Kocha
mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania bara ‘Kilimanjaro Stars’, Abdallah
Kibadeni ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kujiandaa na michuano ya
Kombe la Chalenji itakayoanza kutimua vumbi Jumamosi Novemba 21, nchini
Ethiopia.
Kibadeni anayesaidiwa na kocha msaidizi Juma Mgunda,
amesema wachezaji aliowaita wapo katika hali nzuri na wamekua wakifanya
mazoezi na kikosi cha Taifa Stars ambapo wao kama benchi la ufundi
wamepata nafasi ya kuwa nao kwa muda mrefu na kutambua maendeleo yao.
“Tumechagua
wachezaji kulingana na mahitaji ya timu, tumekua na wachezaji hawa kwa
muda mrefu katika vipindi mbalimbali, tuna amini tuliowachagua watafanya
vizuri katika michuano hiyo mikongwe barani Afrika” amesema Kibadeni.
Wachezaji
walioitwa ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam),
Said Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi Shomari Kapombe (Azam), Hassan
Kessy (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Hassan Isihaka (Simba), Salim
Mbonde (Mtibwa), Juma Abdul (Yanga) na Kelvin Yondani (Yanga).
Viungo
Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Said Ndemla (Simba), Salum
Telela (Yanga), Salum Abubakar (Azam), Deus Kaseke (Yanga),
washambuliaji John Bocco (Azam), Elias Maguri (Stand United), Ibrahim
Hajibu (Simba), Malimi Busungu (Yanga) na Saimon Msuva (Yanga).
Michuano
ya Kombe la Chalenji inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 21 na
kumalizika Disemba 6, ambapo Kilimanjaro Stars imepangwa kundi A, lenye
wenyeji Ethiopia, Rwanda na Somalia.
Wachezaji Said Mohamed,
Juma Abdul, Hassan Kessy, Hassan Isihaka, Salum Abubakar na Ibrahim
wanaendelea na mazoezi jijini Dar es salaam chini ya kocha msaidizi Juma
Mgunda wakati wanawasubiri wachezaji wengine walioko nchini Algeria na
kikosi cha Taifa Stars.
Kundi B lina Bingwa Mtetezi Kenya,
Burundi, Uganda na Zanzibar, huku kundi C likiundwa na timu za Sudan,
Sudani Kusini, Djibouti na waalikwa wa michuano hiyo timu ya taifa
kutoka Malawi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni