Msako mkali unaendelea wa kutafuta
wafuasi wa kundi la Dola ya Kiislam (IS) walionusurika wakati wa
mashambulizi ya kigaidi siku ya Ijumaa yaliyouwa watu 129 Jijini
Paris nchini Ufaransa.
Polisi wamemtaja Salah Abdeslam,
mwenye umri wa miaka 26, kuwa ni mtuhumiwa muhimu, ambaye
alisimamishwa na polisi siku ya mashambulizi na kuachiliwa aende.
Wakati huo huo ndege za kivita za
Ufaransa zimeshambulia ngome kuu ya kundi la Dola ya Kiislma nchini
Syria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni