Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Benki ya
CRDB imeendelea kukuza kipato cha familia nyingi nchini za hali ya chini ,kati
na juu kwa kuwahimiza wateja wake kufanya uwekezaji wenye tija pamoja na
kujiwekea akiba kwa maisha ya baadae.
Hayo
yameelezwa Meneja wa Benki ya CDRB tawi la Usa lilipo mkoani Arusha Jenipher Tond wakati wa maadhimisho ya siku ya Familia ya
CRDB iliyofanyika katika viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha na
kuzikutanisha familia mbalimbali za wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na familia
za wateja wa benki hiyo waishio jijini Arusha.
Meneja huyo
amesema kuwa benki hiyo inaendelea kuhamasisha uwekezaji na kutoa mikopo kwa
ajili ya kukuza mitaji na kuinua pato la mwananchi mmoja mmoja hadi kwa taifa.
Meneja wa
benki hiyo tawi la Meru Leonce Mathey amesema kuwa benki hiyo imesogeza karibu
huduma kwa wananchi ikiwemo boda boda ,mama ntilie pamoja na wajasiriamali kwa
kuanzisha matawi katika maeneo ya masoko .
Leonce
amewataka wafanyakazi wa CRDB kutumia vyema siku familia kwa kukaa karibu na familia zao na kufurahi
pamoja kwani muda mwingi wanautumia katika kufanya kazi za kuwaingizia kipato .
“Kama kwenye
familia mambo hayako vizuri nyumbani hata kazini mambo hayatakua vizuri ni vyema kuhakikisha
mazingira yanakua mazuri kuanzia kwenye familia mpaka kazini” Alisema Leons
Kwa upande
wake Mteja wa benki hiyo Pendo Shoo amesema kuwa benki hiyo imemsaidia
kuwalipia watoto wake ada kupitia akaunti ya Junior Acount ambazo huwawezesha
pia kupata mikopo kwa ajili ya kuwaendeleza watoto kielimu.
Benki ya
CRDB ina matawi 8 na matawi mengine
madogo madogo bado yataendelea kuanzisha ili kusogeza huduma za kibenki karibu
na wananchi.
Siku ya
familia ya CRDB iliambatana na michezo na burudani
ambazo zilipamba siku hiyo ikiwemo mchezo wa kuvuta kamba ,kukimbia na
yai mdomoni pamoja na burudani ya muziki .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni