Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Mhe. Damian Lubuva
Na Lilian Lundo – Maelezo
Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Mhe. Damian Lubuva
ametangaza idadi ya wabunge wa Viti Maalum leo katika ukumbi wa ofisi za
Tume hiyo jijini Dar es Salaam.
Idadi ya Viti Maalum iliongezeka na kufikia asilimia 40 mwaka 2010 kwa mujibu wa uamuzi wa Serikali.
“Katika
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 viti maalum idadi yake ni 113, kutokana na
kuwepo majimbo 8 ambayo hayakufanya uchaguzi mgawanyo wa Viti Maalum kwa
sasa ni 110, viti 3 vilivyobaki, vitagawanywa baada ya kufanyika kwa
uchaguzi katika majimbo hayo.” Alisema Jaji Lubuva.
Jaji Lubuva alisema kuwa, vyama ambavyo vimekidhi vigezo vya kikatiba na kisheria na kupata angalau asilimia 5 ya kura zote halali za wabunge ndio vitakavyo kuwa na wabunge wa Viti Maalum.
Huku
idadi ya wabunge Viti Maalum kutoka katika vyama vinategemea na idadi
ya kura halali za wabunge ambavyo vyama hivyo vimepata.
Kutokana na matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini mwishoni mwa mwezi Oktoba, idadi ya kura halali ya wabunge kwa vyama vitatu vilivyopata angalau asilimia 5 ni CCM kura 8,333,953 imepata jumla ya Viti Maalum 64, CHADEMA kura 4,627,923 imepata jumla ya Viti Maalum 36 na CUF kura 1,257,051 imepata jumla ya Viti Maalum 10.
Majina ya Wabunge wa Viti Maalum yatapatikana katika vyama husika kwa mujibu wa orodha iliyowasilishwa Tume na kila chama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni