Mmoja
wa watoto waliofika katika ofisi za Kijiji cha Maweni kwa ajili ya
kuhudhuria Kliniki tembezi kutoka katika Hospitali ya misheni ya
Kilimatinde,wilayani Manyoni akipimwa uzito na wahudumu wa afya wa
Hospitali hiyo.
Watoto
wakisalimiana wakati wakisubiri kupatiwa huduma za chanjo kutoka kwa
wataalamu wa afya kutoka katika Hospitali ya misheni ya
Kilimatinde,wilayani Manyoni.
Jengo
la zahanati inayojengwa kwa nguvu za wananchi ambayo itakapokamilika
inatarajia kutumia zaidi ya shilingi milioni mia moja.
Uenzi
wa nyumba ya mtumishi wa zahanati inayojengwa kwa nguvu za wananchi wa
Maweni ambayo bado inahitaji nguvu kubwa kukamilika.
Na, Jumbe Ismailly, Manyoni
WANAWAKE
wajawazito wa Kijiji cha Maweni, wilayani Manyoni, Mkoani Singida
wamekuwa wakipoteza maisha yao kwa kwenda kufuata huduma za afya ya
uzazi kwa wakunga wa jadi waliopo umbali wa zaidi ya kilomita kati ya 30
hadi 40 kutokana na kijiji hicho kutokuwa na kituo cha afya au zahanati
tangu nchi ilipopata uhuru.
Hayo
yalibainishwa na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Maweni kwenye
mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hizi aliyetaka kufahamu sababu
za ujenzi wa zahanati ya Kijiji hicho kutokamilika licha ya kupauliwa
kwa muda mrefu hivi sasa.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wananchi hao, Joyce Karikawe alisema kwa muda mrefu
sasa akina mama wajazito hawana huduma za afya jambo linalowafanya
watembee umbali mrefu kutoka katika Kijiji hicho hadi kwenye Hospitali
ya misheni ya Kilimatinde umbali wa takribani kilomita zisizopungua 30.
Aidha
Karikawe alifafanua kwamba pamoja na kufuata huduma hizo Kilimatinde
lakini bado kuna baadhi yao wamekuwa wakienda kujifungulia kwa wakunga
wa jadi waliopo kwenye maeneo ya kata hiyo,ambayo hata hivyo hupata
matatizo makubwa sana,ikiwemo kupoteza maisha yao.
Kutokana
na adha hiyo inayowapata wanawake na wananchi kwa ujumla wa kijiji
hicho,Karikawe alibainisha kwamba kumewalazimu kufikia maamuzi ya
kujenga zahanati katika Kijiji hicho itakayowawezesha kukabiliana na
vifo vya akina mama wajawazito vinavyotokana na kutembea umbali mrefu
kufuata huduma hizo.
Naye
mkazi wa Kijiji cha Maweni, Jacobo Jacksoni Karikawe alifafanua kuwa
tatizo la kukosekana kwa zahanati katika Kijiji hicho ni la muda mrefu
tangu nchi ilipopata uhuru wake,lakini kutokana na jitihada za diwani
wao waliomchagua mwaka 2010 hadi 2015,aliwaonyesha moyo na kuwatia nguvu
hadi wameweza kuinua jengo hilo la zahanati.
“Lakini
jengo hili bado halijakamilika, jengo hili tunaomba msaada kutoka
serikalini kwa sababu kuna akina mama wanatoka umbali wa kilomita 15
hadi 20 wanapata matatizo wengine wanajifungulia njiani”alisisitiza
Karikawe.
Hivyo
mwanachi huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa kuchaguliwa
kutosahau ahadi wanazowaahidi wananchi wakati wa kampeni za auchaguzi
ili waweze kurejesha imani kwa serikali na kuonya kwamba kutotekelezwa
kwa ahadi kunachangia wananchi kutokuwa na imanai na vyama vya siasa
wakati wa kuomba kura.
Kwa
upande wake Yustasi Wilsoni Mahajile aliweka bayana kuwa kutokana na
kukosekana kwa huduma hiyo muhimu imekuwa vigumu kwao kukutana na
vidonge Kijijini hapo,zaidi ya kwenda kuvifuata kwenye vijiji jirani cha
Mvumi,Kintinku hali inayochangia magonjwa ya milipuko pamoja na idadi
kubwa ya wagonjwa kupoteza maisha yao.
“Yaani
ukishakosa huduma ya afya ina maana magonjwa ya milipuko yanaweza
yakatokea na wallio wengi tunakufa,halafu yaani unapokosa dawa ina maana
kwamba unatarajia kifo kwa hivyo ukipata zahanati itakuwa ni kimbilio
la kuweza kupata maisha pale”alifafanua.
Hata
hivyo kwa upande wake aliyekuwa diwani wa kata hiyo ambaye pia
ameshinda katika uchaguzi uliofanyika okt, 25,mwaka huu, Abduli Mwengwa
alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015/2016 Halmashauri ya
wilaya ya Manyoni imetenga zaidi ya shilingi milioni 30 kwa ajili ya
kusaidia kukamilisha ujenzi wa zahanati ya Kijiji hicho.
Kaimu
ofisa mtendaji wa Kijiji cha Maweni,Merina Nyambuya alisema ujenzi wa
zahanati ya Kijiji hicho ulioanza mwaka 2012 kwa nguvu za wananchi
unatarajia kutumia zaidi ya shilingi milioni mia moja utakapokamilika na
kwamba mpaka sasa lilipofikia hatua ya umaliziaji limetumia zaidi ya
shilingi milioni 41.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni