliko hayo aliyoyafanya
baada ya mawaziri sita kujiuzulu kwa tuhuma za rushwa rais Kenyatta
pia ameongeza wizara kutoka 19 na kuwa 20 idara za serikali kutoka 26
hadi 41 ili kuongeza ufanisi.
Katika mabadiliko hayo rais Uhuru
Kenyatta amewatimua kazi mawaziri watano ambao walisimamishwa kazi
kutokana na kukabiliwa na tuhuma za rushwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni