Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari
nje ya ukumbi wa NEC ,CCM Makao Makuu Dodoma akiwa ameshikilia kitabu
cha Kanuni za Kamati ya Wabunge Wote wa Chama Cha Mapinduzi.
Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika kikao chake cha siku moja
kilichofanyika leo Novemba 15, 2015 mjini Dodoma imewateua wana-CCM
watatu watakaopigiwa kura na wabunge wote wa CCM ili kumpata mgombea wa
CCM katika nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Walioteuliwa
kugombea nafasi hiyo na Kamati Kuu iliyofanyika chini ya Mwenyekiti wa
CCM, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni pamoja na Naibu Spika
aliyemaliza muda wake Ndugu JOB NDUGAI, Dkt. TULIA ACKSON na Ndugu
ABDULAH MWINYI.
Kwa
upande wa Naibu Spika wa Bunge, mchakato wa kuchukua fomu kwa wabunge
wa CCM wanaoomba ridhaa kugombea nafasi hiyo utaanza kesho Novemba 16,
2015 na kukamilika Novemba 17, 2015 saa kumi kamili jioni.
Wana-CCM
hao watatu watapigiwa kura na Kikao cha Kamati ya Wabunge wote wa CCM
kitakachofanyika kesho Novemba 16, 2015 saa nne asubuhi katika ofisi za
Makao Makuu ya CCM Dodoma ilikuchagua jina moja kugombea nafasi hiyo
katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Kuhusu
nafasi ya Naibu Spika, alisema kulikuwa na kasoro za kutofuata kanuni
za chama ambapo hadi jana ni mwanachama mmoja tu ndiye
aliyekuwa amechukua fomu ya kugombea ambaye ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan ‘Zungu,’ lakini atatakiwa kuchukua fomu upya.
“Ibara
ya 57, Kanuni za kamati ya wabunge wote wa CCM toleo la 2010 toleo la
nne 2011, mbunge yeyote anayetaka kugombea nafasi ya Naibu Spika
atatakiwa kuchukua fomu kupitia kamati hiyo na atairudisha kisha kamati
itakaa kupata jina moja,” alisema Nape.
Kwa
mujibu wa maelezo hayo mbunge wa chama hicho anayetaka kugombea Unaibu
Spika, atatakiwa kuchukua fomu leo Novemba 16, kwa ada ya Sh
100,000 kisha atairudisha kesho Novemba 17, ndipo kamati itakaa kuchambua na kupitisha jina moja.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni